MUHIMU KWA VIJANA WENZANGU.!
MUHIMU KWA VIJANA WENZANGU.!Wengi itakuwa bado miaka miwili, mitatu au minne kabla ya kutimiza miaka 30. Natambua kuwa kuna waliokwisha fikisha na kuna uwezekano kuna walio nyuma kidogo.
Kama katika umri tulionao sasa kuna mtu anakuambia wewe bado ni mdogo/mtoto, basi huyo mtu hakupendi na anakulemaza kiakili. Kua! Acha utoto! Mambo yafuatayo kwa vigezo vya kibinadamu mwenye akili timamu, mtu mwerevu lazima uwe ushayatimiza.
1) Kuweka misingi ya kifamilia:
Katika umri huo unatakiwa uwe umeoa, umechumbia au uko katika uhusiano wenye kueleweka unaelekea kwenye kujenga familia. Kama katika umri huu bado unabadilisha wanawake na kudandia vicheche, basi sahau kuwa na familia imara. Mambo yafuatayo yatakuwa yanakunyemelea;
- Kuoa/kuolewa msichana/mvulana mdogo sana ambaye atakuona unamzeesha
- Kuoa /kuolewa chapchap bila kuwaza
-Kuokoteza magonjwa ya hatari
- Kunogewa na usela na kusahau kuoa/kuolewa
2)Kujitegemea kiuchumi:
Hapa simaanishi kufanya kazi na kupata mshahara pekee, la hasha! Hapa nalenga wale watoto wa mama ambao pamoja na kuwa wana kazi na mishahara, bado wanalalama mishahara haitoshi na kukimbilia kuomba hela nyumbani wanapoishiwa mara kwa mara. Wale ambao bado wanakaa nyumbani hii inawahusu pia. Pia wale wanaotumia 100% ya mishahara kununua vitu vinavyoisha (consumption) wakingoja wapate hela nyingi au wazazi, ndugu na jamaa wawasaidie kwenye uwekezaji. Africa tunachelewa sana kwenye hii sector.
3) Kuwa na kitega uchumi:
Kama unadhani mshahara wako wa milioni kadhaa ni mwingi sana, ngoja augue mtu wa karibu au wewe mwenyewe halafu daktari akuambie mgonjwa wako/wewe ana/unatakiwa ape/upelekwe nje ya nchi kwa matibabu zaidi wakati huna bima ya afya inayolipia hilo ndo utajijua kama mshahara wako heshima yake inaishia samaki samaki au inavuka border. Kitega uchumi si lazima uwe na mkampuni mkubwa, la hasha! Ila uwe na kitu cha kueleweka na chenye malengo ya kukua kuwa kitu cha maana. Kwa wale wagumu kuelewa, UNATAKIWA UWE NA PATO LA PEMBENI NJE YA MSHAHARA.
4) Makazi:
Uwe hata na kiwanja hapo Bunju Arif! Huezi kunywa bia kila weekend halafu wenzio wakiongelea issues za nyumba/viwanja/mashamba yao unakimbilia kubadilisha mada (Eti Huyu LVG wamuondoe kabisa anaharibu timu). Kumbe unazuga kupotezea story za viwanja/nyumba.
5)Uwe na professional qualification
: ACCA,CPA,CFA,CSIA,CPB, LAW SCHOOL ETC wale wa procurement wana ya kwao n.k. Ikifika huu umri kama CPA imekataa, tafuta hata mitihani za marketing upige, CPA sio issue zako. Lazima uwe na defined career (Kama hukubahatika kwenda kidato kingi, uwe na namna ya halali na ya kudumu ya kukupatia kipato). Umri huu kama huna utaalam katika fani yako, jiandae kuwa frustrated ofisini. Madogo wanasoma jamaa angu! Halafu wako tayari kupewa salary ndogo wapige kazi kuliko wewe.. So take care!
6) Uwe ushaamua ka hicho kitambi unakiondoa au unakilea:
Hapa sichekeshi! Kitambi kina madhara mengi. Suruali haikai vizuri, UTAPIGIWA, Kisukari, pressure n.k. Ukikinyamazia muda huu jua kitakuwa kishakomaa na majukumu yatakuwa mlima. Ukikiachia kijiamulie, kitakuganda kama "roba ya mbao" till death does you apart! Kama unakipenda endelea nacho, kama hukipendi uwe ushaweka program ya kukiondoa.
7)Uwezo wa kusaidia wanaokutegemea:
Kama we ni wa kishua, hapa hapakuhusu. Wewe ambaye si wa kishua, wazazi walikuwa na mategemeo flani walipokuwa wanakusomesha. Kama umefika miaka 30 hujaanza kuyatimiza mategemeo yao bila sababu ya msingi, jua watakuwa washakata tamaa na wewe.
8) Uwe na busara.
Kuwa mtu wa kufikiri kabla ya kutenda. Tengeneza haiba nzuri na ya kuheshimika kwa wanaokuzunguka. Kama huna busara hadi umri huu basi we sahau suala la busara ukiwa hai.. Labda utakutana nayo akhera.!
9) Savings:
Hapa nimeweka kizungu kuonyesha msisitizo. Kila mtu ana kipato chake. Ila formula ni kwamba angalau uwe ushahifadhi fedha sawa na mishahara yako ya mwaka na nusu gross of Tax kwa kipindi hicho. Kwa wale wagumu kuelewa namaanisha Ukiacha kazi au kusimamishwa kazi, uwe na uwezo wa kukaa mwaka na nusu bila kuingiza kitu chochote lakini uendelee kuishi maisha yale yale.
10) Umjue Mungu:
Nimeliweka hili mwisho si kwamba ni la mwisho kwa umuhimu, La hasha! Ni ili ulikumbuke zaidi. Mjue Mungu, mpende na umuogope. Nenda ibadani, soma neno lake na umuombe. Uwe na desturi ya kusali nyumbani kwako angalau kila unapoamka na wakati wa kulala. Kama humuogopi Mungu katika umri huu, basi wewe kwenda Mbinguni ni ngumu kuliko ngamia kupenya tundu la sindani (hata kama ni masikini).
www.karibumbeya.com
0 comments: