Mfalme asiye na jicho moja

21:43:00 Unknown 0 Comments

Hapo zamani kulikuwa na mfalme aliyekuwa hana
jicho moja na mguu mmoja.....
Siku moja akawakusanya wachoraji wote pale
nchini kwake na kuwa ambia wachore picha nzuri
ya yeye...Lakini wale wachoraji wote wakashindwa
kuichora-- Wangewezaje kuichora picha nzuri
wakati mfalme ana kasoro katika jicho na mkuu?
Lakini kwa bahati nzuri mmoja kati ya wachoraji
wale akaamua ajitose na kuchora picha ya
mfalme.
Ilikuwa ni picha nzuri iliyomshangaza kila mtu
pamoja na wachoraji wenzake....
Alischora picha Nzuri ikimwonyesha mfalme
anataka kuwinda na jicho moja kalifunga na
jingine kaliweka kwenye lensi ya bunduki na
mguu mmoja ameukunja
Funzo :
Kwa nini tusichore picha kamahizi kwa
wengine.Kuficha mapungufu ya wenzetu na
kuonyesha mema yao.
Wengi tumekuwa wepesi wa kuonyesha madhaifu
ya wenzetu kuliko mazuri yao

You Might Also Like

0 comments: