Mshtakiwa unamaelezo yoyote?

14:51:00 Unknown 0 Comments

Mshikaji alijikuta yuko mahakamani kwa kosa la kuiba gari. 

HAKIMU: Mshtakiwa unamaelezo yoyote?

MSHKAJI: Mzee, hawa jamaa wamenibambikia kesi, ishu nzima ilianza nilipokuwa pale masikani kwetu naosha
magari kama kawa. Yule maza pale akaja na ndinga lake la nguvu, akaniambia nilioshe, mi nikalipiga maji kisawasawa, huyu maza akanambia niiingie kwenye gari yake kuna ishu muhimu, akanichukua mpaka pale Mwenge, akaniambia nichague viwalo, nikachagua nguo za nguvu akalipa, akanambia nimsindikize
home kwake, tukasepa, nikafika kwake, mjengo wa nguvu, akanambia nioge nikaoga fresh, ile natoka bafuni akanipa msosi wa nguvu nikashushia na mzinga wa Nyagi, kisha akaniita chumbani kwake, akasaula akajitosa
kitandani, kisha akanambia, "
 Mpenzi nimekupenda sana, nimekuridhia kila kitu, chukua unachotaka"

 Basi kusikia hivyo mzee wangu nikacheki kushoto , nikacheki kulia nikaziona funguo za ndinga lake, nikaona poa ngoja nichukue mkoko. Nikachukua nikasepa, sasa hawa polisi wanasema nimeiba gari how kam mzee wangu?

 HAKIMU: Kaaazi kwelikweli aka mbombo ngafu

You Might Also Like

0 comments: