Naombeni wa mawazo nimfanyeje akirudi??

17:14:00 Unknown 0 Comments

Ndugu zangu, Habari zenu?

Jamani mimi nafanya kazi ktk kampuni. Nilipata safari kikazi kwa muda wa wiki moja. Nilipoondoka niliacha kila kitu kwa familia yangu. Mke wangu naye ni mtumishi ktk kampuni nyingine.

Muda wa kurudi ulipofika niliamua kurudi kimyakimya bila kumtaarifu ili nimfanyie 'surprise'.

Leo wakati narudi ikabidi nimwambie driver tupitie Supermarkt ili nichukue mahitaji ya home pamoja na zawadi ya mke wangu.

Ajabu: nilipoingia humo Supermarkt nikamwona mke wangu. Nilijificha kwenye shelves ili asinione, kisha nikaenda upande ambao si rahisi kuniona.

Alipofika sehemu ya malipo nikamwona jamaa mmoja ambaye alikuwa nyuma yake wakikumbatiana na kubusiana kisha yule jamaa akalipa na wakaondoka na mizigo yao.

Ilikuwa saa 12 jioni: na sasa nipo nyumbani nje, bado wife hajarudi na funguo ya nyumba sina.

Naombeni wa mawazo nimfanyeje akirudi??

You Might Also Like

0 comments: