Simulizi ambayo wengi nimewashangaza
Nilihisi kuna mabinti wananitamani sana kuwa na uhusiano wa kimapenzi nami pale ofisini kwangu kwani mitego ilizidi sana jambo lililonipa hofu kubwa.Wakati huu nilishakuwa nimekaa kwenye ndoa kwa jumla ya miaka minne huku nikibahatika kupata mtoto mmoja tuliyebarikiwa na Mungu.
Tuliamua mimi na mke wangu kuwa niichukue nafasi hii ya kazi niliyoipata na kuhamishwa mkoa huu ili tuweze kukusanya fedha za kuweza kujiajiri.
Maisha na mitego ya mabinti wa mkoa huu yakanifanya nichukue hatua ya haraka kumwita mke wangu aje tuishi wote na kuendeleza miradi yake katika mkoa huu nikijua ndio kupona kwangu.
Nilifurahi sana alipowasili maisha yakasonga, mke wangu kwangu alikuwa ni zaidi ya rafiki na niliweza kuongea au hata kushirikiana nae katika kila jambo mpaka watu wakajua sio mke wangu.
Kuna siku tukiwa tunaongea na mke wangu akawa akinisimulia habari za mkoa huu mpaka nikashangaa amezipataje kwa haraka kiasi hiki ingawa akaniambia kama mwanamke lazima ajue mkoa una mambo gani ya kishetani ambayo yangeweza kumpokonya mmewe.
Moja alilonisisitiza ni kuwa uwapo mkoani hapa ogopa kama kifo kupokea zawadi zawadi kutoka kwa kinadada kwani wengi wao hutumia madawa kupata waume na mbaya zaidi waume za watu na mwisho kuzitelekeza familia zao.
Duuh!!!!! MAKUBWA, nilishangaa sana kwani mimi nilijua labda angesema suala la pombe au watoto wa vyuo ila hilo likanipa hofu na kumwahidi kamwe sitojisahau nitakuwa makini na nikaanza kuishi kwa hofu.
Siku moja nilichelewa ofisini na nilipokuwa naingia nilifurahi kuona kahawa yangu tayari imetengezwa na ipo mezani bado ya moto. Nilipouliza ni nani aliyenitengenezea nikaambiwa ni Salome nikamshukuru na kuendelea na kazi nikitoa baridi kwa kahawa maridhawa.
Jioni ile nilirudi nyumbani kwa kuchelewa baada ya kupitia bar na nakumbuka mke wangu aliponiuliza kwa nini nimechelewa sana tofauti na kawaida yangu na sitaki kula?
Nilimchapa kipigo cha mbwa mwizi mpaka majirani walikuja nyumbani kumsaidia na kwa kipigo kile na nilovyokuwa na jazba sikutaka alale pale hivyo akaenda kwa jirani.
Asubuhi nikaondoka zangu kwenda kazini na huku nyuma mke wangu akazidiwa kwani jana yake nikimpiga tumboni na kuangukia kwa tumbo na alikuwa na ujauzito wa miezi minne.
Jirani waliponipigia simu kuwa yupo hospitali nakumbuka hata sikuumiza kichwa changu kutafakari kama natakiwa kwenda huko na nikaachana nae.
Usiku nilirudi na kulala bila kujua mke wangu anaendeleaje huko siku ya pili yake rafiki yangu mmoja alinipigia simu na kunisema sana mpaka akaja kunichukua ndio nikaenda hospitali.
Ilimchukua siku nne mke akaruhusiwa na kurudi nyumbani ingawa sasa mimi nilizidisha vibweka kwake mpaka akafikia hatua ya kumpeleka mtoto wetu shule ya bweni ili apumzike kusikiliza na kuona ugomvi wangu na mama yake kila kukicha.
Hali ikazidi kuwa mbaya mpaka mke akaanza kutafuta watu wa kunishauri akianzia na wasimamizi wa harusi, wazazi na baadhi ya marafiki huku mimi jibu likiwa moja tu kuwa nataka tuachane sio chaguo langu tena.
Wakati huo mimi na salome yule binti wa pale ifisini mapenzi yetu yalichanua kutoka sirini mpaka kuwa ya halaiki huku sasa nikiwa nimemleta pale nyumbani na lala naye katika chumba changu na mke wangu na mke yeye akilala chumba cha wageni.
Vitimbi tulimzidishia kwa ushirikiano na salome lakini mke wangu alikuwa jasiri na hakutaka kuondoka.
Ikafikia kipindi kutokana na kila siku kulia huku akukosa matunzo akaanza kuupoteza ule mvuto wake na kuwa kama mtu mwenye ugonjwa wa ngozi asiye na matunzo mazuri huku kifo kikimnyemelea kwa msongo wa mawazo.
Ni kipindi hiki ambapo tulitembelewa na kaka yake mmoja ambaye hakutaka majadiliano akamchukua dada yake na kusafiri naye kwenda kukaa naye.
Tuliufurahia ule uamuzi na wakati huu sasa mimi na salome ikawa ni kama tumeachiwa huru vile hakuna kilichofanyika zaidi ya starehe na matanuzi mji mzima.
Miezi sita baadae usiku mmoja nikiwa natoka kazini kuelekea bar mmoja tukiwa na salome, tulipata ajali moja ya gari na mimi pekee ndio nilivunjika mguu na mkono na kupata mshtuko mgongoni.
Nikawa sasa ni mtu wa kubebwa, kuvalishwa, kulishwa na kila kitu nikimaliza hapo hapo nilipo.Salome aliniuguza kwa kipindi na kisha kunikimbia na baada ya mke wangu kupata taarifa akaja kuniuguza baada ya kutoroka kwa kaka yake.
Nilipona mwaka mmoja baadae na kurudishwa kazini lakini ile kumwona tu salome nikamsahau mke wangu tena na kuendelea na salome.
Hali hii ikamshangaza kila mtu wakati huo mke wangu nilishangaa kumwona wala haumii kama zamani.
Siku moja asubuhi nikiwa najiandaa kwenda kazini nikasikia kama mlango unagungwa vile na nilipotoka nikiwa tayari kuondoka nikagundua umefungwa na mbaya zaidi hata simu zangu zote hazipo na hakuna wa kumwita anifungilie.
Saa moja baadae walikuja watu watano wakaufungua mlango wakiwa na mke wangu na baada ya kujitambulisha wakaniambia ni wachungaji wamepata habari zangu na wangehitaji kunifanyia maombi.
Baada ya kurupushani walifanikiwa kunidhibiti na kuanza maombi.. niliishiwa nguvu na kama haitoshi nikajikuta naishiwa nguvu na kutaapika maji meusi mithili ya kahawa na kuona fahamu zanijia.
Nikakumbuka kahawa niliyopewa na salome siku ile ofisini huku machozi yakinitoka nikamwomba msamaha mke wangu na kuwashukuru wageni wale na sasa nikaondoka kwenda ofisini.
Nilipofika ofisini kila mtu akanisimulia juu ya mkasa uliotokea pale ofisini dakika chache zilizopita kuwa salome alianguka na kuanza kulitaja jina langu akiniomba nimsamehe kwa kuniwekea madawa na aliposhtuka kwa aibu kakimbia.
Nikatoka kwenda kwake nikiwa na jazba ili nimpe kipigo cha kumbukumbu kwa kunipa wakati mgumu katika maisha yake lakini hakuwepo wala simu zake hazikupatikana.
Kwa hasira nikakaa pale mlangoni kwake na kusema sitoki mpaka aje huku nikiwa nimefura kwa hasira.
Nusu saa baadae akaja akiwa anayemelea na bila kuchelewesha nikashika ipad yangu na kumrushia kabla ya kushtuka muda huu na kugundua ipad yangu imeanguka na kupasuka kioo baada ya kuisukuma kwa bahati mbaya na mkono nikiwa usingizinu.
"Duuh sijui nitaipata wapi ipad nyingine"
Fake story hii haina maana
Sababu 10 za kwa nini hutakuja kuwa tajiri maishani mwako
1. Matumizi yaliyopitiliza - Matumizi yasiyo na mipaka katika mapato yako ya mwezi sio njia sahihi ya kukupa utajiri.
2. Kutokuweka akiba ya kutosha - Kujiwekea akiba ni jambo la m... See More
1. Matumizi yaliyopitiliza - Matumizi yasiyo na mipaka katika mapato yako ya mwezi sio njia sahihi ya kukupa utajiri.
2. Kutokuweka akiba ya kutosha - Kujiwekea akiba ni jambo la m... See More
144 people reached
0 comments: