Showing posts with label Mapenzi. Show all posts

Hatimaye akaolewa na yule mwanaume aliyempenda kwa mika 10...........SOMA NI NZURI



Hatimaye akaolewa na yule mwanaume aliyempenda kwa mika 10..

Mwishoni kabisa mwa tafrija fupi waliyoandaliwa na familia, mama yake alimwita pembeni na alimpa zawadi ya kitabu cha benki kilichokuwa na milioni mbili za kitanzania alizokuwa ameziweka. 

Mama akamwambia mtoto wake pekee wa kike, "Mwanangu, tafadhali chukua hiki kitabu cha benki.Kitunze kama kumbukumbu yako ya maisha ya ndoa. 

Kikitokea kitu kizuri katika maisha yenu na ambacho ukaona ni kumbukumbu basi wewe weka kiasi chochote cha fedha kwenye akaunti hii. Andika chini kitu hicho ni  nini na kiwango cha fedha ulichokiweka.

Jinsi utakavyokuwa na matukio mengi ya furaha basi kumbuka ndio hivyo hivyo na fedha zitaongezeka katika akaunti hii kwa jinsi utakavyoweka. Mimi nimekuanzia kwa kuweka fedha katika akaunti hii kutokana na tukio hili kubwa la wewe kuolewa. Matukio mengine naomba ushirikiane na mmeo kuhakikisha mnayaweka katika kumbukumbu kwa jinsi mlivyoyafurahia pamoja” 

Alipofika nyumbani akamshirikisha mmewe usiku ule alimshirikisha mmewe na wote walilifurahia jambo lile na kuona ni wazo jema sana. Kitabu chao cha benki kilionekana hivi baada ya miezi michache…

- February 7 – 200,000: Kumbukumbu yake ya kwanza ya siku ya kuzaliwa baada ya ndoa
- March 1 – 600,000: Aliongezewa msharaha kazini
- March 20 – 400,000: Shukrani ya kurudi salama kutoka mapumzikoni Kilolo
- April 15 – 4,000,000: Ana ujauzito!
- June 1 – 2,000,000: Alipandisha cheo na kuwa meneja kazini kwake

Mambo yaliendelea kuwa hivi kila tukio lilipojitokeza lenye furaha...

Ingawaje, miaka ilivyozidi kuyoyoma wakajikuta wakianza kupigana na kupigizana kelele kila kukicha.Hawakuongea tena sana kama hapo awali, kila muda walijilaumu kuoana na ule upendo wa awali ukatoweka kabisa.

Siku moja mke akampigia simu mama yake na kumwambia, "Mama, hatuwezi kuendelea na ndoa hii. Tumeamua kupeana talaka. Nashindwa kuamini nini kilinikuta nikaona na huyu mwanaume!”

Mama akamjibu, "Fanya lolote utakalo mwanangu,kama ni kweli umeshindwa kuvumilia. Ila kabla ya kufikia uamuzi huo kuna kitu naomba ukifanye kwanza.Unakumbuka kile kitabu cha benki nilichokupa wakati wa harusi yako? Tafadhali naomba ukachukue fedha zote na uzitumie kwani hutakiwi tena kuwa na kumbukumbu za maisha ya ndoa ambayo yana mwisho mbaya kama huo wako."

MKe alikubaliana na mama yake na akaenda siku ya pili yake benki wakati huu alikuwa kwenye mstari akisubiri nafasi yake ili akatoe fedha zote na kuifunga akaunti ile. Akiwa pale kwemye mstari anaisubiri zamu yake akaona achukue kile kitabu na kuangalia kumbukumbu za matukio yao ya furaha na kiasi cha pesa kilichowekwa. 

Aliangalia tena na tena kwa muda kisha zile kumbukumbu za yale matukio yote yenye furaha zikamrudia. Wakati huo macho yake yakawa yamejawa na machozi hivyo akaamua kurudi nyumbani. 

Aliporudi nyumbani akampa mmewe kile kitabu na kumwambia mmewe akazitumie zile fedha zote kabla ya wao kupeana talaka.

Siku ya pili mme akawasili benki, na tukio lililomtokea mkewe jana yake likamtokea pia mmewe. Alizidiwa pia na furaha ya matukio mazuri nay a kumbukumbu aliyoyafanya na mkewe katika kipindi cha ndoa yao na kumfanya arudi nyumbani machozi yakiwa yanamlengalenga.

Alipofika nyumbani akampa kitabu mkewe na kulikuwa kuwa fedha mpya imeingizwa katika akaunti hiyo (5,000,000) ikiwa na maneno, “Leo ndio siku ambayo nimegundua kuwa nakupenda sana mke wangu katika miaka yote tuliyokaa pamoja na jinsi ulivyonipa furaha katika maisha haya”

Wakakumbatiana na kulia kwa pamoja.KItabu chao kikarudisha katika sanduku lao maalumu na kuendelea kutunzwa huko

AMKA TOKA NDOTONI MAPENZI KAMA HAYA HAKUNA WEWE ENDELEA KUOTA TUU

Ila share

Amri kumi za kukumbukwa kwa mabinti wote single duniani



1. Usiharakishe kutoka nyumbani kwa wazazi wako kwa gia ya kwenda kuolewa.
2. Usimsubiri mwanaume mpaka aje  ndio uanze kuishi. Unaweza kuishi maisha timilifu hata ukiwa huna mwanaume.
3.Achana na pombe zimewauwa wenzako wengi kwa kisingizio cha kuondoa stress na wewe unaweza kufa pia.
4. Usiwe mtu wa kuendekeza kuzipokea na kuzijibu namba ngeni za simu hasa nyakati za usiku.. sio njia sahihi ya kupatia mpenzi.
5. Tengeneza mazingira ya kuilinda afya. Jitahidi kunywa chai asubuhi maji mengi  na acha kula vitu vitamu
6. Vaa vizuri na kiheshima. Watu watavutiwa na wewe ulivyo kabla ya kuongea nawe
7.Usitumie sex kama ndio mzani wa mapenzi.Unaweza ukaachika tuu pamoja na penzi lako taamu.
8. Usiolewe na mtu kwa sababu ya fedha; Utabakia kuwa mtumwa wake
9. Jiongezee ubora wako, Tafuta kazi.Usiwe mpuuzi ukaamini mwanaume atatatua matatizo yako yote.
10. Jiheshimu sana kwa kuangalia namna ya uvaaji wa mavazi yako na mwonekano wako mbele ya jamii…. Usitegemee kuvaa kimini ukutane na mwanaume wa suti… wewe utampata wa milegezo na kubana pua tu.

MAMBO YANAYOWAKERA WAKE



1. Wababa wenye madaraka kuyapeleka madaraka nyumbani
2. Wake kuwajibika na mambo ya nyumbani kwa vile wana mishahara minono
3. Wababa kutotenga muda wa kutosha kukaa na wake zao ili kuongea yanayowahusu
4. Mume kumwachia mke kulea watoto hasa wakati wa usiku
5. Mume kutomtia moyo mke wakati wa ujauzito
6. Mume kumchanganya mama na watoto wa kike wanapokosa
7. Mume kutokuwa na maandalizi mazuri wakati wa kukutana kimwili na mkeo
8. Mume kujijari mwenyeweMume kusaidia ndugu zake bila mke wake kujua
9. Mume kubagua watoto
10. Mume kuwa na upendo na ukaribu au kucheka na binti waishio nao huku yupo mke wake
11. Mume kutomshirikisha mkewe katika huduma yake ya ili aweze kumwombeaKutoonesha shukrani wala kutokuwa na msamaha
12. Mume kutomtazama mkeo usoni mkiwa chumbani.

TABIA 27 ZA WANAUME/­ WAVULANA WANAOJUA KUPENDA



1. Hupiga simu mara kwa mara

kumuulizia mpenzi wake
anaendeleaje 

2. Hujihisi vibaya pale
anaposahau siku ya kuzaliwa
(birthday) au siku mliyoanza
mahusiano (anniversary) na
huomba msamaha

3. Hushukiza na zawadi
mbalimbali hata kama sio
muda maalumu

4. Mara kwa mara hukuambia
"NAKUPENDA">>>"I Love You"

5. Anajua kufanya mapenzi na
wewe

6. Anajua jijnsi ya kujali,
kukumbatia, kuchumu na
kutimiza mahitaji ya
kimahaba kwa mpenzi wake

7. Huhisi kuumia pale mpenzi
wake anapopitia hali ngumu

8. Hupenda kuona mpenzi
wake ana furaha na hutamani
kufurahi pamoja

9. Siku zote hutafuta muda
mzuri kutumia pamoja na
mpenzi wake

10. Kamwe hawezi kumpiga
au kumuumiza kisaikolojia
mpenzi wake

11. Huoa bila kusubiria
sanaaaa...

12. Husamehe na kusahai pale
anapoumizwa hisia zake

13. Hatotumia siri au udhaifu
wako kukufanyia mabaya

14. Hatotangaza kama mpenzi
wake ana madhaifu fulani

15. Ni mvumilivu na tayari
kufanyia usulihisho kwenye
matatizo ya uhusiano wake

16. Anajua kwamba ni
muhimu kwa mpenzi wake
kutumia muda wake akiwa na
marafiki zake, ndugu na
familia yake

17. Kamwe hawezi kutoka nje
ya uhusiano wenu ( will not
cheat on you)

18. Hawezi kuwachokoza
marafiki zako wakike mpaka
point ambayo itakuwa
inakuboa au kukupa mashaka

19. Hawezi kwenda nje ili
mfanye mpenzi wake apate
wivu

20. Humheshimu mpenzi wake
pale awapo na marafiki na
familia yake

21. Humsaidia mpenzi wake na
kazi mbali mbali( mf. za
nyubani au masomo)

22. Hufurahia kampani ya
marafiki na ndugu wa mpenzi
wake

23. Husaidia kufikia malengo
na kutimiza ndoto za mpenzi
wake

24. Kamwe hakatishi tamaa
mpenz wake pale
wanapokuwa wanaongea

25. Hujali sana kuhusu
mawazo, hisia na ushauri wa
mpenzi wake

26. Mara nyingi huwepo pale
mpenzi wake anapohitaji
msaada

27. HUJUA KWAMBA NJIA
YAKE SIO NNJIA PEKEE.....

Kamwe sitosahau jinsi mme wangu alivyonifunga kizazi kishirikina kwa miaka mingi



Miaka kumi na mbili iliyopita binti huyu pichani aitwaye Dear alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na kijana mmoja wakiwa na umri wa miaka 18.
Walipendana sana na kuapiana kuwa wasingesalitiana na kuja kuishi kwa pamoja kama mme na mke baada ya kuhitimu masomo yao.

Binti akatoa wazo kwa kuwa yeye hana imani na wanaume, kwani wengi huwa na tabia za kusaliti mahusiano basi waape kwa kitumia Biblia na kofuli.

Wazo hili kijana alilipokea kwa furaha na binti akafurahi sana kuona yule kijana amekubaliana nae kuwa ataapa kwa njia hiyo kama ishara ya kuwa hawatasalitiana na kupendana kwa dhati.

Wakaondoka wakiwa na biblia na kofuli yao mpaka kwa mzee mmoja aliyeaminika kwa busara na kumweleza adhma yao naye kabla ya kuwakubalia ombi la kuwa shahidi wao akawauliza,

" Je ni kweli mmeamua kuapa kwa kutumia Biblia na kofuli hii kuwa mnaufunga uhusiano wenu kuwa wenu tuu na mnakubali kuwa hamtasalitiana milele?"

Wote wakajibu ndio.

"Je mnatambua kuifunga kofuli hii na ufunguo kuniachia mimi na kofuli kwenda kuitupa mbali mjue kamwe hamtaifungua tena na matatakiwa kuwa pamoja kwa namna yoyote ile?"

Wakasema tumeafikiana.

Mzee akawaongoza kwa sala na kuwaomba waishi kama walivyokubaliana na kisha kuifunga ile kofuli.

Wale vijana wakarudi majumbani kwao na kuendelea kuishi kwa furaha na amani huku kila mtu akiwa na kiu ya kuonyesha zaidi upendo kwa mwenzake.

Miaka ikaenda wakahitimu chuo na kijana akapangiwa kazi kijijini sana na kukawa na matatizo ya usafiri na binti kwa kuwa alipangiwa mjini akawa kila mara akimtembelea kijana na kijana akienda mjini pia.

Miaka ikaenda hatimaye taratibu wakaanza kupunguza mawasiliano baada ya kijana kuhamishiwa mbali zaidi na binti akabadili namba na kuanza mahusiano na boss wa kampuni yake na kisha wakaoana.

Kijana akafanya kazi kule kijijini kwa kujituma na kuweka fedha ili aweze kuja mnunulia pete nzuri ya uchumba na harusi yao ije kufana na waishi vizuri bila kujua kuwa keshaolewa.

Baada ya kujiandaa vya kutosha akaanza kuomba uhamisho ahamie mjini na alipofika mjini akapata habari za mkewe kuolewa na wamehama mji ule.
Kijana aliumia sana na kisha akaamua kuondoka kwenda mbali kuanza maisha mapya akiwa na huzuni sana.

Maisha ya furaha yakamwishia yule binti kwani hakupata mimba wala dalili na kila alipofanyiwa uchunguzi akaonekana yupo safi.

Furaha na amani ikaanza kumpotea katika familia yake na baadae mambo kuwa mabaya zaidi kabla ya kuanza kutembelea kila kibanda kilichoandikwa mganga wa jadi akihisi kafanyiwa mchezo.

Baada ya kwenda kwa njia hizo zote bila mafanikio akawa hana jinsi zaidi ya kuwa mtu wa kulia na kuhuzukika kila mara.

Siku moja akiwa ndotoni akaonyeshwa Biblia na ile kofuli akakumbuka kuhusu nadhiri yake na yule kijana. Akaanza kumtafuta yule kijana amwombe msamaha na baadae akampata.

Baada ya kumwambia kijana huku akimwomba msamaaa kijana akasema mimi sina tatizo ndio maana sikuoa ili nikuone na uje uniruhusu kwa kulingana na agano letu.

Na kilichobaki hapa ni kumtafuta mzee kwani kofuli mimi nilimkabidhi mama yangu na analo kwani niliamini mama ambaye ni mwanamke kama wewe angenirekebisha kama nikikosea na ajue siri yangu na wewe ili azidi kunipa hekima na busara ya kuwa na wewe, je na wewe funguo ya akiba uliweka wapi?

Binti akasema niliipoteza nilipoanza mahusiano na mme wangu.
Wakaenda kwa mzee na kusikia kuwa alishafariki, kijana akampa kofuli bila ufunguo na kumwomba binti ampe ruhusa akaoe.

Binti akakubali na kijana akaoa na sasa ana mke na watoto wawili lakini yule binti mpaka sasa kashaachika zaidi ya ndoa nne akikosa amani kwa kuvunja agano lake na kijana yule.

Dada na kaka zangu kumbukeni

1. Kamwe usimwahidi mtu kumpa mambo makubwa maishani na hali wewe huna uwezo

2. Kamwe usimwambie mwanamke unampenda wakati humaanishi

3. Usitumie vitabu vya dini kufanikisha mipango yako ya ulaghai wa mapenzi

4. Kamwe usiwahusishe watu kukusaidia kushuhudia uongo ili kumpata mwanamke...Hawa ni viumbe ambao kwa asilimia kubwa sisi wanaume ndio huwafanya waumie na kila mwanamke katili,jambazi, kahaba na wengine lazima wana hadithi iliyowafanya kuwa hivyo na ilisababishwa na mwanaume

5. Usijaribu kufanya ahadi yoyote ili kumpata mwanamke ukiapa kwa jina la Mungu kama huamini

Ukishindwa kutekeleza huishia kukosa furaha maishani mwako na kuwa kama dada yetu.

Comment "Nawachukia wasaliti' kisha share na like page hii ya  Fuledi

SABABU ZINAZOMFANYA MWANAMKE KUCHEPUKA

SABABU ZINAZOMFANYA MWANAMKE KUCHEPUKA 
Kuna sababu zinazomfanya mwanamke amsaliti mwenza wake,

Ni muhimu kutambua kuwa mwanamke ni kiumbe mwenye hisia kali na daima huhisi raha na amani pale anapooneshwa upendo, anapoona hapati upendo hufanya usaliti ili kuziba pengo la upungufu unaotokea katika maisha yake. Zifuatazo ni sababu kubwa ambazo zinamfanya amsaliti mumewe.

1. KUTOMPA KIPAUMBELE NA KUTOMTHAMINI
Tunatambua kuwa mke anafanya kazi kubwa sana ambayo lau kama ingekuwa ni kampuni basi pange hitajika watu zaidi ya 10 kuzifanya, mke humtunza
mume, watoto, nyumba na familia kwa ujumla.

Wakati fulani mume anaweza akampuuza na asimthamini, licha ya kujitoa kwa moyo wote kumtunza na kuihudumia familia,Hivyo, kutotoa kipaumble kwa mke ni kosa kubwa ambalo linaweza likamgharimu mume, mke akipata mtu anayempa kipaumbele na kumuonesha thamani hakika hatoacha kuitumia
hiyo fursa.

2. UKOSEFU WA MAHABA
Kwa asili mwanamke ana silika ya hitajio la kupendwa, mwanamke anahitaji kupendwa,Mwanamke anahitaji kupetiwa, anahitaji kudekezwa, anahitaji aambiwe maneno yenye ladha adimu mwanamke anataka hivyo, anataka aone kama anapendwa, anataka aone mtu anamwambia vile alivyo maridhawa amueleze hisia zake.

3. USALITI WA MUME
Miongoni mwa mambo ambayo huibadilisha roho ya mwanamke ni pale anapogundua kuwa mumewe kipenzi anamsaliti, hapo mwanamke anaweza akabadilika kabisa wapo wanao samehe, lakini wapo wanaolipiza kisasi.

4. KUTOJIAMINI
Mwanamke anahitaji mwanaume anayemfanya ajiamini iwapo mumewe hatekelezi jukumu hilo, akimpata mtu anayemfanya ajiamini, yanaweza kutokea mengine kabisa,hivyo, nasaha zangu kwa kaka zangu kuyaangalia kwa makini mambo haya

ZIJUE TABIA ZA WANAUME WANAOTAKA KUOA MWANAMKE, HIZI NDIZO SIFA SIFA 5 KUU ZA WANAWAKE HAO !!. JE WEWE MWANAMKE UNAYETAKA KUOLEWA UPO KATIKA SIFA HIZO !!!

KUTOKANA na hali halisi ya maisha kuwa magumu kutokana na tatizo la ukosefu wa ajira ndani na nje ya nchi, hii imepelekea Wanaume wengi wanapofikia hatua ya kuoa si kwamba wanakurupuka tu na kuoa mwanamke yeyote mwenye sura nzuri, bali huchukua muda wao mwingi kuchunguza mambo mengi juu ya wanawake ambao wanadhani kwamba wanaweza kuwa pamoja kwa kipindi chote cha maisha.


Wanawake wengi wamekua wakipoteza muda wao mwingi katika suala zima la kujiremba na kujichubua ili wawavutie wanaume bila ya kujua kwamba kuolewa ni zaidi ya uzuri


Hali sasa hivi imebadilika ni tofauti na kipindi cha nyuma ambapo ukiwa na sura nzuri na umbo la kuvutia basi una asilimia 100 za kuolewa. 

Kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanywa zinaonesha kwamba zaidi ya uzuri wa tabia na umbo, kuna sifa nyingine za msingi ambazo mwanamke anatakiwa kuwa nazo ili aweze kuwa katika mazingira mazuri ya kupata mchumba wa kumuoa kiasi kwamba asipokuwa nazo ataishia kuchezewa tu lakini haitatokea mtu kwamba anataka kumuoa.Twende pamoja tuzijue sifa muhimu kabisa za kuwa nazo mwanamke fofauti na urembo:


1. MWEYE MAPENZI YA KWELI
Lengo kubwa la mwanaume kuoa ni kutaka kupata mapenzi ya kweli kutoka kwa mwanamke na ikiwezekana waweze kupata watotoa ambapo watoto mara ndio wamekuwa furaha ya ndoa. Wapo wanawake wengine ambao wanonesha wazi kutokuwa na mapenzi ya kweli bali wanakuwa na mapenzi ya kuzuga. Wanachotaka wao aidha kupata umaarufu tu kwamba yuko na mtu fulani ama kuweza kupata pesa alizonazo mwanaume lakini sio kwamba ana mapenzi ya dhati kutoka moyoni mwake. 

Mwanamke asiye na mapenzi ya dhati utamgundua tu, muda mwingi utamuona macho yake yako kwenye mfuko wa mwanaume. Akiona kwamba mfuko umetuna utaona anaonesha mapenzi ya hali ya juu lakini pindi hali inapokuwa kubwa mbaya kifedha mapenzi yanaanza kufifia.

Kwanini wanaume wanapenda wana wake wenye mapenzi ya dhati kutoka mioyoni mwao na si kutokana na fedha walizonazo? Hii inatokana na ukweli kwamba maisha siku zote yanabadilika, kama waswahili wanavyosema, kuna kupanda na kushuka.

Sio kwamba kila siku utakuwa na maisha mazuri na kama itatokea hivyo basi ushukuru mungu.Hivyo basi mwanamke wa kuoa lazima afahamu hivyo na awe tayari kuonesha mapenzi yake ya dhati wakati wote wa maisha yao na si kwa kipindi fulani tu cha neema.

Si hivyo tu pia asilimia kubwa ya maisha ya ndoa yanatawaliwa na mapenzi, kwa hiyo nyanja hiyo inakuwa ya msingi sana kwa wanaume wengi kuiangalia ili wasije wakajikuta wanaoa mwanamke ambaye baada ya muda mapenzi yanakwenda likizo hali ambayo inaweza kuwafanya wasiishi maisha ya raha mustarehe.



2. WENYE TABIA NZURI
Tabia njema ndio silaha ya maisha, ukiwa na tabia nzuri kila mtu atakupenda, hiyo ni katika maisha ya kawaida. Lakini linapokuja suala na kuoa tabia inakuwa kitu cha awali sana kungaliwa na hiyo inaweza kuwa na ukweli kwa sababu wapo wasichana wazuri wenye mvuto wa aina yake na maumbile mazuri, lakini wanakosa wanaume wa kuwaoa, ukiuliza kwani utaambiwa anatabia mbaya.

Naweza kusema hilo ndilo limekuwa tatizo kubwa kwa baadhi ya wanawake kukosa wanaume wa kuwaona. Hakuna mwanaume hata mmoja kati ya wale ambao nimejaribu kuongea naye ambaye ameonesha kulidharau suala hilo la tabia.

Si hivyo tu wapo wanaume ambao wameingia kichwa kichwa na kuoa kwa kuangalia sura tu bila kujali tabia, matokeo yake baada ya siku chache yanatokea machafuko ya aina yake hali ambayo imepelekea kuvunjika kwa ndoa kutokana na tabia mbaya alizonazo mwanamke.


3. WENYE UCHU NA MAENDELEO
Hivi karibuni kumekuwepo na mabadiliko ya aina yake kwa wanaume, wengi sasa hivi hawapendi kabisa kuoa mwanamke ambaye hana kazi yaani 'golikipa'. Kama atakuwa hana kazi basi awe na uchu wa maendeleo kwa kujituma kufanya kazi mbalimbali za kimaendeleo kama vile kilimo kwa wale walio vijijini na biashara ndogondogo kwa wale ambao wako mijijini na hata vijijini. 

Ile dhana ya kusema mwanamke ni mama wa nyumbani wa kukaa na kujipodoa akimsubiria mwnaume arudi amstarehesha, sasa hivi imepitwa na wakati. Wanaume wengi wanapenda wanawake ambao ni wahangaikaji, wenye ndoto za maendeleo katika maisha yao. Hata kama watakuwa si wafanyakazi lakini wawe wenye kutoa ushauri kwa waume zao juu ya jinsi gani wafanye ili wafanikiwe.



4. WASIOPENDA MAKUU
Kuna wanawake wengine wanakuwa na tabia za ajabu sana kiasi kwamba yaweza kuwa kero kwa wanaume. Wapo wanawake ambao wanapenda makuu bila kujali hali halisi ilivyo. Kuna wanawake naweza kusema wana tamaa, kila wikiendi utamsikia "leo tunakwenda wapi dear?"


Akimuona rafiki yake kanunua simu ya laki tatu na yeye utamsikia akisema, ‘na mimi naomba uninunulie simu kama ya Grace’. Ukienda naye Pub anakuambia, "mimi sinywi pombe za chupa natumia za kopo tena Heineken’. Yeye hajali kiasi cha pesa mwanaume alicho nacho na usipotekelezea anachukia na anaweza hata kupunguza mapenzi.

Wanawake kama hawa wako katika mazingira magumu sana ya kuweza kupata wanaume wa kuwaoa. Mara nyingi katika maisha fedha huzungumza, kama mwanaume atakuwa na pesa ya kutosha itakuwa rahisi sana kwa mwanamke kupata kila atakachopenda lakini si kwa kumwambia mimi nataka kitu fulani.Mwanaune mwenyewe utamsikia akisema, ‘unataka nikununulie simu ya aina gani, au leo unataka twende wapi?’ hapo ndipo utakuwa na nafasi ya kusema, ‘mimi nataka uninunulie simu kama ya fulani ama leo nataka twende sehemu fulani.’

Wanaume ni warahisi sana wa kuwapatia wale ambao wanatarajia kuwaoa chochote ambacho watahitaji kama tu pesa haitakuwa tatizo. Kitu ambacho kinawaudhi wanaume wengi ni ile tabia ya mwanamke kupenda mambo makubwa bila kuangalia uwezo uliopo kwa mwanume.

Kuna wanawake wengine wao si wasemaji kabisa, yeye anasubiri leo amemletea hiki, anapokea na kushukuru, kesho akiambiwa twende beach anakubali. Au wengine wanasubiri mpaka waulizwe wanataka nini, ndio wanasema. 



Sisemi kwamba uwe mkimya tu hata kama una shida ya kitu fulani na unafahamu kwamba ukimweleza mwenza wako anaweza kukusaidia, hapana! kama unaona kwamba uwezekano wa kupata kile ambacho unakihitaji upo mweleze kwa utaratibu naamini atakuelewa na kukutimizia.Tabia ambayo hawaipendi wanaume wengi ni ile ya kulazimisha ufanyiwe kitu fulani wakati inawezekana uwezekano haupo.
 
5. WAVUMILIVU
Wapo wanawake ambao sio wavumilivu kabisa katika maisha.Tunajua kwamba maisha siku zote hayatabiriki, yanaweza kutokea matatizo ya kiafya ama kifedha.Huu ndio wakati wa kuona uvumilivu wa mtu.Kama mwanamke anatarajia kwamba siku zote ni za raha tu na pindi matatizo yanapotokea anachukua uamuzi wa kumtoroka mwanume, huyo siyo mwanamke wa kuoa.

Wangapi leo hii huwatoroka waume zao pindi inapotokea kuumwa, kufilisika ama kupatwa na tatizo lolote ambalo kwa namna moja ama nyingine yanaweza kuwafanya maisha yao kutingishika?

Uvumilivu kwa mwanamke utakuwepo kama tu atakuwa na mapenzi ya dhati kama nilivyozungumza hapo awali. Mwanamke mweye mapenzi ya dhati ni lazima atakuwa mvumilivu na atakuwa tayari kuishi katika maisha ya aina yoyote, yawe ya raha ama ya starehe.Hawa ndio wale ambao wanaume wengi wengependa kuwa nao maishani mwao.

Licha ya kupenda kuoa wanawake amabo wana tabia hizo nilizozitaja hapo juu, wanachukizwa sana na wanawake ambao wanavijitabia vidogo vidogo ambavyo kimsingi havikubaliki katka jamii.

Tabia hizo ni kama wambea, wasio wakweli na wawazi, wasioridhika, wagumu kusamehe na wapesi wa kuchukia, wagomvi na wenye roho ya kwanini.
Utafiti huu umefanyikwa kwa baadhi ya wanaume ambao wanatarajia kuoa wanawake ambao wanaoishi katika maeneo mbalimbali 

 
Kwa maana hiyo basi hiyo iwe changamoto kwa wanawake. Wajue kwamba wanaume wanafurahi kuwa na wanawake wa aina gani.



Hata kama utakuwa umeshaolewa, kama kuna wakati kunakuwa na kutokuelewana baina yenu, chunguza yawezekana kwamba unakosa mojawapo ya tabia ambazo nimezitaja hapo juu. Waweza kubadilika kwani inawezekana.