Huyu ndiye jogoo mwenye tabia za kibinadamu

13:11:00 Unknown 0 Comments

MKULIMA mmoja alikuwa anafuga kuku wa kienyeji. Alikuwa na majike 25 jogoo mmoja.

Baada ya kuona jogoo amekuwa mzee akaamua kununua jogoo jipya. Ile jogoo mpya kufika tu kukawa na mazungumzo kati ya majogoo;
JOGOO MZEE: Karibu dogo, karibu sana nadhani tutashirikiana vizuri ili kuhakikisha hawa kuku wanataga mayai
JOGOO DOGO: Wewe umeshazeeka ndio maana
nimeletwa mimi damu mpya. Hakuna kushirikiana wala nini umekwisha wewe
JOGOO MZEE: Kama unaona nimekwisha basi tufanye mashindano unipime
JOGOO DOGO: Mashindano gani?
JOGOO MZEE: Tushindane mbio tuzunguke nyumba mara mbili, ukishinda mi najitoa. Ila kwa kuwa mi mzee naomba uniache nianze
kama hatua kumi mbele
JOGOO DOGO: Poa sana hiyo haya anza kukimbia... mbio zikaanza, walizunguka nyumba mara moja tu, mkulima akamfwata JOGOO
DOGO akamkamata na kumchinja huku akilalamika
MKULIMA: Yaani dunia imeharibika, huyu Jogoo wa sita sasa namnunua badala ya kufukuza
majike analeta ukameruni hapa! Anataka kupanda jogoo mwenzake badala ya mitetea! Labda ahamie huko kwa kameruni

You Might Also Like

0 comments: