Showing posts with label Maisha. Show all posts

Baada ya kila dhoruba kali nuru huonekana

Nilikulia katika kijiji kimoja kusini mwa Tanzania na mama yangu yeye alikuwa mwalimu wa chekechea wa kujitolea katika shule hiyo ya watoto wadogo pale kijijini.
Mtu niliyeambiwa kuwa ni baba yangu alikuwa ni mlevi wa kupindukia pale kijijini na fundi selemara aliyemiliki sehemu ndogo ya kufanyia kazi kama ofisi yake ya kujipatia kipato ambacho alikitumia kwa kununulia pombe na kubaki katika maisha duni sana.
Baba huyu alikuwa mkali akimpiga mama na mimi kila siku na sitaki kukumbuka jinsi kila siku mama alivyonikumbatia na tukasaidiana kulia tukimwomba Mungu ambadilishe baba huyu ambaye pia alikuwa na wake wengine wawili na kunifanya kutambua kuwa mama yangu alikuwa ni mke wa nje wa baba.
Nililia na kumwomba Mungu ayabadilishe maisha yetu kila siku na nilifurahi sana kila siku jumapili nilipomwona mama akiimba kwa furaha katika kwanya pale kanisani na kunifanya kufurahi kila ifikapo jumapili ambapo ndio nilimshuhudia mama yangu akiwa na furaha ya ajabu na kuyasahau magumu ya nyumbani na kumshukuru Mungu.
Mama alinifanya kuona kuwa kanisani na kumwomba Mungu kipindi hicho ndio ilikuwa faraja yetu kubwa na alinisisitiza kuwa nitafanikiwa na kuwa mtu mkubwa katika maisha haya na kunifundisha kusamehe.
Somo la kusamehe lilinikaa sawa sawa na kumsamehe baba yangu kwa kila alichomfanyia mama na kusababisha maisha yetu kuwa magumu hasa baada ya kumpa mama ujauzito uliomfanya aishie kidato cha tatu na kusitisha masomo ili anikuze mimi huku familia yake ikimtenga na kuanza maisha yake.
Nilimsamehe na miezi michache baadae alifariki baada ya kupata tatizo la mapafu yaliyoharibiwa na uvutaji wa sigara na kufa kwa kukosa fedha za kumfanya atibiwe katika hospitali kubwa pamoja na jitihada za kuuza ardhi yetu na baadae maisha yetu yakazidi kuwa magumu.
Nakumbuka kila siku asubuhi nikiwa naenda shuleni jinsi mama alivyonipa nguvu na maneno ya ujasiri yenye uthubutu kuwa nitakuja kufanikiwa na kuitunza familia yetu na pia nakumbuka jirani yetu mama fred ambavyo yeye naye aliwahi kunipa zawadi ya viatu pamoja na ufukara wake ambao ulilingana na ule wetu na kuniambia kila nivaapo vinifanye niamini nitafanikiwa kuyakanyaga maumivu yote na kusonga mbele kufuata sauti ya ushindi na kuja kuwa mtu mwenye mafanikio.
Kila nilipovivaa viatu vile nilihisi kuwa yale maumivu ya mama na maumivu ya ufukara wetu wa kutisha pale kijijini kuna siku ningekuja kuyakanyanga na kumvalisha mama viatu vya furaha na kuja kumfanya maisha yake yote yawe ya furaha na tabasamu kama awapo kwenye kwaya yake siku za jumapili, kwa kweli nilikuwa nikisikia sauti za mafanikio zikiniambia nijitume..
Siku moja tukiwa shule ya sekondari tumekaa kando ya barabara tunacheza na kufurahi mbele yetu alikuja baba mmoja akiwa kashika begi mkononi na mkono mwingine kashika fimbo na miwani jambo lilinifanya nihisi kuwa mzee yule alikuwa ni kipofu.
Akaomba kwa sauti "wanangu naomba mnisaidie kuvuka barabara!"
Hakuna aliyemsikiliza zaidi ya watu kumcheka pale na kuendelea kucheza, mimi nikaamua kusimama na kwenda kumsaidia na nilipofika pale nikamwambia
"naweza kukusaidia?"
Akajibu "ndio"
Nikamwambia naomba nishike bega langu la kulia na nikamvusha na kumbe alikuwa anakuja pale shuleni kwetu na baada ya kuniuliza ni sehemu ipi anaweza kukaa na kumwonesha basi akalifungua lile begi lake na kutoa pipi na biskuti na kuzitandaza juu ya kitambaa chake na kuanza kuziuza na mimi akiniambia,
"mwanangu Mungu atakubariki sana na nitatamani siku nifungue macho yangu kuona mafanikio yako kwani sauti yako tu inanionyesha una hekima na huruma"
Nilimwangalia kwa dakika kadhaa nikiwa pembeni huku akiuza pipi, chocolate na biskuti zake kisha machozi yakanitoka na kushindwa kuyahimili na kuondoka zangu kurejea kwa wenzangu.
Tuliendelea kuwa marafiki na kila siku muda kama ule nilimsaidia kumvusha pale baada ya kuniulizia dan niko wapi, kusikia sauti yangu na mara nyingine alinikuta namsubiri nimvushe pale.
Kuna siku nilifika pale kituoni na kugundua hajafika nikakaa pale kwa dakika kadhaa nikiwa nimejificha sehemu na alipofika nikaaendelea kukaa pale na hakumwita mtu mpaka watu wakaondoka nami nikamsogelea na kukaaa kimya kwa dakika bila kuongea kitu na baada ya watu wachache kupita akaniita "DAN"
Nikaitika nakusema "NAAM", umejuaje kuwa nitakuja na kwanini hujamwomba mtu yoyote akusaidie kuvuka?
Akaniambia " Niliamini kuwa utakuja kwa kuwa wewe ni rafiki na kuna sauti iliniambia lazima utakuja nami nikakusubiri"
Nilishangaa wala sikuongea kitu chochote na kumsaidia kuvuka kisha tukaenda na nikamwacha akiuza nami nikaingia darasani.
Alikuwa rafiki kwani kuna nyakati nilimsaidia hasa pale wanafunzi walipokuwa wakimlipa shilingi mia tano badala ya alfu moja wanunuapo vitu na kunifanya mimi kuwa na maadui wengi pale shuleni zaidi ya marafiki na ikafika kipindi nahitimu pale aliniita na kunipa yeye aliyoiita zawadi ya kuwa
"mwanangu utafanikiwa kama nawe utaisikia sauti ya mafanikio kama mimi nilivyokuwa na imani kuwa kila mara ungenisaidia na ukawa hivyo"
Nilimjibu amen na kuondoka ingawa nilihisi nampoteza rafiki ambaye alinijenga sana.
Miaka miachache baadae kwa jitihada za mama yangu nilifanikiwa kuhitimu chuo kikuu na kupata kazi katika kampuni moja ya kutengeneza vitabu na kipata mwanya wa ufadhili na nikaandika historia ya maisha yangu niliyoiita "Maisha ya Salome na Mwanae Dan" kitabu ambacho kikauzika sana na kunifanya mimi kuweza kumtunza mama.
Nilirudi mpaka ile shule na kumulizia rafiki yangu yule ambaye alikuwa kipofu na kwa bahati mbaya niliambiwa alifariki kwa ajali ya gari baada ya kujitahidi kuvuka barabra kwa kukosa msaada na kugongwa na gari. Nililia sana na kuishia kubaki na yale aliyoniambia na mpaka sasa mimi na mama tuna shirika la kusaidia wajane na walemavu wa macho liitwale "fuata sauti yako foundaton"
Kwa nini nimetaka kuandika kisa hiki cha kufikirika?
Kila mtu ana historia ya mapito magumu katika maisha yake na pengine hata sasa una wakati mgumu sana na hujui nini cha kufanya.
Hebu fikiri wakati mama yangu ananyanyasika na kufanya kazi kwa taabu ili kunipa maisha mimi aligundua kuwa ana tone la furaha na kulitumia ipasavyo hasa zile nyakati za kwenda kanisani na kuimba na wenzake na kusahau maumivu ya muda na kujipanga kuona atayakabili vipi.
Mama Fred yeye hakuwa na fedha sana na alikuwa ni maskini kama sisi lakini vile viatu ambavyo alinunua na kunipa pamoja na yale maneno mazuri vilinihamasisha kufanya vizuri. Je wewe umekuwa msaada kwa wenzako hata kama na wewe unaona huna kitu? Umewapa maneno ya faraja au umekuwa ukifurahia magumu yao?
Yule kipofu aliomba msaada na wengi wakawa wakimwangalia na kumcheka je ni mara ngapi na wewe umeomba msaada na watu na kuchukulia ni utani na kuja kujutia baada ya kugundua kuna mtu ulishindwa kumsaidia katika nyakati aliyohitaji msada wako?
Ni mara ngapi umewasamehe wale waliokufanyia mabaya na hata kuwafanyia mabaya wale uwapendao mbele yako kama nilivyomshuhudia baba akimnyanyasa mama na mwisho wa siku nikamsamehe ingawa alifariki baadae hata kabla ya kuja kula mafaniko ya mwanae?
Ni mara ngapi umesaidiwa na kuwa na shukrani hata ya maneno mazuri kama vile yule kipofu alivyomfanyia dan na hata kujenga imani ya kuwa huyo mtu aliyekusaidia unahitaji kumwamini na kuuthamini mchango wake?
Ni mara ngapi umerudi kuwashukuru wale waliokusaidia nyakati za shida au ulivyowahitaji wakusaidia na wakakusaidia?
Katika kufanikiwa kwako au katika jitihada za mafanikio yako umefuata sauti liyomo ndani yako kuwa utafanikiwa na ukaishi kwa ndoto zako huku ukijituma na kujikabidhi kwa mungu ?
Baada ya kila dhoruba kali nuru huonekana ....... nakutakia wiki hii kuwa ya mafanikio kwako......AMEN-------------> share ------------>

MAMBO AMBAYO KIJANA WA SASA UNATAKIWA KUWA MAKINI NAYO SANA.....

MAMBO AMBAYO KIJANA WA SASA UNATAKIWA KUWA MAKINI NAYO SANA.....
1. Epuka na ujitoe kabisa kutoka katika Kundi la watu wenye mitazamo hafifu juu ya maisha yao.
2. Acha kuwa king'ang'anizi kwa wale waliokutenga katika maisha yako.
3. Kuwa mtu wa haki na upendo hata kwa watu usiowajua.
4. Kuwa mtu wa heshima na upendo kwa kila mtu.
5. Kubali kuishi na watu kwa jinsi walivyo na sio wewe utakavyo.
6. Wahamasishe wenzio kufanya mambo yenye mafanikio na furahia mafanikio yao bila unafiki.
7. Kuwa mtu wa kuaminika kwa kila ukifanyacho
.
8. Samehe watu na endelea na maisha yako bila kuwafikiria tena
.
9. Kila siku fanya kitu kidogo kizuri kwa watu wakuzungukao
.
10. Kuwa makini na mwangalifu kwa hao unaowaita marafiki
.
11. Daima kuwa mkweli
.
12. Wasialiana na kuwa karibu na watu unaowajali katika maisha
.
13. Kuwa mtu wa kitimiza ahadi zako na kuwa mkweli
.
14. Toa kitu amabo nawe unatarajia upokee
.
15. Sema unachomaanisha na maanisha unachosema
.
16. Uwe mtu wa kukubali na wengine watoe maamuzi
.
17. Ongea kidogo na kuwa makini nkatika kusikiliza
18. Usiwe mtu wa mabishano kila mara yasiyo na tija
.
19. Achana na umbea au maneno yanayoweza kuja kukunyima furaha
.
20. Uwe makini na mahusiano yako mwenyewe na mahusiano yako na MUNGU

Kama ulikuwa hujui kuhusu yanayotokea makaburini, basi soma hii


Makaburini ndiko sehemu tajiri kuliko sehemu yoyote ile hapa duniani. Ni sehemu pekee ambako ndoto nyingi za watu mbalimbali zimezikwa nao.
Wengi wao walikufa kabla ya kufanikisha malengo na baadhi walikufa wakiwa hawajathubutu kujaribu kutimiza ndoto zao na kujikuta wakifa wakiwa maskini.
Jambo hili linanikumbusha ule msemo kuwa " WATU WENGI HUFA WAKIWA NA MIAKA 25 NA HUJA KUZIKWA WAKIWA NA MIAKA 50 NA KUENDELEA"
Maana yake tunakufa kifo cha kwanza katika umri wa miaka 25, umri ambao kwa kawaida mtu yoyote anatakiwa kuanza kuhangaika kwa kujutuma na kwa uthubutu ili kufa kufanikiwa.
Lakini kwa kuwa tunashindwa kuchukua hatua basi kuanzia hapo tunajikuta tunaisha maisha ambayo hatukuyatarajia na hatuyapendi yaani kwa kifupi maisha yasiyoeleweka.
Jamani tujitume na kufanya uthubutu muda huu............
kama mie nimethubutu kunywa kakonyagi asubuhi hii ...

Jihadharini na wachapaji wa kadi za harusi

*Jihadharini na wachapaji wa kadi za harusi.* 
Hakikisha unasoma maandishi yaliyochapwa kabla ya kadi kuchapwa na kusambazwa!
*Mchapaji* aliombwa aweke 1Yohana 4:18 ktk kadi ya harusi lakini mchapaji kwa makosa aliweka Yohana 4:18.
1 Yohana 4:18 panasema, *"Katika pendo hakuna hofu, lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu..."*
Lakini Yohana 4:18 tunasoma, *"Kwa maana umekuwa na waume watano , naye uliye naye sasa siye mume wako."*

Hatimaye akaolewa na yule mwanaume aliyempenda kwa mika 10...........SOMA NI NZURI



Hatimaye akaolewa na yule mwanaume aliyempenda kwa mika 10..

Mwishoni kabisa mwa tafrija fupi waliyoandaliwa na familia, mama yake alimwita pembeni na alimpa zawadi ya kitabu cha benki kilichokuwa na milioni mbili za kitanzania alizokuwa ameziweka. 

Mama akamwambia mtoto wake pekee wa kike, "Mwanangu, tafadhali chukua hiki kitabu cha benki.Kitunze kama kumbukumbu yako ya maisha ya ndoa. 

Kikitokea kitu kizuri katika maisha yenu na ambacho ukaona ni kumbukumbu basi wewe weka kiasi chochote cha fedha kwenye akaunti hii. Andika chini kitu hicho ni  nini na kiwango cha fedha ulichokiweka.

Jinsi utakavyokuwa na matukio mengi ya furaha basi kumbuka ndio hivyo hivyo na fedha zitaongezeka katika akaunti hii kwa jinsi utakavyoweka. Mimi nimekuanzia kwa kuweka fedha katika akaunti hii kutokana na tukio hili kubwa la wewe kuolewa. Matukio mengine naomba ushirikiane na mmeo kuhakikisha mnayaweka katika kumbukumbu kwa jinsi mlivyoyafurahia pamoja” 

Alipofika nyumbani akamshirikisha mmewe usiku ule alimshirikisha mmewe na wote walilifurahia jambo lile na kuona ni wazo jema sana. Kitabu chao cha benki kilionekana hivi baada ya miezi michache…

- February 7 – 200,000: Kumbukumbu yake ya kwanza ya siku ya kuzaliwa baada ya ndoa
- March 1 – 600,000: Aliongezewa msharaha kazini
- March 20 – 400,000: Shukrani ya kurudi salama kutoka mapumzikoni Kilolo
- April 15 – 4,000,000: Ana ujauzito!
- June 1 – 2,000,000: Alipandisha cheo na kuwa meneja kazini kwake

Mambo yaliendelea kuwa hivi kila tukio lilipojitokeza lenye furaha...

Ingawaje, miaka ilivyozidi kuyoyoma wakajikuta wakianza kupigana na kupigizana kelele kila kukicha.Hawakuongea tena sana kama hapo awali, kila muda walijilaumu kuoana na ule upendo wa awali ukatoweka kabisa.

Siku moja mke akampigia simu mama yake na kumwambia, "Mama, hatuwezi kuendelea na ndoa hii. Tumeamua kupeana talaka. Nashindwa kuamini nini kilinikuta nikaona na huyu mwanaume!”

Mama akamjibu, "Fanya lolote utakalo mwanangu,kama ni kweli umeshindwa kuvumilia. Ila kabla ya kufikia uamuzi huo kuna kitu naomba ukifanye kwanza.Unakumbuka kile kitabu cha benki nilichokupa wakati wa harusi yako? Tafadhali naomba ukachukue fedha zote na uzitumie kwani hutakiwi tena kuwa na kumbukumbu za maisha ya ndoa ambayo yana mwisho mbaya kama huo wako."

MKe alikubaliana na mama yake na akaenda siku ya pili yake benki wakati huu alikuwa kwenye mstari akisubiri nafasi yake ili akatoe fedha zote na kuifunga akaunti ile. Akiwa pale kwemye mstari anaisubiri zamu yake akaona achukue kile kitabu na kuangalia kumbukumbu za matukio yao ya furaha na kiasi cha pesa kilichowekwa. 

Aliangalia tena na tena kwa muda kisha zile kumbukumbu za yale matukio yote yenye furaha zikamrudia. Wakati huo macho yake yakawa yamejawa na machozi hivyo akaamua kurudi nyumbani. 

Aliporudi nyumbani akampa mmewe kile kitabu na kumwambia mmewe akazitumie zile fedha zote kabla ya wao kupeana talaka.

Siku ya pili mme akawasili benki, na tukio lililomtokea mkewe jana yake likamtokea pia mmewe. Alizidiwa pia na furaha ya matukio mazuri nay a kumbukumbu aliyoyafanya na mkewe katika kipindi cha ndoa yao na kumfanya arudi nyumbani machozi yakiwa yanamlengalenga.

Alipofika nyumbani akampa kitabu mkewe na kulikuwa kuwa fedha mpya imeingizwa katika akaunti hiyo (5,000,000) ikiwa na maneno, “Leo ndio siku ambayo nimegundua kuwa nakupenda sana mke wangu katika miaka yote tuliyokaa pamoja na jinsi ulivyonipa furaha katika maisha haya”

Wakakumbatiana na kulia kwa pamoja.KItabu chao kikarudisha katika sanduku lao maalumu na kuendelea kutunzwa huko

AMKA TOKA NDOTONI MAPENZI KAMA HAYA HAKUNA WEWE ENDELEA KUOTA TUU

Ila share

Amri kumi za kukumbukwa kwa mabinti wote single duniani



1. Usiharakishe kutoka nyumbani kwa wazazi wako kwa gia ya kwenda kuolewa.
2. Usimsubiri mwanaume mpaka aje  ndio uanze kuishi. Unaweza kuishi maisha timilifu hata ukiwa huna mwanaume.
3.Achana na pombe zimewauwa wenzako wengi kwa kisingizio cha kuondoa stress na wewe unaweza kufa pia.
4. Usiwe mtu wa kuendekeza kuzipokea na kuzijibu namba ngeni za simu hasa nyakati za usiku.. sio njia sahihi ya kupatia mpenzi.
5. Tengeneza mazingira ya kuilinda afya. Jitahidi kunywa chai asubuhi maji mengi  na acha kula vitu vitamu
6. Vaa vizuri na kiheshima. Watu watavutiwa na wewe ulivyo kabla ya kuongea nawe
7.Usitumie sex kama ndio mzani wa mapenzi.Unaweza ukaachika tuu pamoja na penzi lako taamu.
8. Usiolewe na mtu kwa sababu ya fedha; Utabakia kuwa mtumwa wake
9. Jiongezee ubora wako, Tafuta kazi.Usiwe mpuuzi ukaamini mwanaume atatatua matatizo yako yote.
10. Jiheshimu sana kwa kuangalia namna ya uvaaji wa mavazi yako na mwonekano wako mbele ya jamii…. Usitegemee kuvaa kimini ukutane na mwanaume wa suti… wewe utampata wa milegezo na kubana pua tu.

MAMBO YANAYOWAKERA WAKE



1. Wababa wenye madaraka kuyapeleka madaraka nyumbani
2. Wake kuwajibika na mambo ya nyumbani kwa vile wana mishahara minono
3. Wababa kutotenga muda wa kutosha kukaa na wake zao ili kuongea yanayowahusu
4. Mume kumwachia mke kulea watoto hasa wakati wa usiku
5. Mume kutomtia moyo mke wakati wa ujauzito
6. Mume kumchanganya mama na watoto wa kike wanapokosa
7. Mume kutokuwa na maandalizi mazuri wakati wa kukutana kimwili na mkeo
8. Mume kujijari mwenyeweMume kusaidia ndugu zake bila mke wake kujua
9. Mume kubagua watoto
10. Mume kuwa na upendo na ukaribu au kucheka na binti waishio nao huku yupo mke wake
11. Mume kutomshirikisha mkewe katika huduma yake ya ili aweze kumwombeaKutoonesha shukrani wala kutokuwa na msamaha
12. Mume kutomtazama mkeo usoni mkiwa chumbani.

KWA WALE MSIO IJUA TANZANIA VIZURI SOMENI KWA MAKINI UTAJIRI WA TANZANIA HALAFU JIULIZE KWA NINI NI MASIKINI WA MWISHO NA MALI ZOTE HIZI




KWA WALE MSIO IJUA TANZANIA VIZURI SOMENI KWA MAKINI UTAJIRI WA TANZANIA HALAFU JIULIZE KWA NINI NI MASIKINI WA MWISHO NA MALI ZOTE HIZI👇👇👇

😰😭😁😳






1.Tz ilipata uhuru mwaka 1961 ina miaka 54 tangu ipate uhuru ikiwa ni ya kwanza Afrika Mashariki.
2.Tz Kwa miaka 38 imeongozwa na CCM peke yake ambayo ni zao la TANU na ASP.
3.Tz ni nchi ambayo haijawahi kupata majanga makubwa kama matetemeko ya ardhi, magonjwa
ya mlipuko kama ebola, mafuriko na vimbunga au ukame.
4.Tz ni nchi ambayo imekuwa na kitu ambacho nchi za Afrika zimekikosa. Kitu hicho ni AMANI. Kwa miaka yote 54 ya uhuru haijawahi kupigana vita vya wenyewe kwa wenyewe.
5.Tz ina ukubwa wa 945,000 km za mraba yani sawa na uchukuwe Denmark, France, United Kingdom, Netherland, Ireland ujumlishe zote kwa pamoja.
6.Tz ina eneo la bahari lenye ukubwa wa 1,424 km. Bahari inaleta fursa za usafirishaji, uvuvi, utalii na nyinginezo.
7.Tz ni nchi ambayo imepakana na nchi za (Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia, Malawi, D. R. Congo) ambazo zinategemea bahari yetu kwa usafirishaji wa mizigo na ni fursa nzuri ya kuzipelekea bidhaa za viwanda vyetu.
8. Tz ina maziwa makubwa manne na mengine madogo mengi.
Maziwa matatu makubwa yako kwenye kumi bora za ukubwa duniani na Maziwa makubwa matatu yote yapo Tanzania. Ziwa Victoria ni la tatu kwa ukubwa duniani (la kwanza Afrika) na ziwa
Tanganyika ni la sita kwa ukubwa (la pili Afrika) na la kwanza kwa kuwa na kina kirefu duniani. Ziwa Nyasa ni la tisa kwa ukubwa duniani (ni la tatu Afrika).
9.Tz ina mito mikubwa kumi ambayo ni mto Kagera, mto Ruvuma, mto Rufiji, mto Wami, mto Malagarasi, mto Mara, mto Pangani, mto Ruaha, mto Gombe, mto Mweupe wa Nile na ina mito midogo mengi kama mto Kilombero, mto Mbemkuru n.k
10.Tz ndiyo nchi ya kwanza Afrika kuwa na maji mengi yasio na chumvi yaliyokuwa kwenye uso wa dunia (fresh surface water) kutokana na kuwa
na mito na maziwa mengi na kupitiwa na bonde la ufa.
11.Tz ni nchi ya nne kwa uzalishaji dhahabu Afrika baada ya Afrika Kusini, Ghana na Mali na ipo TOP 20 duniani. Kuna migodi nane inayochimbwa dhahabu na miwili imefungwa. Migodi inayochimbwa ni Buzwagi gold mine- (Shinyanga), Geita gold mine-(Geita), Golden pride gold mine-Nzega (Tabora), Bulyanhulu gold mine- (Shinyanga). New leuka Gold mine- (Mbeya),
Tulawaka gold mine-(Kagera), North mara gold mine-(Mara). Iliyofungwa ni Korandoto gold mine (Shinyanga), Senkenke gold mine-(Shinyanga???).
12.Tz ina madini ya almasi yanayopatikana Mwadui Shinyanga. Mgodi huo ulianza kuchimbwa tangu mwaku 1940. Mpaka leo bado unachimbwa, unamilikiwa na kampuni ya Waingereza.
13.Tz ni nchi ya kwanza na ni nchi pekee inayozalisha madini ya tanzanite duniani. Mkufu wa kuvaa shingoni unatengenezwa na tanzanite na almasi unauzwa hadi shilingi milioni 25 za Kitanzania.
14.Tz ina madini ya chuma yanayopatikana Mchuchuma, Ludewa- Njombe mgodi unamilikiwa na Wachina. Mgodi huo una hifadhi ya madini ya chuma tani milioni 122 ambayo yanawezwa kuchimbwa kwa zaidi ya miaka 100.
15.Tz ina madini ya makaa ya mawe (Coal) yanayochimbwa Kiwira Mbeya, Mchuchuma na
Liganga Njombe. Unamilikiwa na Wachina. Pia mgodi wa Ngaka kule Mbinga-Ruvuma unamilikiwa na
kampuni ya Tancoal ya Australia. Hifadhi ya madini ya makaa ya mawe iliyopo ni tani bilioni 2. Makaa ya mawe ndio chanzo cha pili cha umeme wa bei nafuu duniani baada ya maji.
16.Tz ina hifadhi ya madini ya Uranium kule Dodoma (Bahi) na ni mgodi ambao unamilikiwa na
Warusi. Pia madini haya yanapatikana Namtumbo (Mkuju), Galapo, Minjingu, Mbulu, Simanjiro, Lake Natron, Manyoni, Songea, Tunduru, Madaba and Nachingwea.
17.Tz ni moja ya nchi tatu Afrika zikiwemo Zimbabwe na Madagascar kwa kuwa na madini mengi ya graphite. Madini haya yapo Tanga, Mahenge-Morogoro, Mererani- Manyara. Madini ya graphite ndiyo yanayotumika
kutengenezea betri za simu, kwenye injini na brake za magari na kwenye karamu za risasi (pencili).
18.Tz ina madini ya nickel yanayopatikana kule Kabanga Kagera, milima ya Uluguru-Morogoro, North Mara, Ngasoma-Mwanza.
19.Tz ni nchi ya tatu duniani kwa kuwa na hifadhi kubwa ya magadi soda duniani baada ya Marekani na Uturuki. Magadi soda hutumika kutengeneza vioo vya aina zote. Vioo vya nyumbani hadi magari pia kutengeneza sabuni na dawa mbalimbali za usafi.
20.Tz ina hifadhi na mgodi wa madini ya niobium uliopo Panda hill Mbeya ambao ndio utakuwa mgodi mkubwa wa kwanza Afrika na wa nne duniani. Mgodi huu unamilikiwa na kampuni ya Australia. Madini ya niobium ni magumu sana
hutumika kutengeneza mabomba pamoja na madini chuma pia hutumika kutengeneza baadhi ya sehemu za injini za ndege na vyombo vinavyoenda nje ya uso wa dunia (mfano Apollo 15 CSM), vioo vya computer na lenzi za camera.
21.Tz ni nchi ya kwanza Afrika na ya pili duniani kwa kuwa na vivutio vingi vya utalii. Ya
kwanza ni Brazil. Nchi zilizokuwa kwenye tano bora kwa utalii Afrika ni Tanzania, Botswana, Afrika Kusini, Kenya na Zambia.
22.Tz ina mbuga zipatazo 16 na ile mbuga maarufu kuliko zote duniani Serengeti ipo Tanzania, mbuga iliyopakana na bahari iitwayo Saadani ipo Tanzania na mlima mrefu kuliko wote Africa Kilimanjaro upo Tanzania.
24. Tz ina ardhi kubwa yenye rutuba na inayofaa kwa kilimo cha mazao mengi tofauti tofauti. Mashamba makubwa ya mpunga kwa mfano yaliyokuwa chini ya Shirika la NAFCO yalitoa mazao ya kulisha Tanzania na pia nchi nyingine.
24.Tz ina gesi ya asili ya Carbon Dioxide (CO2) inayovunwa kule Kyejo, Rungwe-Mbeya na kampuni ya TOL. Gesi ya asili ya cardon dioxide inatumika sana kutengenezea vinywaji laini kama soda, bia na pia kutengenezea madawa, makaratasi na kutibia maji (water treatment).
25.Tz ina gesi ya asili inayopatikana katika kisiwa cha Songo songo mkoa wa Lindi. Gesi hii imekuwa ikichimbwa na kusafirishwa hadi Dar es salaam tangu mwaka 2004. Inamilikiwa na kampuni ya Songas ya Uingereza.
26.Tz imengundua gesi ya asili yenye zaidi ya meta za ujazo trilioni 55.3 iliyongunguliwa katika maeneo ya bahari ya Hindi na Mtwara.
Pamoja na sifa zote hizi lakini Tz ni nchi iliyo kwenye kundi la nchi maskini duniani ambayo asilimia kubwa ya raia wake wanaishi chini ya Dola moja za Marekani na hali ya huduma za kijamii ikiwa duni.
TATIZO NI NINI? NANI ANAFAIDI HUU UTAJIRI? NANI WA KUMLAUMU? NANI NI SABABU?
KWA NINI TUNASHINDWA KUTUMIA HUU UTAJIRI?

Jinsi jamaa alivyoponea kuliwa na simba kisa ubishi



Miaka mingi iliyopita mfalme mmoja alikuwa na mtumishi wake ambaye alibahatika kuwa mcha Mungu sana.

Lakini mfalme huyo alikuwa haamini kabisa kuwa kuna Mungu zaidi ya miungu yake aliyokuwa akiiabudu.

Alichukizwa sana na mtumishi huyo hasa alipokuwa akilitaja jina la Mungu kila aliposhukuru au kutaka kuomba ulinzi wa jambo fulani au baada ya jambo fulani kumtokea.


Taratibu yule mtumishi akaanza kumwelezea mfalme huyo juu ya Mungu wa kweli lakini mfalme alikuwa mkali na hata kumpa adhabu kali.

Siku moja wakawa wameenda kuwinda na walipokuwa huko waka koswakoswa kuuawa na nyati na yule mtumishi akaanza kusali akimshukuru Mungu lakini mfalme alichukizwa zaidi Na kumwambia mtumishi huyo kuwa Mungu hajahusika hapo zaidi ya wao kuwa hodari wa kukimbia na wakarudi nyumbani.

Siku nyingine wakiwa wanawinda mara simba akatokea na kumdaka mfalme na yule mtumishi akafanikiwa kumuua yule simba ingawa mfalme alijeruhiwa kidole chake kimoja cha mkononi na kuvunjika.

Mfalme akachukia zaidi kwa jinsi mtumishi huyo alivyokuwa mzembe wa kumwokoa mpaka akaliwa kidole, lakini mtumishi akasali kushukuru kuwa mfalme hakuuawa.

Waliporudi nyumbani mfalme akaamuru mtumishi huyo afungwe gerezani baada ya kusababisha uzembe uliotaka kuhatarisha maisha ya mfalme na kweli mtumishi akafungwa gerezani

Siku nyingine mfalme akaenda peke yake mwituni kuwinda na alipofika huko akakamatwa na watu amabo huwashika watu na kuwatumia kwa ajili ya sadaka za miungu yao kama sala zao.

Kwa mara ya kwanza mfalme yule akasema Mungu wangu naomba niokoe na walipofika watu wale sehemu ya kutolea sadaka mfalme aliachiwa huru kwa sababu hakuwa na viungo vyote yaani hakuwa timilifu kwani kidole mkimoja hakuwa nacho.

Mfalme aliporudi akaamuru yule mtumishi afunguliwe na alipoletewa akamwambia, " Ndugu unajua leo nilikamatwa na watu porini nikiwa nawinda na wakanipeleka mpaka kwenye sehemu ya kutolea sadaka yao na miungu yao ikanikataa kwa kuwa sikuwa na kidole kimoja yaani sikuwa kamili ni kama kilema sadaka isiyo kamili, hakika nimeamini Mungu wako ana nguvu"

"Mfalme wangu, nilikuambia kila kitu kinatokea kwa sababu na Mungu hujua yote haya, maana leo usingekuwa umenifunga tukaenda wote mimi ndio ningetolewea sadaka"

Kila kitu hutokea kwa sababu

MUHIMU KUJIKUMBUSHA HAYA KUHUSU MFALME DAUDI

Siku moja mfalme Daudi akiwa katika moja ya vyumba vyake kupitia dirishani alimwona mwanamke mmoja nyumba jirani akiwa anaoga.
Daudi akampenda sana na kuwatuma watumishi wake wakatafute habari zake nao waliporudi wakamwambia kuwa yule ni Bath-sheba mke wa Uria ambaye ni jemadari wa vikosi vya israel.
Mfalme Daudi akaomba binti yule apelekwe katika jumba la kifalme na akalala naye.Baada ya siku kadhaa yule binti akapeleka ujumbe kwa mfalme Daudi kuwa alikuwa na mimba yake.
Daudi akapeleka ujumbe kwa mkuu wa vikosi vilivyokuwa vitani Yoab kuwa amwambie Uria arudi mara moja. Uria akafika na baada ya kuulizwa hali ya vita mfalme Daudi akampa baadhi ya zawadi na kumruhusu aende nyumbani akijua angelala na mkewe na mimba ikawa yake.
Asubuhi akashangaa baada ya kuamka na kuambiwa Uria na watu wake hawakwenda majumbani mwao ila walilala mlangoni pake.
Mfalme akamwita Uria na kumuuliza kwa nini hukwenda kulala kwako? Naye akajibu kuwa kamwe nisingeweza kwenda kulala na kufurahi nyumbani wakati kuna watu wako vitani wakiumia.
Wakalala pale na siku ya pili Uria akaondoka kurudi vitani bila kwenda kwake na ndipo mfalme Daudi akatuma ujumbe kwa yoab kuwa uria apangwe mstari wa mbele kwenye mashambulizi makali na kisha wenzake wamwache apigwe hadi kufa.
Yoab akafanya hivyo na baada ya muda wa maombolezo ya kifo cha Uria kwisha, Daudi akamchukua Bath-sheba na kumfanya mke wake ndani ya jumba lake na akamzalia mtoto.
Mungu akamtuma Nathan na kumwambia Daudi, “Palikuwa na wanaume wawili waliokuwa katika jiji moja, mmoja alikuwa tajiri na yule mwingine alikuwa maskini.
Yule mwanamume tajiri alikuwa na kondoo na ng’ombe wengi sana; lakini yule mwanamume maskini hakuwa na chochote isipokuwa mwana-kondoo jike mmoja, aliye mdogo, ambaye alikuwa amenunua.
Naye alikuwa akimhifadhi hai, na huyo kondoo alikuwa akikua pamoja naye na wanawe, wote pamoja. Kondoo huyo alikuwa akila tonge lake, na kunywa kutoka katika kikombe chake, naye alikuwa akilala kifuani pake, na kondoo huyo akawa kama binti kwake.
Baada ya muda, mgeni akaja kwa yule mwanamume tajiri, lakini hakuchukua kutoka kati ya kondoo zake na ng’ombe zake ili kumwandalia yule msafiri aliyekuja kwake. Kwa hiyo akachukua yule mwana-kondoo jike wa yule mwanamume maskini, akamwandalia yule mtu aliyekuja kwake.”
Ndipo hasira ya Daudi ikamwakia sana yule mwanamume, naye akamwambia Nathani: “Kama Yehova anavyoishi, mtu huyo aliyefanya hivyo anastahili kufa Na kuhusu yule mwana-kondoo jike, atamlipa mara nne, kwa sababu yeye amefanya jambo hili na kwa sababu hakuwa na huruma.”
Ndipo Nathani akamwambia Daudi: “Wewe mwenyewe ndiye yule mwanamume!
Basi Daudi akamwambia Nathani: “Nimemtendea Mungu dhambi.” Kwa hiyo Nathani akamwambia Daudi: “Yehova naye ameacha dhambi yako ipite. Hutakufa. Ingawa hivyo, kwa kuwa bila shaka hukumheshimu Yehova kwa jambo hili, pia yule mwana, uliyemzaa, atakufa hakika. Kisha Nathani akaenda zake nyumbani kwake.
Na Mungu akampiga yule mtoto ambaye mke wa Uria alikuwa amemzalia Daudi, akawa mgonjwa.
Mfaleme daudi akafunga akilala chini na kumwomba Mungu amponye yule mtoto huku akilia na hata wafanyakazi wake walipotaka kumnyanyua yeye alikataa akiendelea kuomba kwa siku kadhaa.
Siku moja watumishi wake wakawa wananong'onezana jinsi ya kumwambia daudi kuwa mtoto yule amekufa. Wakasema kama wakati akiwa hai aliomboleza vile itakuaje kusikia amekufa?
Daudi akagundua wakiwa wananong'onezana akawauliza amekufa? wakajibu ndio... ndipo akanyanyuka na kwenda kuoga, akavaa mavazi mapya , akaenda nyumba ya bwana kusujudu na kisha akaomba aletewe mkate wale watumishi wakashangaa na kumuuliza,
“Ni nini maana ya jambo hili ambalo umefanya? Ulifunga na ulikuwa ukimlilia mtoto alipokuwa hai; na mara tu mtoto alipokufa ukasimama, ukaanza kula mkate.”
Daudi akajibu, “Nilifunga, nikawa nikilia mtoto alipokuwa bado hai, kwa sababu nilisema,
‘Ni nani anayejua kama Yehova huenda akanipa kibali, na hakika mtoto aishi?’ Sasa kwa kuwa amekufa, kwa nini nifunge?
Je, ninaweza kumrudisha tena? Mimi nitakwenda kwake, lakini yeye hatarudi kwangu.”
Na Daudi akaanza kumfariji Bath-sheba mke wake. Na zaidi ya hayo, akaingia kwake, akalala naye. Baada ya muda akazaa mwana, naye akaitwa jina lake Sulemani. Na Yehova akampenda mwana huyo. Basi akamtuma Nathani na kumwita jina lake Yedidia, kwa ajili ya Yehova.
Funzo
*Hakuna kitu kibaya kama tamaa ya kutaka kutamani mali isiyo yako na kuichukua kwa hila kama mfalme daudi alivyoweza mpokonya mke wa uria na kisha kuamuru Uria awekwe mstari wa mbele katika mapigano ili afe
*Mungu akiamua kukuumbua huwezi jificha hebu fikiri jinsi Daudi alivyoamua kutumia ujanja wa kumrudisha Uria ili alale na mkewe na mimba ionekane yake lakini bado ikashindikana na pia jinsi alivyomtuma Nathani na kwenda kumpa daudi mfano uliogua tukio lake
*Mungu pia huchukizwa na dhami za tamaa kama alivyoweza kumadhibu daudi na kumuua yule mtoto
*Kwa kula anguko ni muhimu sana kumrudia mungu wako kama vile daudi alivyolitambua kosa lake na kisha kuomba msamha kwa Mungu wake wa kweli
*Ni vizuri kuacha mambo yapite na kutoyakumbuka kama vile mfalme daudi baada ya mtoto kufa alivyosahau na kuanza maisha mapya na kisha kuja kupata mtoto sulemani ambaye pia Mungu alipendezwa naye na baadae alikuja kuwa mfalme mwenye hekima
Ni vyema tuutumie mfano huu wa Daudi kusahihisha maisha yetu na jinsi tunavyoishi na jamii inayotuzunguka na matendo yetu kwao.
Kama umeelewa comment Amen na kisha share

Kamwe sitosahau jinsi mme wangu alivyonifunga kizazi kishirikina kwa miaka mingi



Miaka kumi na mbili iliyopita binti huyu pichani aitwaye Dear alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na kijana mmoja wakiwa na umri wa miaka 18.
Walipendana sana na kuapiana kuwa wasingesalitiana na kuja kuishi kwa pamoja kama mme na mke baada ya kuhitimu masomo yao.

Binti akatoa wazo kwa kuwa yeye hana imani na wanaume, kwani wengi huwa na tabia za kusaliti mahusiano basi waape kwa kitumia Biblia na kofuli.

Wazo hili kijana alilipokea kwa furaha na binti akafurahi sana kuona yule kijana amekubaliana nae kuwa ataapa kwa njia hiyo kama ishara ya kuwa hawatasalitiana na kupendana kwa dhati.

Wakaondoka wakiwa na biblia na kofuli yao mpaka kwa mzee mmoja aliyeaminika kwa busara na kumweleza adhma yao naye kabla ya kuwakubalia ombi la kuwa shahidi wao akawauliza,

" Je ni kweli mmeamua kuapa kwa kutumia Biblia na kofuli hii kuwa mnaufunga uhusiano wenu kuwa wenu tuu na mnakubali kuwa hamtasalitiana milele?"

Wote wakajibu ndio.

"Je mnatambua kuifunga kofuli hii na ufunguo kuniachia mimi na kofuli kwenda kuitupa mbali mjue kamwe hamtaifungua tena na matatakiwa kuwa pamoja kwa namna yoyote ile?"

Wakasema tumeafikiana.

Mzee akawaongoza kwa sala na kuwaomba waishi kama walivyokubaliana na kisha kuifunga ile kofuli.

Wale vijana wakarudi majumbani kwao na kuendelea kuishi kwa furaha na amani huku kila mtu akiwa na kiu ya kuonyesha zaidi upendo kwa mwenzake.

Miaka ikaenda wakahitimu chuo na kijana akapangiwa kazi kijijini sana na kukawa na matatizo ya usafiri na binti kwa kuwa alipangiwa mjini akawa kila mara akimtembelea kijana na kijana akienda mjini pia.

Miaka ikaenda hatimaye taratibu wakaanza kupunguza mawasiliano baada ya kijana kuhamishiwa mbali zaidi na binti akabadili namba na kuanza mahusiano na boss wa kampuni yake na kisha wakaoana.

Kijana akafanya kazi kule kijijini kwa kujituma na kuweka fedha ili aweze kuja mnunulia pete nzuri ya uchumba na harusi yao ije kufana na waishi vizuri bila kujua kuwa keshaolewa.

Baada ya kujiandaa vya kutosha akaanza kuomba uhamisho ahamie mjini na alipofika mjini akapata habari za mkewe kuolewa na wamehama mji ule.
Kijana aliumia sana na kisha akaamua kuondoka kwenda mbali kuanza maisha mapya akiwa na huzuni sana.

Maisha ya furaha yakamwishia yule binti kwani hakupata mimba wala dalili na kila alipofanyiwa uchunguzi akaonekana yupo safi.

Furaha na amani ikaanza kumpotea katika familia yake na baadae mambo kuwa mabaya zaidi kabla ya kuanza kutembelea kila kibanda kilichoandikwa mganga wa jadi akihisi kafanyiwa mchezo.

Baada ya kwenda kwa njia hizo zote bila mafanikio akawa hana jinsi zaidi ya kuwa mtu wa kulia na kuhuzukika kila mara.

Siku moja akiwa ndotoni akaonyeshwa Biblia na ile kofuli akakumbuka kuhusu nadhiri yake na yule kijana. Akaanza kumtafuta yule kijana amwombe msamaha na baadae akampata.

Baada ya kumwambia kijana huku akimwomba msamaaa kijana akasema mimi sina tatizo ndio maana sikuoa ili nikuone na uje uniruhusu kwa kulingana na agano letu.

Na kilichobaki hapa ni kumtafuta mzee kwani kofuli mimi nilimkabidhi mama yangu na analo kwani niliamini mama ambaye ni mwanamke kama wewe angenirekebisha kama nikikosea na ajue siri yangu na wewe ili azidi kunipa hekima na busara ya kuwa na wewe, je na wewe funguo ya akiba uliweka wapi?

Binti akasema niliipoteza nilipoanza mahusiano na mme wangu.
Wakaenda kwa mzee na kusikia kuwa alishafariki, kijana akampa kofuli bila ufunguo na kumwomba binti ampe ruhusa akaoe.

Binti akakubali na kijana akaoa na sasa ana mke na watoto wawili lakini yule binti mpaka sasa kashaachika zaidi ya ndoa nne akikosa amani kwa kuvunja agano lake na kijana yule.

Dada na kaka zangu kumbukeni

1. Kamwe usimwahidi mtu kumpa mambo makubwa maishani na hali wewe huna uwezo

2. Kamwe usimwambie mwanamke unampenda wakati humaanishi

3. Usitumie vitabu vya dini kufanikisha mipango yako ya ulaghai wa mapenzi

4. Kamwe usiwahusishe watu kukusaidia kushuhudia uongo ili kumpata mwanamke...Hawa ni viumbe ambao kwa asilimia kubwa sisi wanaume ndio huwafanya waumie na kila mwanamke katili,jambazi, kahaba na wengine lazima wana hadithi iliyowafanya kuwa hivyo na ilisababishwa na mwanaume

5. Usijaribu kufanya ahadi yoyote ili kumpata mwanamke ukiapa kwa jina la Mungu kama huamini

Ukishindwa kutekeleza huishia kukosa furaha maishani mwako na kuwa kama dada yetu.

Comment "Nawachukia wasaliti' kisha share na like page hii ya  Fuledi