RIWAYA: MKONO WA JASUSI - 01


01

DAR ES SALAAM – Miezi Sita ilopita…

“KAMANDA Amata,” sauti iliita kutoka nyuma yake. Akageuka na kumwona Madam S akiwa na faili moja mkononi. Alikuwa amesimama katika sehemu ya mbele ya nyumba kubwa huko Gezaulole, mkono wake ukiwa na bandeji kubwa. Akageuka na kumtazama Madam S.
“Yes Mom,” akaitikia na kuitoa miwani yake usoni.
“Mheshimiwa Rais anakupongeza kwa kazi ulioifanya, anakubali sana uwepo wako hapa nchini na hususan katika idara nyeti kama hii, nimetoka kuzungumza naye sasa hivi, tumekubaliana jambo moja,” akamkabidhi lile faili ambalo juu yake lilikuwa limeandikwa Rhobinson Quebec na chini yake maandishi mazito ‘Wanted’, akatalizama na kumwangalia Madam S.
“Roho yake tu wala hatumwitaji akiwa hai,” kisha akageuka na kuondoka.
T.S.A MAKAO MAKUU – 1999
“Unakunywa chai au kahawa?” Gina alimuuliza swali Amata aliyekuwa ametingwa, macho kodo kompyutani akiperuzi hiki na kile.
“Swali lako hilohilo kila siku, na jibu langu lilelile kila mara,” akamjibu na wote wakacheka kwa sauti.
“Nyie kuna nini huko?” Madam S aliuliza akiwa tayari kasimama mlangoni.
Wote wakasimama kumpa heshima yake, “Karibu Madam, umeingia kama kivuli!” Kamanda akatania.
“Hata kivuli huonekana, sema kama hewa!” akajibu kisha wote wakacheka tena, “Kamanda Amata, uje ofisini baada ya mambo yako kuna jambo nikueleze na ulifanyie kazi,” akaondoka. Amata akamtazama Gina kisha wakaendelea na vicheko vyao na mabishano ya chain a kahawa.
“Madam anakuita ofisi, kuna kazi au?” Gina akaanza uchokozi.
“Hapana, kungekuwa na kazi angenikurupusha na ninyi nyote mngekuwa katka hekaheka ya kupanga kazi hiyo, itakuwa anataka kuniuliza kama nakuoa au la,” Amata akajibu.
“Mmmmmhh! Hiyo ndoa ya mi na wewe itakuwa ndoano,” Gina akaendeleza mazungumzo na kumpa Amata kikombe cha Kahawa.
Mbele ya kompyuta hiyo, Amata alikuwa ametingwa bila kuongea na mtu yeyote, hakuna aliyejua ni nini anakitafuta isipokuwa ni yeye peke yake. Alipokuja kumaliza kazi yake na kuinua macho alijikuta peke yake na kahawa iliyopoa mezani. Akainua walkie talk yake na kuita.
“We, njoo huku, tupo kwenye chumba namba tano,” Gina akamwita Amata hata kabla hajaambiwa lolote.
§§§§§
Ndani ya chumba hicho kulikuwa na watu wane, Madam S, Gina, Jasmine na Amata, waliketi wakitazama moja ya muvi nzito ya kipelelezi ambayo kwa roho yako nyepesi huwezi kuitazama mara mbili. Kwao muvi hiyo iliwafunza mengi sana hasa katika ukachero wa ndani na nje.
Ilikuwa ikionesha hatua thelathini na tisa za Kijasusi, kila mmoja alikuwa katulia kimya akifuatilia muvi hiyo ambayo kwayo ilikuwa na mafunzo mengi sana. Ilipomalizika baada ya dakika tisini, kila mtu alishusha pumzi ndefu na kumtazama Madam S aliyekuwa ameketi kimya mkono wake ukiwa umekuwa egemeo la kidevu chake. Akainuka akawatazama wote.
“Nakaribia kustahafu mama yenu, umri umenitupa mkono, kaeni tayari kwa lolote kutoka sasa. Kamanda njoo ofisini,”
Amata akainuka na kumfuata Madam S mpaka ofini kwake, ofisi pana yenye nafasi ya kutosha, ilikuwa na viti sita vya vono safi, meza kubwa ya mpingo iliyochongwa na vijana wa Suma J.K.T ilipendezesha ofisi hiyo. Ukutani kulining’inizwa picha kubwa ya Hayati Baba wa Taifa, na pembeni sana kulikuwa na picha ya mtu mmoja mwenye macho angavu yaliyoonekana kujua mambo mengi sana. Ukiitazama picha hiyo unaweza kuiuliza swali lakini ilikuwa picha. Kamanda Amata ijapokuwa alikuwa ni T.S.A 1 lakini bado katika ofisi hii aliingia mara chache sana. Picha iliyokuwa hapo ilimkumbusha Mogadishu alipokutana na mtu huyo The Chamelleon, alitamani kumwambia Madam S juu ya hilo lakini bado agano lake na marehemu bandia huyo lilikuwa ni kutunza siri.
Madam S akazunguka nyuma ya meza hiyo, akasimama mbele ya bendera kubwa ya taifa iliyokuwa kulia kwake na kushoto kwake kulikua na nembo kubwa ya T.S.A, nembo iliyobeba ngao ya Taifa na kunakshiwa kwa dhahabu safi kwenye kingo yake, juu yake kulitokeza kichwa cha Twiga ambacho kilitanguliwa na barafu ya mlima Kilimanjaro. Chini kabi say a nembo hiyo herufi tatu yaani T.S.A zilibebwa ju ya mikuki miwili iliyofanya alama ya X.
“Saa kumi jioni ya leo, kuna kikao nyeti Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, nitakwenda pale, lakini nataka nionane na wewe mara tu nikitoka, kama kuna lolote tofauti nitakushtua, uwe tayari muda wote,” Madam akamwambia akiwa amesimama wima.
“Yes! Madam, daima nipo tayari,”
“Kuna kazi kubwa Amata, ngumu sana mbele yako, itakayoweka maisha yako rehani kuliko siku zote, lakini huna budi kuifanya, nasi tutakuwa bega kwa bega na wewe,”
“Yes, Madam,” akajibu kwa ukakamavu.
“Sasa nakwenda kuonana na Mheshimiwa Waziri kisha nitakuita kiofisi ili tuone tunafanya nini katika hili, kwa maana hata mimi bado sijui ila nimedokezeaa tu juu yake,” Madam alimaliza maelezo yake.
§§§§§
Jioni ya siku hiyo ilimkuta kamanda Amata D.D.C Kariakoo akipata moja mbili baridi, akili yake ilizunguka kama pia, alijikuta akishikwa na donge kubwa la kujua nini kinataka kujiri katika ofisi yao. Alikwishazoea kuwa kazi zote huwa anaambiwa moja kwa moja na Madam S na kuianza muda huohuo lakini alishangaa kwa sasa Madam S anampa dokezo na kumwambia nitakuita baadae.
Bia ilishuka taratibu lakini haikuleta matata yoyote katika ubongo wa kijana huyo, ilishuka kama maji na kumtaka kwenda haja ndogo mara kadhaa. Muziki wa Kitanzania uliokuwa ukiporomoshwa na bendi ya Msondo ulimfanya japo kupoteza mawazo yake kwa nukta tu na si sekunde. Aliburudika kwa kuimba kidogo lakini mawazo yaliporudi katika lile analolisubiri kwa hamu. Aliitazama saa yake tayari ilitimu saa kumi na moja na nusu jioni, jua lilikuwa limeuacha mji na ukiliangalia lilichwea katika milima ya Pugu. Akanyanyuka na kupenya katikati ya watu, moja kwa moja akatoke kwenye lango la kutokea nje, akateremka ngazi na kuliendea gari lake aliloliegesha jirani kabisa na duka la Mhindi.
Alipoketi tu kitini simu yake ikaita, akainyanyua na kuichungulia, Chiba, akaifyatua na kuiweka sikioni.
“Vipi kijana, likizo imeisha?”
“Aaa ofisi zetu hazina likizo, dili likitokea popote na muda wowote unajiongeza man,” Chiba akajibu.
“Niambie!”
“Vipi hali ya hewa hapo ulipo?” Chiba akauliza.
“Pako shwari nimejificha kibandani, nyunyiza tu,” Kamanda akamwambia.
“Kaka kuna nini huko? Maana Madam kanambi nirudi, hapa nilipo tayari niko Uwanja wa Ndege wa Mauritius narudi,” Chiba akaeleza.
“Aaah! Huyu bibi naona anazeeka sasa, mi mwenyewe kanambia nisubiri ataniita,” Kamanda akamjuza.
“Ok, saa nne zijazo nitakuwa Dar kaka,”
“Na motto wa Ki-Mauritius?” Kamanda akatania.
“Hapana, mwenyewe tu, hayo nayaacha hukuhuku, over!” Chiba alimaliza kuongea, kwa kusema neno hilo over alimaanisha maongezi yasiendelee.
“Tuonane Ruvuma mpaka Maputo dakika 500 zijazo, over!” Kamanda akakata simu na kurudisha mahala pake, kisha taratibu akaingiaza barabarani na kuondoka eneo hilo. Daima hakupenda kukaa eneo moja kwa muda mrefu. Alaiingia barabara ya Msimbazi na kuelekea Faya, pale akakunja kulia kufuata barabara ya Morogoro mpaka karibu na Chuo cha Ufundi cha Dar es salaam akakunja kushoto akachukua barabara ya vumbi ya Ally Khan, akapita Zanaki na kuendelea mpaka mgahawa wa Red Carpet, akaegesha gari yake nje na kuteremka, akaangaza macho huku na kule kisha akaufunga mlango huku funguo ya gari akiwa kaiacha ndani.
§§§§§
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
“Madam S,” Mheshimiwa Francis Kifaru aliita kwa sauti yake nzito iliyoelemewa na unene uliopita kiasi. Daima alikuwa akiketi kama anayesinzia kutokana na umri uliopitiliza. “Wazee kama hawa wastahafu tu, wanang’ang’ania madaraka mpaka wafie maofisini, ndio maana nch haiendelei” Madam aliwaza.
“Ndio Mheshimiwa,” akaitika.
“Kama nilivyokuambia, hilo na hao jamaa wametuomba kuwasaidia na si kama tuwaombavyo basi ni zamu yetu, naamini idara yako itafanya vizuri,” Yule Mzee alitoa maelekezo na kumpa Madam S kabrasha lenye karatasi kadhaa ndani yake juu likiwa na maandishi Siri Nzito, akalitazama haraka haraka na kuliweka vyema.
“Ok, kazi imefika mahala pake na itatekelezwa,” akajibu na kumuaga mzee huyo, kisha akatoka nje.
Alipoketi garini, akatulia kwanza, “safi sana, sasa kazi ni moja tu, nilikuwa namuwaza sana mshenzi huyu” Madam S akajiwazia huku akiondosha gari yake maegeshoni.
§§§§§
Musanda, Pretoria - a.kusini
DUMISAN SAJAK MBEKHI, kiongozi mkuu wa Idara ya Kijasusui ya Afrika ya Kusini (N.I.A) alitulia tuli kama aliyegandishwa na barafu katika meza yake kubwa hapo ofisini. Giza lilikuwa tayari limeutawala mji huo wa Pretoria mju wenye amani na utulivu katika miji ya Afrika ya Kusini.
Akiwa bado katika fikra nzito, mlango wa ofisi yake ulisukumwa, na mwanadada mwenye mwili wa kati, sio mrefu sio mfupi aliingia akiwa katika mavazi ya kijeshi, aliposimama mbele ya mwenyeji wake, huku wakitenganisha na ile meza kubwa, aliiachua kofia yake mabegani na kuivaa kichwani pake kisha akasimama kiukakamavu.
Dumisan akasimama akionekana wazi amefura kwa hasira na kisasi.
“Debra, sina haja ya kupoteza muda, nimekuteua wewe kwa kuwa najua wasifu wako jeshini, unapaswa kuondoka usiku huu na ndege ya Uingereza, uende Canada pale kuna mtu unatakiwa ukaitoe roho yake kisha urudi mara moja. Nataka ukamuue na si vinginevyo, nategemea majibu mazuri kutoka kwako, asante.” Dumisan akaketi. Debra akapiga saluti na kutoka katika ofisi ile, hakutakiwa kujibu lolote kwani hiyo ni amri alichotakiwa kufanya ni kutekeleza aliloambiwa tu basi.


2
MIEZI MIWILI ILIYOPITA
ILIKUWA HALI YA SINTOFAHAMU katika machimbo ya dhahabu huko Mashariki mwa Johanesburg, Afrika ya kusini. Katika moja ya mashimo makubwa ya tajiri maarufu, Khumalo, wafanyakazi takribani kumi na tano waliokuwa wakifanya kazi kwa ukaribu sana na mtu huyo aliyeuawa miaka kadhaa nyuma nao waliuawa na maiti zao kukutwa ndani ya mashimo hayo.
Machimbo ya dhahabu ya The Great Khumalo yalifungwa kwa muda ili kupisha uchunguzi wa mauaji hayo yaliyotokea ndani ya siku moja lakini haikujulikana ni nani hasa aliyeyatekeleza hayo.


ITAENDELEA !



wife atumia akaunti feki ya fb na kumfanya mme amtajie idadi na majina ya mabinti wote aliochepuka nao


Leo asubuhi nimeingia kazini mapema sana kuliko kawaida yangu baada ya kugombana na wife home.

Nilipofika nikatulia kwenye computer na kuwa busy na mitandao ya kijamii kujipa nafasi ya kusahau maugomvi.

Ile kufungua facebook tu nikakutana na friend request ya binti mmoja mtamu sana mwenye pic za kuvutia na kuanza kuchati naye.

Kwa kweli binti yule anajua sana kuchati na huwezi amini mpaka kufikia mida ya saa nne nilikuwa sijafanya kazi yoyote pale ofisini kwa utamu wa text zake.

Tukazidi kufahamishana na yeye akadai ana mme anaye pendana naye sana na mimi nikawa namwambia nina mke ila ana longo longo sana hivyo simpendi kiviiile ni basi tu yaani.

Tukaendelea kuchati na akawa anaonekana anasogea sogea kwangu na akaniuliza niwe muwazi kumwambia kama tangu nuanze ndoa kuna wanawake nimewahi tembea nao ndio anikubali kuwa nae kwani anaogopa magonjwa, nikampa idadi yake bila kusita na hata alivyoomba majina yao nikampa yale ya mwanzo tu.

Akanipenda sana kwa kuwa muwazi na kuniambia atafikiria kwa kuwa mimi ni mkweli sana.

Baadae nikamwomba afanye tuonane akanipa namba ya voda nami baada ya kufurahi nikamwambia ningempigia mchana huu.

Mida hii nimeipiga ile namba na sauti ni ya mke wangu na nilipojaribu kutumia njia ya kujifanya natuma fedha kwa mpesa, nimeishiwa nguvu kuona ni jina la mke wangu na hakuwa na laini ya voda kabla.

Jamani nimetoka kazini nipo hapa bar nakunywa na sijui leo nyumbani itakuwaje...:..

Naombeni ushauri vijana wenzangu kwani hapa kati nimekuwa mkorofi sana kwa mke wangu na akasema kuna siku atanibamba tuu.....

Naumia zaidi ile kutoa list ya mabinti niliotembea nao wote....

Nahitaji ushauriwa akili imesizi....

Baada ya kila dhoruba kali nuru huonekana

Nilikulia katika kijiji kimoja kusini mwa Tanzania na mama yangu yeye alikuwa mwalimu wa chekechea wa kujitolea katika shule hiyo ya watoto wadogo pale kijijini.
Mtu niliyeambiwa kuwa ni baba yangu alikuwa ni mlevi wa kupindukia pale kijijini na fundi selemara aliyemiliki sehemu ndogo ya kufanyia kazi kama ofisi yake ya kujipatia kipato ambacho alikitumia kwa kununulia pombe na kubaki katika maisha duni sana.
Baba huyu alikuwa mkali akimpiga mama na mimi kila siku na sitaki kukumbuka jinsi kila siku mama alivyonikumbatia na tukasaidiana kulia tukimwomba Mungu ambadilishe baba huyu ambaye pia alikuwa na wake wengine wawili na kunifanya kutambua kuwa mama yangu alikuwa ni mke wa nje wa baba.
Nililia na kumwomba Mungu ayabadilishe maisha yetu kila siku na nilifurahi sana kila siku jumapili nilipomwona mama akiimba kwa furaha katika kwanya pale kanisani na kunifanya kufurahi kila ifikapo jumapili ambapo ndio nilimshuhudia mama yangu akiwa na furaha ya ajabu na kuyasahau magumu ya nyumbani na kumshukuru Mungu.
Mama alinifanya kuona kuwa kanisani na kumwomba Mungu kipindi hicho ndio ilikuwa faraja yetu kubwa na alinisisitiza kuwa nitafanikiwa na kuwa mtu mkubwa katika maisha haya na kunifundisha kusamehe.
Somo la kusamehe lilinikaa sawa sawa na kumsamehe baba yangu kwa kila alichomfanyia mama na kusababisha maisha yetu kuwa magumu hasa baada ya kumpa mama ujauzito uliomfanya aishie kidato cha tatu na kusitisha masomo ili anikuze mimi huku familia yake ikimtenga na kuanza maisha yake.
Nilimsamehe na miezi michache baadae alifariki baada ya kupata tatizo la mapafu yaliyoharibiwa na uvutaji wa sigara na kufa kwa kukosa fedha za kumfanya atibiwe katika hospitali kubwa pamoja na jitihada za kuuza ardhi yetu na baadae maisha yetu yakazidi kuwa magumu.
Nakumbuka kila siku asubuhi nikiwa naenda shuleni jinsi mama alivyonipa nguvu na maneno ya ujasiri yenye uthubutu kuwa nitakuja kufanikiwa na kuitunza familia yetu na pia nakumbuka jirani yetu mama fred ambavyo yeye naye aliwahi kunipa zawadi ya viatu pamoja na ufukara wake ambao ulilingana na ule wetu na kuniambia kila nivaapo vinifanye niamini nitafanikiwa kuyakanyaga maumivu yote na kusonga mbele kufuata sauti ya ushindi na kuja kuwa mtu mwenye mafanikio.
Kila nilipovivaa viatu vile nilihisi kuwa yale maumivu ya mama na maumivu ya ufukara wetu wa kutisha pale kijijini kuna siku ningekuja kuyakanyanga na kumvalisha mama viatu vya furaha na kuja kumfanya maisha yake yote yawe ya furaha na tabasamu kama awapo kwenye kwaya yake siku za jumapili, kwa kweli nilikuwa nikisikia sauti za mafanikio zikiniambia nijitume..
Siku moja tukiwa shule ya sekondari tumekaa kando ya barabara tunacheza na kufurahi mbele yetu alikuja baba mmoja akiwa kashika begi mkononi na mkono mwingine kashika fimbo na miwani jambo lilinifanya nihisi kuwa mzee yule alikuwa ni kipofu.
Akaomba kwa sauti "wanangu naomba mnisaidie kuvuka barabara!"
Hakuna aliyemsikiliza zaidi ya watu kumcheka pale na kuendelea kucheza, mimi nikaamua kusimama na kwenda kumsaidia na nilipofika pale nikamwambia
"naweza kukusaidia?"
Akajibu "ndio"
Nikamwambia naomba nishike bega langu la kulia na nikamvusha na kumbe alikuwa anakuja pale shuleni kwetu na baada ya kuniuliza ni sehemu ipi anaweza kukaa na kumwonesha basi akalifungua lile begi lake na kutoa pipi na biskuti na kuzitandaza juu ya kitambaa chake na kuanza kuziuza na mimi akiniambia,
"mwanangu Mungu atakubariki sana na nitatamani siku nifungue macho yangu kuona mafanikio yako kwani sauti yako tu inanionyesha una hekima na huruma"
Nilimwangalia kwa dakika kadhaa nikiwa pembeni huku akiuza pipi, chocolate na biskuti zake kisha machozi yakanitoka na kushindwa kuyahimili na kuondoka zangu kurejea kwa wenzangu.
Tuliendelea kuwa marafiki na kila siku muda kama ule nilimsaidia kumvusha pale baada ya kuniulizia dan niko wapi, kusikia sauti yangu na mara nyingine alinikuta namsubiri nimvushe pale.
Kuna siku nilifika pale kituoni na kugundua hajafika nikakaa pale kwa dakika kadhaa nikiwa nimejificha sehemu na alipofika nikaaendelea kukaa pale na hakumwita mtu mpaka watu wakaondoka nami nikamsogelea na kukaaa kimya kwa dakika bila kuongea kitu na baada ya watu wachache kupita akaniita "DAN"
Nikaitika nakusema "NAAM", umejuaje kuwa nitakuja na kwanini hujamwomba mtu yoyote akusaidie kuvuka?
Akaniambia " Niliamini kuwa utakuja kwa kuwa wewe ni rafiki na kuna sauti iliniambia lazima utakuja nami nikakusubiri"
Nilishangaa wala sikuongea kitu chochote na kumsaidia kuvuka kisha tukaenda na nikamwacha akiuza nami nikaingia darasani.
Alikuwa rafiki kwani kuna nyakati nilimsaidia hasa pale wanafunzi walipokuwa wakimlipa shilingi mia tano badala ya alfu moja wanunuapo vitu na kunifanya mimi kuwa na maadui wengi pale shuleni zaidi ya marafiki na ikafika kipindi nahitimu pale aliniita na kunipa yeye aliyoiita zawadi ya kuwa
"mwanangu utafanikiwa kama nawe utaisikia sauti ya mafanikio kama mimi nilivyokuwa na imani kuwa kila mara ungenisaidia na ukawa hivyo"
Nilimjibu amen na kuondoka ingawa nilihisi nampoteza rafiki ambaye alinijenga sana.
Miaka miachache baadae kwa jitihada za mama yangu nilifanikiwa kuhitimu chuo kikuu na kupata kazi katika kampuni moja ya kutengeneza vitabu na kipata mwanya wa ufadhili na nikaandika historia ya maisha yangu niliyoiita "Maisha ya Salome na Mwanae Dan" kitabu ambacho kikauzika sana na kunifanya mimi kuweza kumtunza mama.
Nilirudi mpaka ile shule na kumulizia rafiki yangu yule ambaye alikuwa kipofu na kwa bahati mbaya niliambiwa alifariki kwa ajali ya gari baada ya kujitahidi kuvuka barabra kwa kukosa msaada na kugongwa na gari. Nililia sana na kuishia kubaki na yale aliyoniambia na mpaka sasa mimi na mama tuna shirika la kusaidia wajane na walemavu wa macho liitwale "fuata sauti yako foundaton"
Kwa nini nimetaka kuandika kisa hiki cha kufikirika?
Kila mtu ana historia ya mapito magumu katika maisha yake na pengine hata sasa una wakati mgumu sana na hujui nini cha kufanya.
Hebu fikiri wakati mama yangu ananyanyasika na kufanya kazi kwa taabu ili kunipa maisha mimi aligundua kuwa ana tone la furaha na kulitumia ipasavyo hasa zile nyakati za kwenda kanisani na kuimba na wenzake na kusahau maumivu ya muda na kujipanga kuona atayakabili vipi.
Mama Fred yeye hakuwa na fedha sana na alikuwa ni maskini kama sisi lakini vile viatu ambavyo alinunua na kunipa pamoja na yale maneno mazuri vilinihamasisha kufanya vizuri. Je wewe umekuwa msaada kwa wenzako hata kama na wewe unaona huna kitu? Umewapa maneno ya faraja au umekuwa ukifurahia magumu yao?
Yule kipofu aliomba msaada na wengi wakawa wakimwangalia na kumcheka je ni mara ngapi na wewe umeomba msaada na watu na kuchukulia ni utani na kuja kujutia baada ya kugundua kuna mtu ulishindwa kumsaidia katika nyakati aliyohitaji msada wako?
Ni mara ngapi umewasamehe wale waliokufanyia mabaya na hata kuwafanyia mabaya wale uwapendao mbele yako kama nilivyomshuhudia baba akimnyanyasa mama na mwisho wa siku nikamsamehe ingawa alifariki baadae hata kabla ya kuja kula mafaniko ya mwanae?
Ni mara ngapi umesaidiwa na kuwa na shukrani hata ya maneno mazuri kama vile yule kipofu alivyomfanyia dan na hata kujenga imani ya kuwa huyo mtu aliyekusaidia unahitaji kumwamini na kuuthamini mchango wake?
Ni mara ngapi umerudi kuwashukuru wale waliokusaidia nyakati za shida au ulivyowahitaji wakusaidia na wakakusaidia?
Katika kufanikiwa kwako au katika jitihada za mafanikio yako umefuata sauti liyomo ndani yako kuwa utafanikiwa na ukaishi kwa ndoto zako huku ukijituma na kujikabidhi kwa mungu ?
Baada ya kila dhoruba kali nuru huonekana ....... nakutakia wiki hii kuwa ya mafanikio kwako......AMEN-------------> share ------------>

Shkamoo sudani, uholanzi na usb sooooory usa


LANGO LA MOTONI CHAPTER 13

SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU

LANGO LA MOTONI 

CHAPTER 13

Ilipoishia

Alipiga simu ya samira kwa muda ingawa haikupokelewa alipoiangalia saa yake akagundua kuwa ni saa nane kasoro za usiku. akaishiwa nguvu na kuingia hotel kulipa bili yake na kisha kurudi kwenye gari na muda mfupi baadae akawa barabarani.

Wakati anatokeza barabara kuu kuna magari mawili yalikuja kwa kasi moja likitokea nyuma na jingine mbele na kumzingira ben na..........................


Endelea

Wakati anatokeza barabara kuu kuna magari mawili yalikuja kwa kasi moja likitokea nyuma na jingine mbele na kumzingira ben na watu wale wakalivamia gari la lake na kumtoa nje kwa kurupushani  huku mmoja wao akiutumia mwanya huo kumchoma sindano moja iliyomfanya ben alegee taratibu na kisha kutupwa kwenye moja kati ya magari yale siti ya nyuma na safari ikaanza huku ben akiwa sasa kalala na hajitambui.

Watu wale walikuwa wamevaa mask ambazo hazikuweza kuruhusu kuzifahamu sauti wala sura zao  kutokana na aina ya mask hizo, hivyo ule muda wa purukushani ingekuwa ni ngumu kwa ben kuwatambua .

Mgari yale yalitembea kwa muda wa takribani dakika kama 30 na baadae yaliingia katika jumba moja pembeni ya mji lililoonekana kuwa ni kubwa na pengine mmiliki wake kuwa na kipato cha kutosha. Walimshusha ben aliyekuwa kalala kutokana na ile sindano na kisha watu wale wakamfungia kwenye chumba kimoja na kumwacha.

" Mkuu tumempata mtu uliyetutuma tukamchukue na tumeshamfungia kwenye chumba ulichotuamuru, kuna jingine la kufanya kwa sasa?" alihoji mmoja wa watu wale ambaye kutokana na amri zake kwa wenzake ni dhahiri kuwa alikuwa ndio kiongozi

" Hapana nafikiri mwacheni kama nusu saa kwani kuna kitu nakifanya kisha nitakuja nyie mwongezeni ile sindano ili asizinduke sasa" " Sawa mkuu" alimalizia kijana huyo na kisha kwenda kutekeleza amri.

Saa tisa kasoro za usiku samira alishtuka kutoka usingizini na akawa anajisikia kiu ya maji hivyo akanyanyuka na kwenda jikoni akachukue maji. Baada ya kunywa maji akaona sio mbaya aangalie simu, alishtuka kuona kuna missed calls pamoja na sms kutoka kwa Ben.

" Nimevumilia kwa muda lakini najikuta nashindwa kuendelea kujifanya sina hisia nawe, naomba kama ikiwa ni kwa mapenzi yako pia bila kuathiri uhusiano wetu basi tufungue ukurasa mpya"

Sms hii ilimfanya samira apoteze usingizi wake wote na kujitupa kwenye sofa pale sebuleni na kuanza kuitafakari,  " maskini!!!! kumbe muda wote huu ben ana hisia na mimi na akaogopa kuniambia. Au ndio maana kamsaidia aunt amina? Na je nikimkataa inamaana ndio utakuwa mwisho wa msaada wake kwetu au hata kututoa kwenye nyumba?

Je nimwambie aunt amina au nitulie, na je nikimwambia atanichukuliaje? Hapana liwalo na liwe kwa sasa mapenzi hapana, ila nafikiri ni bora nimpigie na kujaribu kumwambia kuwa kutokana na yote yaliyonisibu kwa sasa sina fikra na mambo hayo, ili anipe muda kisha nikihitimu shule tulijadili, je ataelewa lakini?

Hapana nafikiri ngoja nimpigie simu sasa, mmmh!! ila nahisi kama ni usiku sana, nitampigia asubuhi, lakini kwa mtu mwenye kujitoa kama huyu katika maisha yetu, si na mimi natakiwa kumfikiria nae afurahi na kuona pia kuna watu wanamjali?"Samira alijiuliza na kujijibu bila ya jibu sahihi na hatimaye usingizi ukamchukua pale kwenye sofa na kulala usingizi mzito.

Saa tisa na nusu ikielekea saa kumi kasoro za alfajiri mlango wa chumba alichowekwa ben ulifunguliwa na boss wa vijana wale akaanza kuwakaripia wale vijana wake,  " jamani mmefanya nini tena? huyu mliyemleta ni nani, mbona simfahamu? Huyu siye angalieni vyema ile picha ya gari niliyowapa"

" samahani boss basi magari yanafanana sana tukajua ndio hili kwani lilikuwa sehemu uliyotuambia tukatege na ni kama lile" 

" haya sasa haraka mfungueni na nendeni mkarudishe pale mlikomchukua na hakikisheni hakuna anayewafuatilia, na mara nyingine kuweni makini makosa kama haya hayahitajiki na ni hatari" 

"Sawa boss" Aliongea kijana huyo kwa uoga huku akimchukua ben ambaye bado alikuwa hajaamka kutokana na sindano ile.

Muda mfupi baadae vijana wale walifika pale njia panda walikomchukua ben na kumwingiza kwenye gari lake na kisha wao wakatokomea kusikojulikana wakimwacha ben akiwa pale ndani ya gari lake na wakati huo  ilikuwa inakaribia kumi na moja kasoro za alfajiri.


Saa moja kasoro za asubuhi ben ali............................................................



KIsa hiki kitaendelea KESHO na kwa wale wanaotaka kukisoma kupitia Telegram wasiliana nasi kwa Telegram  namba 0713317171 na pia waweza kuwa mdhamini


KUmbuka ku-comment, share na kutag marafiki

LANGO LA MOTONI CHAPTER 12

SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU

LANGO LA MOTONI 

CHAPTER 12

Ilipoishia

Aunt amina aliwasili pale baada ya ndege yake kushuka samira alipong'aza aunt amina alirukwa na furaha na kujikuta akimkumbatia na kulia kwa furaha na hakuamini kama kweli alikuwa kapona na anaona tena.Walingia garini na ben akawachukua moja kwa moja mpaka moshono na kwenda kupaki mtaa wa ichenga na kisha wakashuka garini.

Aunt amina alisita kungia ndani na akajikuta akitokwa na machozi na.................


Endelea

Aunt amina alisita kungia ndani na akajikuta akitokwa na machozi na ghafla akawa kama mtu aliyepandwa na kichaa na kuanza kupiga kelele huku akikimbia kuifuata barabara kuu ili arudi mjini.

Iliwachukua zaidi ya saa moja na nusu Ben na Samira kuweza kumtuliza na kumwambia ukweli aunt amina juu ya mmewe kuuawa katika tukio lile, nyumba kuchomwa moto na kila njia aliyoipitia samira mpaka kukutana na ben aliyemsaidia na kuhakikisha kuwa aunt anatibiwa na kurudi salama.

Samira pia akamweleza aunt amina kuwa hajawahi kuona mtu mwenye moyo wa kusaidia kama wa ben  na imemshangaza na kuona kumbe kuna binadamu bado wa chembe ya utu hata kama dunia na watu wake wanazidi kuwa vichaa na wanyama wasio wajali wenzao na mapito yao.

" Asante sana mwanangu Ben, Mungu akupe baraka tele na pia awe mlinzi wako katika kila njia ya mafanikio mbele yako. Mimi nitaomba jambo moja tuu"


"Asante, sema tu aunt amina"

"Nitaomba kesho kwenda kuliona kaburi la mme wangu na kuwashukuru majirani na kisha nije kuishi hapa kwa muda kama ulivyosema" Aliongea aunt amina kwa sauti ya unyonge na maumivu.

" usiseme kwa muda aunt amina, mimi naomba ukae tuu na pia nitajitahidi kujaribu kuangalia nini nikupe ukifanye ili uweze pata kipato na Samira arudi shule aendelee maana mwaka huu ni kama hajasoma kutokana ma shida hizi

" asante sana kaka ben, mungu akubariki" alidakia samira na kumfuta ben na kumnyanyua aunt amina ambaye alimkumbatia ben kama ishara kuonesha kuukubali na kuuthamini mchango wake na kisha akamalizia kwa kusema " mwanangu ni wanaume wachache sana wanaoweza kumsaidia mtu bila ya kutarajia malipo, nakushurukuru kwa kunifanya nione tena"

Ben aliwaacha na kuliwasha gari lake na kisha akaondoka kwenda mjini ambako aliishia kwenye hotel moja na kujipatia chakula cha usiku huku akiwa na fikra nyingi juu ya aunt amina ambaye kiukweli hata kama ungekuwa ni wewe msomaji ungetokwa na machozi kwa jinsi alivyoumia kuona mmewe kaondoka katika tukio la kikatili.

Usiku ule aunt amina aliongea mengi sana na samira na walijadili mengi na kila halipoongea aliishia kulia kwani aliamini kuwa furaha yake na faraja pekee imetoweka, " hebu fikiria unakaa na mwanaume kwa miaka nenda rudi hujabahatika kupata mtoto lakini bado anakupenda kwa dhati na hana hata dalili za kutoka nje ya ndoa au kukusaliti, na hata ndugu wanapojaribu kuwagombanisha bado yuko upande wako, Kweli nimeamini kuwa watu wazuri huwa hawadumu" 

Maneno hayo aliyatoa aunt amina bila hata kutarajia na kumfanya samira agundue jambo ambalo alikuwa halijui kwa undani.Samira na aunt amina walikuwa na jambo moja ambalo kwa pamoja walibarikiwa nalo lilikuwa ni kuimba nyimbo kila walipokuwa katika wakati mgumu, muda huu walijikuta wakianza kuimba wimbo wao waupendao ambao taratibu uliwateka na usingizi ukatumia mwanya huo kuwabeba.


Ben alikaa pale hotelini na kuendelea kuagiza vinywaji huku sasa akijikuta kuanza kumfikiria samira kwa mtazamo tofauti na kila alipoongeza funda jipya la kinywaji chake akajikuta akipata ujasiri wa kumpigia samira na kumwambia neno ingawa ujasiri huo kuna wakati ulitoweka na kuamua kuacha.

Alikaa pale kwa muda na akaitoa simu yake na kuiangalia kwa umakini picha ya samira na  kila alipotaka kumwambia kitu samira alishindwa akaamua kuandika sms hii, " Nimevumilia kwa muda lakini najikuta nashindwa kuendelea kujifanya sina hisia nawe, naomba kama ikiwa ni kwa mapenzi yako pia bila kuathiri uhusiano wetu basi tufungue ukurasa mpya"

Alishikilia kitufe cha kutumia ujumbe huu kwa muda akitafakari kama atume au asitume. Akiwa katika hali hiyo kuna rafiki yake mmoja alifika pale na kama ilivyo kwa taratibu zao za kusalimiana alimgonga bega ben kwa nyuma na kumsalimia jambo lililomshtua ben kwani alikuwa kwenye dimbwi la mawazo.

Alipokuja kupata fahamu akagundua kumbe  ile meseji ilijipekeka alipogongwa bega na yule rafiki, ben alijikuta akitamka kwa sauti kubwa NOOO!!!! NOOO!!! na kutoka nje ili ampigie samira kumwambie sio ujumbe wake.


Alipiga simu ya samira kwa muda ingawa haikupokelewa alipoiangalia saa yake akagundua kuwa ni saa nane kasoro za usiku. akaishiwa nguvu na kuingia hotel kulipa bili yake na kisha kurudi kwenye gari na muda mfupi baadae akawa barabarani.


Wakati anatokeza barabara kuu kuna magari mawili yalikuja kwa kasi moja likitokea nyuma na jingine mbele na kumzingira ben na..........................


KIsa hiki kitaendelea KESHO na kwa wale wanaotaka kukisoma kupitia Telegram wasiliana nasi kwa Telegram  namba 0713317171 na pia waweza kuwa mdhamini


KUmbuka ku-comment, share na kutag marafiki

LANGO LA MOTONI CHAPTER 11




SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU

LANGO LA MOTONI 

CHAPTER 11

Ilipoishia


Samira alimshukuru sana  na wakaachana na ben kwa miadi ya kuwa aende mpaka hostel akaweke mizigo yake sawa ili dereva aende kumchukua na kumpeleka hoteli mpya.


Samira alifika mpaka pale hostel na kabla ya kuufungua mlango wake akaona aende pale alikojificha usiku kwani kumbukumbu ilimrudia na kukumbuka kila kilichofanyika pale jana yake usiku na wale watu waliokuwa dirishani kwake.

Alipolikaribia dirisha lake kwa chini samira aliona.......................


Endelea


Alipolikaribia dirisha lake kwa chini samira aliona kuna pakiti ya sigara iliyotumika na kilichimfanya asimame na kuokota ilikuwa ni business card moja iliyokuwa na jina la  h zombo ambaye alionesha kuwa ni mmiliki wa kampuni moja ya usindikaji vyakula na matunda.

Kilichomshutua zaidi ni nyuma ya  business card hiyo kuwa na jina lake na la aunt amina. Moyo ulimruka na ghafla jasho la uoga likaanza kumtoka bila hta ya kutarajia akajikuta akitamka " Mungu wangu, ina maana watu hawa bado wananitafuta mimi na aunt amina, na je huyu mzee kombo ni nani?" 

Hata kabla ya kujipa jibu akasikia muungurumo wa gari likija alipochungulia akaona ni dereva aliyetumwa na Ben, akaificha ile business card na kisha kaingia kuchukua mizigo na kuondoka kuelekea hoteli.

Hoteli hiyo ilikuwa nzuri na aliufurahia ulinzi wa eneo hilo na kwa hakika akijesemesha " Asante Mungu naamini kwa muda hapa nitakuwa salama na naomba umrejeshe salama aunt amina na hakika tuweke mikononi mwako ili tuwe salama"

Kwa upande mwingine mapambano huko mtaani yalipamba moto sana kwani samira alipotea kutoka mikononi mwa vijana wa mzee zombo. Walijaribu kufuatilia kila kona lakini hawakupata dalili yoyote juu ya wapi aliko samira ikabidi wampigie simu bosi wao.

" Pumbavu sana nyie yaani mnakuwa kwama landline crocodilelicious, yaani katoto kadogo kanwashinda... Sasa nasema nitamtuma mtu aje awalete hapa muone moto au mpaka jioni mnipe jibu zuri"

Kijana aliyekuwa anapiga simu akajikuta akishindwa kuvumilia na kucheka na kumuuliza, "mzee kwani hiyo landline crocodilelicious ni nini?"

" acha ujinga, hilo swali muulize baba yako ambaye hakukupeleka high education institute of centre, hapo nimekutukana sana kwa kiingereza, haya sina muda wa kuongea na mapuuzi sasa nasema rudini kazini"

Kijana yule aliishiwa nguvu na kujikuta akikaa chini na kucheka hasa akikumbuka kiingereza cha mzee zombo ambaye hakuwa na historia ya kuhudhuria shule kama alivyokuwa akijitamba na maneno ya kiingereza kisichoeleweka na muda mfupi baadae waliondoka eneo hilo kuendelea kumsaka samira.


Siku hiyo samira aliwahi kuamka na tayari alikuwa ameshajiandaa akimsubiri Ben ili waende airport kumpokea aunt amina ambaye akikuwa akirudi siku hiyo. Ben alifika pale hotelini akiwa analalamika njaa hivyo akaona ni boda aagize chakula kwa kuwa muda ulikuwa bado unaruhusu hivyo wakajumuika pamoja na samira.

Muda mfupi baadae ben na samira walikuwa sehemu ya kupokelea wageni pale airport. Samira alikuwa kavaa sketi yake fupi na top moja iliyomfanya aonekane vizuri hasa chuchu zake zilizokuwa zimechomoza pale kifuani mithili ya vichuguu uchungu viwili huku sketi ikiuacha mguu wake uliojazia nao upate kuonekana kiurahisi.

Lakini hips, nywele ndefu za kimanga na jicho la samira ndio vitu vilivyowafanya baadhi ya wanaume wakware wenye nia binafsi na samira wamkodolee macho huku wengine nao wakimchukia ben kwa kuwa karibu na binti huyu ingawa nae ben mara moja au tatu alidakwa na jicho la samira akiwa anamkodolea macho na akapotezea kwa kumsifia au kumfariji juu ya aunt amina.

Aunt amina aliwasili pale baada ya ndege yake kushuka samira alipong'aza aunt amina alirukwa na furaha na kujikuta akimkumbatia na kulia kwa furaha na hakuamini kama kweli alikuwa kapona na anaona tena.Walingia garini na ben akawachukua moja kwa moja mpaka moshono na kwenda kupaki mtaa wa ichenga na kisha wakashuka garini.

Aunt amina alisita kungia ndani na akajikuta akitokwa na machozi na .................


KIsa hiki kitaendelea KESHO na kwa wale wanaotaka kukisoma kupitia Telegram wasiliana nasi kwa Telegram  namba 0713317171 na pia waweza kuwa mdhamini



KUmbuka ku-comment, share na kutag marafiki


LANGO LA MOTONI CHAPTER 10



SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU

LANGO LA MOTONI 

Mtunzi: Fred Kihwele 0713317171


CHAPTER 10

Ilipoishia



"Ok, basi mie nakuacha nafikiri zile hela bado unazo hivyo hakuna shida upande wako, nitakucheki kwa simu mida mida" Alihitimisha Ben na kisha wakaachana na samira yeye akaingia hostel.

Wakati anakaribia mlango wa hostel samira kuna kitu kilimfanya asite kuingia na kuamua kurudi nyuma na kujibana sehemu kwani muda huo giza lilikuwa limeanza kuwa la kumfanya mtu asione vyema.

Akajisogeza hatua kama nne na ku...................

Endelea

Akajisogeza hatua kama nne na kukijibanja pembeni ya ukuta wa hostel hiyo, sehemu ambapo hakuna mtu ambaye angefanikiwa kumwona kwa urahisi ingawa yeye aliweza kuona na kusikia vyema kila kilichoendelea.

" Oya huyu mtoto inaonekana hayupo na kama haitoshi muda huu bado kweupe kweupe na kuna wapangaji wengine wanaweza kuja na kuharibu deal, kama vipi wewe zima simu ili boss asitupate muda huu na ikifika mida ya saa sita tuje tufanye kazi hawa ngedere wakiwa wamelala"

Alimaliza kuongea mtu mmoja ambaye kwa mbali alionesha kama alikuwa akitaka kurudi lango kuu kutokea dirishani mwa chumba cha kulala samira  alipokuwa kasimama huku mwenzie akimfuata taratibu.

Hazikupita hata sekunde kadhaa, samira alishtuka kuona akiwa kashikwa na mtu aliyembana kwa kitambaaa fulani kwenye mdomo wake na pia kilichoifunika pua yake jambo lililomfanya alishindwe kupiga kelele hata ile ya kurusha mguu na hatimaye taratibu alijikuta akiishiwa nguvu na kupoteza fahamu.

Saa tano na dakika 45 za asubuhi mlango wa chumba uligongwa na kisha dada mmoja aliingia na kukaa kitanda alichokuwa kalala samira ambaye nae ndio alikuwa akianza kurudiwa na fahamu.

" Umeamkaje dada?"

"salama kiasi kwani nipo wapi hapa na nimekujaje hapa?" Alihoji samira ambaye kwa uchovu alikuwa akijiweka sawa pale kitandani.

" Dada, hii inaitwa PLEASE REST IN PEACE GUEST HOUSE," aliongea dada huyo ingawa ilimbidi atulie kuongea baada ya samira kushtuka kulisikia jina hilo.

"Rest in peace!!!!!! yani kama ile ya R.I.P? oooh maskini  mimi!!!, MUNGU wangu kwani nini  tena?"

"samahani dada, sio rest in peace kama maana ya ile ya kumwambia marehemu hapana,hii ni maana nyingine" aliongea dada huyo huku akimsaidia kumpa tishu ya kufutia machozi samira na kisha akaendelea kuongea

" jana nilikuwa zamu ya usiku ambayo huishia asubuhi ya leo saa mbili, na wakati nikiwa mapokezi nilisikia kishindo hapo nje na nilipoenda haraka nikaona ukiwa umeanguka pale sakafuni.

Ulikuwa haujielewi na kama umelewa vile maana hukuweza kuongea wala kusema lolote. Nikakupekua na kuona mfukoni una shilingi laki 2 na simu yako, vyote nikakuwekea na kuamua kukupa chumba ili upumzike kwani nilihisi utakuwa uliwekewa madawa ya kulevya ili wakuibie na sasa ulifanikiwa kufika mpaka hapa na unahitaji msaada"

Wakati wote huo samira alikuwa kashikwa na bumbuazi iliyomfanya hata yale machozi yakauke na sasa akabaki kushangaa kwani kumbukumbu pia zilianza kumrejea na akakumbuka kuwa jana yake hakuwa na fedha nyingi hivyo bali alikuwa na shilingi elfu kumi na mbili na tena hakuwa ametembea nayo.

Mawazo yakaanza kumrudia tena na wakati huu akafikiria suala la mtu kumwekea fedha na kumpeleka katika hoteli hiyo ambayo hajawai kuisikia na haraka akamuuliza yule dada,

" Samahani dada kwani mtaa huu unaitwaje? na je ni mbali sana na stand kuu?"

" hapana ni umbali mdogo kwani unapanda daladala moja tuu au hata kwa bodaboda ni shilingi elfu tatu tuu."

" ok, asante naomba simu na hela" Samira alimwomba dada huyo na kisha akapokea fedha hizo na baada ya kumlipa akaondoka haraka na kuchukua bodaboda mpaka stand kuu.

Alipofika stand kuu akaenda moja kwa moja kwenye kibanda kimoja cha simu na kuweka zile fedha kwenye simu yake na baada ya hapo akampigia simu Ben na baada ya ben kumwambia sehemu aliyoko. Samira alichukua tena bodaboda na kumfuata.

Walionana na baada ya kumsimulia ben, ben akamhakikishia usalama na kumwambia sasa atahakikisha anamwamisha pale na kupeleka hoteli nyingine ambako atalala kwa siku mbili na siku ya tatu yake wakishampokea aunt amina basi watahama  eneo hilo na kwenda kuishi kule Moshono  ambako hakuna atakayepajua.

Na kuhusu suala la pesa ile laki mbili ben akamwambia umefanya vyema kuiweka kwenye simu ili tusubiri tuone kama kuna mtu atapatikana ili tumchukulie hatua za kisheria, maana nafikiri kuna kitu kinasukwa na hatujui ni nani maana unakutana na mambo makubwa sana dada samira.

Samira alimshukuru sana  na wakaachana na ben kwa miadi ya kuwa aende mpaka hostel akaweke mizigo yake sawa ili dereva aende kumchukua na kumpeleka hoteli mpya.


Samira alifika mpaka pale hostel na kabla ya kuufungua mlango wake akaona aende pale alikojificha usiku kwani kumbukumbu ilimrudia na kukumbuka kila kilichofanyika pale jana yake usiku na wale watu waliokuwa dirishani kwake.

Alipolikaribia dirisha lake kwa chini samira aliona.......................



KIsa hiki kitaendelea JUMATATU na kwa wale wanaotaka kukisoma kupitia whatsapp wasiliana nasi kwa whatsapp  namba 0713317171 na pia waweza kuwa mdhamini



KUmbuka ku-comment, share na kutag marafiki

LANGO LA MOTONI CHAPTER 9



SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU

LANGO LA MOTONI

Mtunzi: Fred Kihwele 0713317171 

CHAPTER 9

Ilipoishia

Mtoto huyu nikamtunza kwa mapenzi ya dhati na mpaka hivi leo ni binti mkubwa na anayesoma kidato cha tatu na jina lake anaitwa SALHA yaani wewe mwanangu. Kwa hiyo ukweli ni kwamba wewe ndio mtoto yule niliyekuwa nikimtunza pale hospitali."

Salha alipatwa mshtuko na ku....

Endelea

Salha alipatwa mshtuko na kuanza kulia kwa mfululizo kilio ambacho kilimfanya na mama yake aanze kulia ingawa yeye hakuwa akilia kwa yaliyomsibu Salha la hasha ila yeye sasa akakumbuka jinsi amilvyompoteza mmewe mtarajia asubuhi ya siku ya harusi yao.

Siku hiyo asubuhi mmewe mtarajiwa alikuwa  kwenye bodaboda  akiwahi kwenda salon kwa ajili ya maandalizi ndipo akakutana ana ajali hiyo iliyomfanya mama salha kuzirai zaidi ya siku nne akiwa mahututi na aliopoamka akapewa habari ya mimba yake ya miezi minne kutoka kwa sababu ya mshtuko.

Waliendelea kulia kwa muda mpaka pale salha aliponyanyuka na kumwendea mama yake na kumwambia, " 

"mama, tambua sijalia kwa sababu ya kuwapoteza ndugu ila nalia kwa furaha kwani pamoja na dunia kuwa na watu wa ajabu wenye matukio ya kutisha na kusikitisha ila bado kuna watu kama wewe wenye kutetea uhai wa watu... Nitakuita mama daima na utakuwa mama daima naamini hata mama na baba watafurahi kuona nikifanya hivyo katika ulimwangu wao wa roho, ila nina hamu ya kumfahamu dada"

"Utamfahamu tu mwanangu muda ukifika, ila kwa sasa hata mimi naumiza kichwa kujua yuko wapi maana ndugu zako hawajaweka bayana yuko wapi na ni wagumu sana kuingilika, ila nitajaribu kutafuta mawasiliano ya shangazi yenu mmoja mbaye yeye hakuwa akikaa sana pale wazazi wako na baadhi ya ndugu zako walipokuwa wakiishi"

"Asante sana mama, nakupenda na amini nipo kwa ajili yako" Alinyanyuka Salha na kwenda chumbani kwake ambako mawazo yalimsonga juu ya dada yake na vifo vya baba na mama na baadae usingizi ukamnyemelea na kulala.

**********
Ben na Samira walionekana wakiwa kwenye gari wakitoka hostel na baada ya kutembea umbali wa kilomita kama 25 hatimaye wakawasili kwenye mji mmoja uliofahamika kwa jina la Moshono na moja kwa moja gari likanyoosha na kwenda kusimama katika mtaa mmoja wa watu waliostaarabika uitwao Ichenga na kupaki mbele ya nyumba moja ya kifahari.

"tumefika sasa Samira" aliongea ben huku akimsaidia samira kushuka kwenye gari kisha wakaisogelea hiyo nyumba na kuingia ndani.

" Kaka Ben hii nyumba ni nzuri sana ila mbona inaonesha hakuna watu" alihoji samira huku wakiingia chumba baada ya chumba katika nyumba hiyo ambayo hata kama ilionesha kuwa imetoka kufanyiwa marekebisho lakini bado ile hali ya uzamani iliifanya nyumba hiyo kuwa bora na ya kuvutia tofauti na baadhi ya nyumba  pale mtaani.

"samira unajua ninahofia sana na usalama wa Aunt amina na wewe kwani pale nyumba yenu ilishaharibiwa na pia sina uhakika kama hiyo jumamosi  akirudi itakuwa busara kumpeleka pale asije patwa na mshtuko, hivyo mtakaa kwa muda katika hii nyumba ili nimsikie nae atakuwa na lipi la kusema"

"Sijui nikuambie nini ili uuje furaha niliyonayo hapa moyoni mwangu, lakini nina imani baba na mama kokote waliko watakuwa wanakuona na kubfurahi pia, Mungu akupe mafanikio mara mia ya sasa.. asante sana kaka" alihitimisha maneno hayo Samira na kuanza kuangua kilio cha chini chini huku wakielekea kwenye gari..

Ni wakati huu ambapo samira akaanza kurudiwa na picha ya udogo wake akiwa na mama yake kwenye gari akipelekwa shule na sehemu mbalimbali na mara mambo ya hatari yakaanza kumsakama mara baada ya baba na mama kufa katika kisa cha ajabu na hatimaye alivyokuja kuokolewa na aunt amina ambaye sasa kuja kwa samira kumekuwa kama mkosi kwa maisha ya familia hiyo.

Akiwa katika msongo huo wa mawazo alishtushwa na sauti ya Ben ikimwambia " samira, tumeshafika hostel yaani ulikuwa na mawazo sana kwenye gari kuna nini kinakusibu kwani nimekusemesha zaidi ya mara tatu unaonekana kama upo haupo vile"

"kaka nilipitiwa na furaha ya nyumba sasa najua nitapumzika salama na kuisubiri siku ya aunt kurudi, zimebaki siku tatu ila naona ni kama miaka nimemkumbuka sana na nina furaha zaidi kuwa sasa kapona"

"Ok, basi mie nakuacha nafikiri zile hela bado unazo hivyo hakuna shida upande wako, nitakucheki kwa simu mida mida" Alihitimisha Ben na kisha wakaachana na samira yeye akaingia hostel.

Wakati anakaribia mlango wa hostel samira kuna kitu kilimfanya asite kuingia na kuamua kurudi nyuma na kujibana sehemu kwani muda huo giza lilikuwa limeanza kuwa la kumfanya mtu asione vyema.

Akajisogeza hatua kama nne na ku...................

KIsa hiki kitaendelea kesho na kwa wale wanaotaka kukisoma kupitia whatsapp wasiliana nasi kwa whatsapp   namba 0713317171 na pia waweza kuwa mdhamini


KUmbuka ku-comment, share na kutag marafiki

Soma kisa cha 1 mpak cha 8 kupitia Karibu Mbeya​

HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU " Season 10

HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Season 10

Yaliyomo
Baba Pachu ni kijana aliyejaliwa kuwa na mke na watoto wawili na familia yake imekuwa ya furaha na amani kwa muda mrefu.

Pamoja na kuwa na furaha hiyo pia Baba Pachu amejaliwa kuwa na mafanikio makubwa katika kazi zake binafsi na pia ni mfanyakazi wa kampuni moja maarufu sana yautafiti wa madini.

Siku moja akiwa katika mihangaiko yake binafsi nje ya jiji la Mbeya majira ya usiku akiwa chumbani mwake mara anapokea simu ngeni kutoka kwa mtu asiyemfahamu.

Mara ya kwanza ilionekana kama ni WRONG NUMBER lakini baada ya muda ulivyozidi kwenda ikaonekana kuwa sio WRONG NUMBER tena bali ni mtu anayemfahamu fika ingawa yeye hamtambui na nia yake ikiwa haieleweki.

Simu hii ya AJABU ikanza kuipoteza furaha ya baba pachu na hatimaye furaha ya familia nzima, kazini mpaka jamii inayomzunguka kuanza kumwona kama mtu anayeanza kuchanganyikiwa.

Baba Pachu anaanza mkakati wa kutatua tatizo lake na mkakati huo unamfanya baba Pachu kujikuta anapita katika njia zenye visa vya kutisha, majaribu, vioja na heka heka nyingine nyingi zenye maumivu na kuifunza jamii.


ILIPOISHIA 
Safari hii mambo yalikuwa tofauti kabisa na nilivyodhania kwani simu iliita kwa muda kidogo halafu ikapokelewa. 
Mwee!! mwee!! mwee!! mwee!! niliachia shuzi moja kubwa kama bomu la nyuklia kwani nilisikia sauti ya yule dada akasema hivi..........................

Endelea

Mwee!! mwee!! mwee!! niliachia shuzi moja kubwa kama bomu la nyuklia kwani nikasikia sauti ya yule dada akasema hivi, "  Haya niambie sasa naona leo umeamua kunipigia kwani niliitegemea sana simu hii kutoka kwako"
Aliendelea kusema, " We mwanaume umeniudhi sana kwa tabia uliyoifanya na kama utarudia siku nyingine yaani kitu nitakachokufanyia hutokaa usahau maisha yako yote"
Muda wote huo sikujibu hata neno moja nikipumua kwa chini chini mithili ya askari aliyeko vitani na kupata ishara ya adaui kuwepo eneo hilo na sikuweza kukumbuka aliendelea kuongea maneno gani zaidi ya neno la mwisho alilosema " NAJUA KILA KITU UNACHOKIFANYA NA NITAKUFUATA POPOTE UTAKAPOENDA"
Kwa uoga nilikata simu ile na nikapata wazo la kumpigia rafiki yangu mmoja maana niliona maji yashazidi unga, na nikiendelea kuficha nikakumbuka ule msemo wa vijana usemao mficha maradhi kifo kitamuumbua hivyo nikampigia rafiki yangu aitwaye Dole Gumba Mwakibubu.
Mwakibubu ni moja kati ya marafiki zangu niliosoma nao enzi hizo nikiwa chuoni Tumaini pale iringa na nakumbuka mara baada ya kuhitimu na kupata kazi njombe na kufanya kwa miezi kadhaa alibahatika kupata ufadhili wa kwenda kusoma nje kwa mwaka mmoja.
Kwa kuwa mkewe alikuwa mjamzito wa mwezi mmoja aliamua kutafuta binti wa kazi ili asaidiane na mkewe kwa kipindi atakacho kuwa masomoni na binti yule alipatikana ingawa kwa mwonekano alionekana ni binti wa kawaida sana aliyehitmu masomo ya kidato cha nne na kukosa nafasi ya kujiendeleza.
Akiwa masomoni akaongezewa muda na kukaa mwaka mmoja na miezi kadhaa na siku anarudi mkewe alikuwa kijijini na yule binti wa kazi kabaki nyumbani.
 Mwakibubu alishikwa na mshangao kuona jinsi yule binti alivyobadilika na kuwa mtoto mzuri tena mwenye mvuto wa ajabu tofauti na alivyomwacha.
Wajua tena mtoto wa kibongo ambaye ni kuku wa kienyeji apate bahati na akae sehemu yenye rutuba anavyonawiri!!!!. Basi mwakibubu akamwomba penzi na binti akakataa kwa jinsi alivyokuwa akimheshimu dada yake ambaye ni mke wa mwakibuku ingwa hakuweza kumdhibiti mwakibubu kwani alifanikiwa kumwingilia kinguvu binti yule.
Binti akamwamabia mwakibubu akimtahadharisha kuwa angepatwa na mkasa mzito lakini yeye kwa dharau akacheka na kuendelea na mambo yake. Muda ulipozdi kwenda na mkewe yupo kijijini mwakibubu akaanza kugunduaq boxer zake zinapotea mle ndani kimiujiza na baada ya kushindwa kuvumilia akamuuliza yule binti.
Mwakibubu kidogo azimie baada ya kujibiwa na yule binti kuwa boxer hizo amezichukua na kazituma kwa babu yake huko sumbawanga kwani babu alimkataza asitembee na mtu yoyote mpaka ndoa hivyo atakayemfanya avunje ahadi hiyo lazima afanyiwe mila.
Ilichukua zaidi ya siku tisini za kutolala usingizi na kuchanganyikiwa huku akizidi kukonda bwana mwakibubu na kujikuta akimlipa fedha nyingi huyo binti ili amtumie babu yake na mwakibubu aokoke kukumbwa na janga la kimila na mwishowe mwakibubu akaja kugundua kuwa hakukuwa na mila yoyote zaidi ya binti kufungua duka kubwa la nguo mtaa wa nne kutoka kwao kwa ufupi binti alitumia fursa ya kibunifu kujipatia mtaji.
Kutokana na kisa hicho cha mwakibubu ambacho kilitufanya tumcheke sana na kumwona ni zube lakini wakati huu nikaona kuwa yawezekana visa vyetu vinaendana nimfuate ingawa mimi simwoni adui yangu na mpaka sasa sijui anataka nini na uwezo wake wa kutambua ratiba zangu anautoa wapi na kwa namna zipi?
Nilimpigia simu ili nimweleze yanayonisibu na nakumbuka tuliongea kwa muda kisha tukakubaliana tukutane ili nimweleweshe kwa undani zaidi. 
Basi tukakubaliana tukutane maeneo ya forest na kwa kuwa ni jirani na Gracious House of Cakes, tukaona ni vyema tukutane hapo na maongezi yaendelee huku tukitafuna cake na bisi kuyafanya mazungumzo yetu yanoge zaidi ingawa kwangu bado nilikuwa naona kama natazama filamu tena ya kihindi..
Mwakibubu aliwahi kufika pale na nikamkuta akiwa tayari akinisubiri na maongezi yetu yakaanza kwa mimi kumsimulia kisa kizima tangu sekeseke hili linaanza mpaka lilipogeuka na kuwa muvi ya kutisha na kuninyima usingizi.
Alishangaa sana na kunilaumu kwa kukaa kimya kwa muda wote huo na kuniomba nimpe meseji hizo ili azisome mwenyewe na kuhakikisha maana aliona ni kama filamu, eti kudume mimi natishiwa mpaka nanusurika kugongwa tako na bodaboda kisa ujumbe wa simu???? Haikumwingia akilini.
Aliichukua simu ile na alipoifungua meseji ya kwanza  alishtuka na kuniambia............................................................................................................. Je ni nini aliniambia? Na aliona nini kwenye hiyo meseji? Je tatizo litatatulika au ndio mwanzo wa safari mpya ya kutisha????
Usikose kusoma kisa hiki cha kusisimua jumatatu mida kama hii.

Unaweza kuwa mdhamini wa kisa hiki cha kusisimu na chenye funzo kubwa kwa vijana wa sasa katika masuala ya mapenzi.


Nawe waweza kuwa mdhamini wa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

share, like na comment