Showing posts with label Mafunzo. Show all posts

Baada ya kila dhoruba kali nuru huonekana

Nilikulia katika kijiji kimoja kusini mwa Tanzania na mama yangu yeye alikuwa mwalimu wa chekechea wa kujitolea katika shule hiyo ya watoto wadogo pale kijijini.
Mtu niliyeambiwa kuwa ni baba yangu alikuwa ni mlevi wa kupindukia pale kijijini na fundi selemara aliyemiliki sehemu ndogo ya kufanyia kazi kama ofisi yake ya kujipatia kipato ambacho alikitumia kwa kununulia pombe na kubaki katika maisha duni sana.
Baba huyu alikuwa mkali akimpiga mama na mimi kila siku na sitaki kukumbuka jinsi kila siku mama alivyonikumbatia na tukasaidiana kulia tukimwomba Mungu ambadilishe baba huyu ambaye pia alikuwa na wake wengine wawili na kunifanya kutambua kuwa mama yangu alikuwa ni mke wa nje wa baba.
Nililia na kumwomba Mungu ayabadilishe maisha yetu kila siku na nilifurahi sana kila siku jumapili nilipomwona mama akiimba kwa furaha katika kwanya pale kanisani na kunifanya kufurahi kila ifikapo jumapili ambapo ndio nilimshuhudia mama yangu akiwa na furaha ya ajabu na kuyasahau magumu ya nyumbani na kumshukuru Mungu.
Mama alinifanya kuona kuwa kanisani na kumwomba Mungu kipindi hicho ndio ilikuwa faraja yetu kubwa na alinisisitiza kuwa nitafanikiwa na kuwa mtu mkubwa katika maisha haya na kunifundisha kusamehe.
Somo la kusamehe lilinikaa sawa sawa na kumsamehe baba yangu kwa kila alichomfanyia mama na kusababisha maisha yetu kuwa magumu hasa baada ya kumpa mama ujauzito uliomfanya aishie kidato cha tatu na kusitisha masomo ili anikuze mimi huku familia yake ikimtenga na kuanza maisha yake.
Nilimsamehe na miezi michache baadae alifariki baada ya kupata tatizo la mapafu yaliyoharibiwa na uvutaji wa sigara na kufa kwa kukosa fedha za kumfanya atibiwe katika hospitali kubwa pamoja na jitihada za kuuza ardhi yetu na baadae maisha yetu yakazidi kuwa magumu.
Nakumbuka kila siku asubuhi nikiwa naenda shuleni jinsi mama alivyonipa nguvu na maneno ya ujasiri yenye uthubutu kuwa nitakuja kufanikiwa na kuitunza familia yetu na pia nakumbuka jirani yetu mama fred ambavyo yeye naye aliwahi kunipa zawadi ya viatu pamoja na ufukara wake ambao ulilingana na ule wetu na kuniambia kila nivaapo vinifanye niamini nitafanikiwa kuyakanyaga maumivu yote na kusonga mbele kufuata sauti ya ushindi na kuja kuwa mtu mwenye mafanikio.
Kila nilipovivaa viatu vile nilihisi kuwa yale maumivu ya mama na maumivu ya ufukara wetu wa kutisha pale kijijini kuna siku ningekuja kuyakanyanga na kumvalisha mama viatu vya furaha na kuja kumfanya maisha yake yote yawe ya furaha na tabasamu kama awapo kwenye kwaya yake siku za jumapili, kwa kweli nilikuwa nikisikia sauti za mafanikio zikiniambia nijitume..
Siku moja tukiwa shule ya sekondari tumekaa kando ya barabara tunacheza na kufurahi mbele yetu alikuja baba mmoja akiwa kashika begi mkononi na mkono mwingine kashika fimbo na miwani jambo lilinifanya nihisi kuwa mzee yule alikuwa ni kipofu.
Akaomba kwa sauti "wanangu naomba mnisaidie kuvuka barabara!"
Hakuna aliyemsikiliza zaidi ya watu kumcheka pale na kuendelea kucheza, mimi nikaamua kusimama na kwenda kumsaidia na nilipofika pale nikamwambia
"naweza kukusaidia?"
Akajibu "ndio"
Nikamwambia naomba nishike bega langu la kulia na nikamvusha na kumbe alikuwa anakuja pale shuleni kwetu na baada ya kuniuliza ni sehemu ipi anaweza kukaa na kumwonesha basi akalifungua lile begi lake na kutoa pipi na biskuti na kuzitandaza juu ya kitambaa chake na kuanza kuziuza na mimi akiniambia,
"mwanangu Mungu atakubariki sana na nitatamani siku nifungue macho yangu kuona mafanikio yako kwani sauti yako tu inanionyesha una hekima na huruma"
Nilimwangalia kwa dakika kadhaa nikiwa pembeni huku akiuza pipi, chocolate na biskuti zake kisha machozi yakanitoka na kushindwa kuyahimili na kuondoka zangu kurejea kwa wenzangu.
Tuliendelea kuwa marafiki na kila siku muda kama ule nilimsaidia kumvusha pale baada ya kuniulizia dan niko wapi, kusikia sauti yangu na mara nyingine alinikuta namsubiri nimvushe pale.
Kuna siku nilifika pale kituoni na kugundua hajafika nikakaa pale kwa dakika kadhaa nikiwa nimejificha sehemu na alipofika nikaaendelea kukaa pale na hakumwita mtu mpaka watu wakaondoka nami nikamsogelea na kukaaa kimya kwa dakika bila kuongea kitu na baada ya watu wachache kupita akaniita "DAN"
Nikaitika nakusema "NAAM", umejuaje kuwa nitakuja na kwanini hujamwomba mtu yoyote akusaidie kuvuka?
Akaniambia " Niliamini kuwa utakuja kwa kuwa wewe ni rafiki na kuna sauti iliniambia lazima utakuja nami nikakusubiri"
Nilishangaa wala sikuongea kitu chochote na kumsaidia kuvuka kisha tukaenda na nikamwacha akiuza nami nikaingia darasani.
Alikuwa rafiki kwani kuna nyakati nilimsaidia hasa pale wanafunzi walipokuwa wakimlipa shilingi mia tano badala ya alfu moja wanunuapo vitu na kunifanya mimi kuwa na maadui wengi pale shuleni zaidi ya marafiki na ikafika kipindi nahitimu pale aliniita na kunipa yeye aliyoiita zawadi ya kuwa
"mwanangu utafanikiwa kama nawe utaisikia sauti ya mafanikio kama mimi nilivyokuwa na imani kuwa kila mara ungenisaidia na ukawa hivyo"
Nilimjibu amen na kuondoka ingawa nilihisi nampoteza rafiki ambaye alinijenga sana.
Miaka miachache baadae kwa jitihada za mama yangu nilifanikiwa kuhitimu chuo kikuu na kupata kazi katika kampuni moja ya kutengeneza vitabu na kipata mwanya wa ufadhili na nikaandika historia ya maisha yangu niliyoiita "Maisha ya Salome na Mwanae Dan" kitabu ambacho kikauzika sana na kunifanya mimi kuweza kumtunza mama.
Nilirudi mpaka ile shule na kumulizia rafiki yangu yule ambaye alikuwa kipofu na kwa bahati mbaya niliambiwa alifariki kwa ajali ya gari baada ya kujitahidi kuvuka barabra kwa kukosa msaada na kugongwa na gari. Nililia sana na kuishia kubaki na yale aliyoniambia na mpaka sasa mimi na mama tuna shirika la kusaidia wajane na walemavu wa macho liitwale "fuata sauti yako foundaton"
Kwa nini nimetaka kuandika kisa hiki cha kufikirika?
Kila mtu ana historia ya mapito magumu katika maisha yake na pengine hata sasa una wakati mgumu sana na hujui nini cha kufanya.
Hebu fikiri wakati mama yangu ananyanyasika na kufanya kazi kwa taabu ili kunipa maisha mimi aligundua kuwa ana tone la furaha na kulitumia ipasavyo hasa zile nyakati za kwenda kanisani na kuimba na wenzake na kusahau maumivu ya muda na kujipanga kuona atayakabili vipi.
Mama Fred yeye hakuwa na fedha sana na alikuwa ni maskini kama sisi lakini vile viatu ambavyo alinunua na kunipa pamoja na yale maneno mazuri vilinihamasisha kufanya vizuri. Je wewe umekuwa msaada kwa wenzako hata kama na wewe unaona huna kitu? Umewapa maneno ya faraja au umekuwa ukifurahia magumu yao?
Yule kipofu aliomba msaada na wengi wakawa wakimwangalia na kumcheka je ni mara ngapi na wewe umeomba msaada na watu na kuchukulia ni utani na kuja kujutia baada ya kugundua kuna mtu ulishindwa kumsaidia katika nyakati aliyohitaji msada wako?
Ni mara ngapi umewasamehe wale waliokufanyia mabaya na hata kuwafanyia mabaya wale uwapendao mbele yako kama nilivyomshuhudia baba akimnyanyasa mama na mwisho wa siku nikamsamehe ingawa alifariki baadae hata kabla ya kuja kula mafaniko ya mwanae?
Ni mara ngapi umesaidiwa na kuwa na shukrani hata ya maneno mazuri kama vile yule kipofu alivyomfanyia dan na hata kujenga imani ya kuwa huyo mtu aliyekusaidia unahitaji kumwamini na kuuthamini mchango wake?
Ni mara ngapi umerudi kuwashukuru wale waliokusaidia nyakati za shida au ulivyowahitaji wakusaidia na wakakusaidia?
Katika kufanikiwa kwako au katika jitihada za mafanikio yako umefuata sauti liyomo ndani yako kuwa utafanikiwa na ukaishi kwa ndoto zako huku ukijituma na kujikabidhi kwa mungu ?
Baada ya kila dhoruba kali nuru huonekana ....... nakutakia wiki hii kuwa ya mafanikio kwako......AMEN-------------> share ------------>

MAMBO AMBAYO KIJANA WA SASA UNATAKIWA KUWA MAKINI NAYO SANA.....

MAMBO AMBAYO KIJANA WA SASA UNATAKIWA KUWA MAKINI NAYO SANA.....
1. Epuka na ujitoe kabisa kutoka katika Kundi la watu wenye mitazamo hafifu juu ya maisha yao.
2. Acha kuwa king'ang'anizi kwa wale waliokutenga katika maisha yako.
3. Kuwa mtu wa haki na upendo hata kwa watu usiowajua.
4. Kuwa mtu wa heshima na upendo kwa kila mtu.
5. Kubali kuishi na watu kwa jinsi walivyo na sio wewe utakavyo.
6. Wahamasishe wenzio kufanya mambo yenye mafanikio na furahia mafanikio yao bila unafiki.
7. Kuwa mtu wa kuaminika kwa kila ukifanyacho
.
8. Samehe watu na endelea na maisha yako bila kuwafikiria tena
.
9. Kila siku fanya kitu kidogo kizuri kwa watu wakuzungukao
.
10. Kuwa makini na mwangalifu kwa hao unaowaita marafiki
.
11. Daima kuwa mkweli
.
12. Wasialiana na kuwa karibu na watu unaowajali katika maisha
.
13. Kuwa mtu wa kitimiza ahadi zako na kuwa mkweli
.
14. Toa kitu amabo nawe unatarajia upokee
.
15. Sema unachomaanisha na maanisha unachosema
.
16. Uwe mtu wa kukubali na wengine watoe maamuzi
.
17. Ongea kidogo na kuwa makini nkatika kusikiliza
18. Usiwe mtu wa mabishano kila mara yasiyo na tija
.
19. Achana na umbea au maneno yanayoweza kuja kukunyima furaha
.
20. Uwe makini na mahusiano yako mwenyewe na mahusiano yako na MUNGU

Jihadharini na wachapaji wa kadi za harusi

*Jihadharini na wachapaji wa kadi za harusi.* 
Hakikisha unasoma maandishi yaliyochapwa kabla ya kadi kuchapwa na kusambazwa!
*Mchapaji* aliombwa aweke 1Yohana 4:18 ktk kadi ya harusi lakini mchapaji kwa makosa aliweka Yohana 4:18.
1 Yohana 4:18 panasema, *"Katika pendo hakuna hofu, lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu..."*
Lakini Yohana 4:18 tunasoma, *"Kwa maana umekuwa na waume watano , naye uliye naye sasa siye mume wako."*

Hatimaye akaolewa na yule mwanaume aliyempenda kwa mika 10...........SOMA NI NZURI



Hatimaye akaolewa na yule mwanaume aliyempenda kwa mika 10..

Mwishoni kabisa mwa tafrija fupi waliyoandaliwa na familia, mama yake alimwita pembeni na alimpa zawadi ya kitabu cha benki kilichokuwa na milioni mbili za kitanzania alizokuwa ameziweka. 

Mama akamwambia mtoto wake pekee wa kike, "Mwanangu, tafadhali chukua hiki kitabu cha benki.Kitunze kama kumbukumbu yako ya maisha ya ndoa. 

Kikitokea kitu kizuri katika maisha yenu na ambacho ukaona ni kumbukumbu basi wewe weka kiasi chochote cha fedha kwenye akaunti hii. Andika chini kitu hicho ni  nini na kiwango cha fedha ulichokiweka.

Jinsi utakavyokuwa na matukio mengi ya furaha basi kumbuka ndio hivyo hivyo na fedha zitaongezeka katika akaunti hii kwa jinsi utakavyoweka. Mimi nimekuanzia kwa kuweka fedha katika akaunti hii kutokana na tukio hili kubwa la wewe kuolewa. Matukio mengine naomba ushirikiane na mmeo kuhakikisha mnayaweka katika kumbukumbu kwa jinsi mlivyoyafurahia pamoja” 

Alipofika nyumbani akamshirikisha mmewe usiku ule alimshirikisha mmewe na wote walilifurahia jambo lile na kuona ni wazo jema sana. Kitabu chao cha benki kilionekana hivi baada ya miezi michache…

- February 7 – 200,000: Kumbukumbu yake ya kwanza ya siku ya kuzaliwa baada ya ndoa
- March 1 – 600,000: Aliongezewa msharaha kazini
- March 20 – 400,000: Shukrani ya kurudi salama kutoka mapumzikoni Kilolo
- April 15 – 4,000,000: Ana ujauzito!
- June 1 – 2,000,000: Alipandisha cheo na kuwa meneja kazini kwake

Mambo yaliendelea kuwa hivi kila tukio lilipojitokeza lenye furaha...

Ingawaje, miaka ilivyozidi kuyoyoma wakajikuta wakianza kupigana na kupigizana kelele kila kukicha.Hawakuongea tena sana kama hapo awali, kila muda walijilaumu kuoana na ule upendo wa awali ukatoweka kabisa.

Siku moja mke akampigia simu mama yake na kumwambia, "Mama, hatuwezi kuendelea na ndoa hii. Tumeamua kupeana talaka. Nashindwa kuamini nini kilinikuta nikaona na huyu mwanaume!”

Mama akamjibu, "Fanya lolote utakalo mwanangu,kama ni kweli umeshindwa kuvumilia. Ila kabla ya kufikia uamuzi huo kuna kitu naomba ukifanye kwanza.Unakumbuka kile kitabu cha benki nilichokupa wakati wa harusi yako? Tafadhali naomba ukachukue fedha zote na uzitumie kwani hutakiwi tena kuwa na kumbukumbu za maisha ya ndoa ambayo yana mwisho mbaya kama huo wako."

MKe alikubaliana na mama yake na akaenda siku ya pili yake benki wakati huu alikuwa kwenye mstari akisubiri nafasi yake ili akatoe fedha zote na kuifunga akaunti ile. Akiwa pale kwemye mstari anaisubiri zamu yake akaona achukue kile kitabu na kuangalia kumbukumbu za matukio yao ya furaha na kiasi cha pesa kilichowekwa. 

Aliangalia tena na tena kwa muda kisha zile kumbukumbu za yale matukio yote yenye furaha zikamrudia. Wakati huo macho yake yakawa yamejawa na machozi hivyo akaamua kurudi nyumbani. 

Aliporudi nyumbani akampa mmewe kile kitabu na kumwambia mmewe akazitumie zile fedha zote kabla ya wao kupeana talaka.

Siku ya pili mme akawasili benki, na tukio lililomtokea mkewe jana yake likamtokea pia mmewe. Alizidiwa pia na furaha ya matukio mazuri nay a kumbukumbu aliyoyafanya na mkewe katika kipindi cha ndoa yao na kumfanya arudi nyumbani machozi yakiwa yanamlengalenga.

Alipofika nyumbani akampa kitabu mkewe na kulikuwa kuwa fedha mpya imeingizwa katika akaunti hiyo (5,000,000) ikiwa na maneno, “Leo ndio siku ambayo nimegundua kuwa nakupenda sana mke wangu katika miaka yote tuliyokaa pamoja na jinsi ulivyonipa furaha katika maisha haya”

Wakakumbatiana na kulia kwa pamoja.KItabu chao kikarudisha katika sanduku lao maalumu na kuendelea kutunzwa huko

AMKA TOKA NDOTONI MAPENZI KAMA HAYA HAKUNA WEWE ENDELEA KUOTA TUU

Ila share

Jinsi jamaa alivyoponea kuliwa na simba kisa ubishi



Miaka mingi iliyopita mfalme mmoja alikuwa na mtumishi wake ambaye alibahatika kuwa mcha Mungu sana.

Lakini mfalme huyo alikuwa haamini kabisa kuwa kuna Mungu zaidi ya miungu yake aliyokuwa akiiabudu.

Alichukizwa sana na mtumishi huyo hasa alipokuwa akilitaja jina la Mungu kila aliposhukuru au kutaka kuomba ulinzi wa jambo fulani au baada ya jambo fulani kumtokea.


Taratibu yule mtumishi akaanza kumwelezea mfalme huyo juu ya Mungu wa kweli lakini mfalme alikuwa mkali na hata kumpa adhabu kali.

Siku moja wakawa wameenda kuwinda na walipokuwa huko waka koswakoswa kuuawa na nyati na yule mtumishi akaanza kusali akimshukuru Mungu lakini mfalme alichukizwa zaidi Na kumwambia mtumishi huyo kuwa Mungu hajahusika hapo zaidi ya wao kuwa hodari wa kukimbia na wakarudi nyumbani.

Siku nyingine wakiwa wanawinda mara simba akatokea na kumdaka mfalme na yule mtumishi akafanikiwa kumuua yule simba ingawa mfalme alijeruhiwa kidole chake kimoja cha mkononi na kuvunjika.

Mfalme akachukia zaidi kwa jinsi mtumishi huyo alivyokuwa mzembe wa kumwokoa mpaka akaliwa kidole, lakini mtumishi akasali kushukuru kuwa mfalme hakuuawa.

Waliporudi nyumbani mfalme akaamuru mtumishi huyo afungwe gerezani baada ya kusababisha uzembe uliotaka kuhatarisha maisha ya mfalme na kweli mtumishi akafungwa gerezani

Siku nyingine mfalme akaenda peke yake mwituni kuwinda na alipofika huko akakamatwa na watu amabo huwashika watu na kuwatumia kwa ajili ya sadaka za miungu yao kama sala zao.

Kwa mara ya kwanza mfalme yule akasema Mungu wangu naomba niokoe na walipofika watu wale sehemu ya kutolea sadaka mfalme aliachiwa huru kwa sababu hakuwa na viungo vyote yaani hakuwa timilifu kwani kidole mkimoja hakuwa nacho.

Mfalme aliporudi akaamuru yule mtumishi afunguliwe na alipoletewa akamwambia, " Ndugu unajua leo nilikamatwa na watu porini nikiwa nawinda na wakanipeleka mpaka kwenye sehemu ya kutolea sadaka yao na miungu yao ikanikataa kwa kuwa sikuwa na kidole kimoja yaani sikuwa kamili ni kama kilema sadaka isiyo kamili, hakika nimeamini Mungu wako ana nguvu"

"Mfalme wangu, nilikuambia kila kitu kinatokea kwa sababu na Mungu hujua yote haya, maana leo usingekuwa umenifunga tukaenda wote mimi ndio ningetolewea sadaka"

Kila kitu hutokea kwa sababu

Ujumbe wa Asubuh,i Mungu anapokuuliza swali




Ujumbe wa Asubuhi 
Mungu anapokuuliza swali
Nimemwandikia ujumbe huu rafiki yangu sana ambaye anapita katika kipindi kigumu cha mpito ya masha yake. Nikaona ni bora nikupe nawe rafiki wa hapa upate kusoma na kuitumia fursa hii.
Tunavyosoma Biblia, Huwa napenda Mungu anavyouliza maswali. Hajiulizi yeye hapana ila yeye huwa na majibu ya maswali hayo. Bali hutuuliza sisi kwa kuwa hutaka sisi tupate uelewa wa maswali na majibu yake na kuyafanyia kazi.
Alimuuliza Adamu, "Uko wapi?" Kuna kipindi huwa hatujui tuko wapi katika Maisha yetu ya kawaida hivyo twaitaji sauti ya MUngu kutukumbusha wapi tulipo na kuweza kupata nguvu za kuishi vyema..
Alimuliza Musa, "Nini umekibeba mikononi mwako?" Mara nyingi kila tunachokihitaji na baraka nyingi tayari huwa mikononi mwetu lakini bado huwa ngumu kwa sisi kutambua hilo.
Alimuuliza Malaki, "Mtu anaweza mwibia Mungu wake?" katika Maisha ya sasa imekuwa rahisi sana kwa sisi kutumia muda wetu kwa kila jambo lakini tukamsahau Mungu.
Alimuuliza Ezekiel, "Mifupa hii inaweza ishi?" Kuna wakati unaweza pita katika nyakati mbaya nakujiona kama mfu lakini Mungu anakukumbusha kuwa bado uko salama na mambo bado mazuri kwako.
Alimuuliza mtu aliyepooza, " Unataka kupona??" Mungu tayari anajua unahitaji kupata ahueni ya Maisha yako ila anasubiri kwanza wewe ulione hilo na kulitamka kwa kunywa chako
Alimuuliza Abraham, "Kuna jambo lililo gumu kwa Mungu?"
Nafikiri unavyozidi kuendelea kuishi katika dunia hii. Hata kama mambo yakawa magumu au yakutisha kiasi gani, hakuna jambo linalomshinda Mungu.
Nakuombea wewe leo rafiki zako na ngudu zako
Asubuhi Njema

MUHIMU KUJIKUMBUSHA HAYA KUHUSU MFALME DAUDI

Siku moja mfalme Daudi akiwa katika moja ya vyumba vyake kupitia dirishani alimwona mwanamke mmoja nyumba jirani akiwa anaoga.
Daudi akampenda sana na kuwatuma watumishi wake wakatafute habari zake nao waliporudi wakamwambia kuwa yule ni Bath-sheba mke wa Uria ambaye ni jemadari wa vikosi vya israel.
Mfalme Daudi akaomba binti yule apelekwe katika jumba la kifalme na akalala naye.Baada ya siku kadhaa yule binti akapeleka ujumbe kwa mfalme Daudi kuwa alikuwa na mimba yake.
Daudi akapeleka ujumbe kwa mkuu wa vikosi vilivyokuwa vitani Yoab kuwa amwambie Uria arudi mara moja. Uria akafika na baada ya kuulizwa hali ya vita mfalme Daudi akampa baadhi ya zawadi na kumruhusu aende nyumbani akijua angelala na mkewe na mimba ikawa yake.
Asubuhi akashangaa baada ya kuamka na kuambiwa Uria na watu wake hawakwenda majumbani mwao ila walilala mlangoni pake.
Mfalme akamwita Uria na kumuuliza kwa nini hukwenda kulala kwako? Naye akajibu kuwa kamwe nisingeweza kwenda kulala na kufurahi nyumbani wakati kuna watu wako vitani wakiumia.
Wakalala pale na siku ya pili Uria akaondoka kurudi vitani bila kwenda kwake na ndipo mfalme Daudi akatuma ujumbe kwa yoab kuwa uria apangwe mstari wa mbele kwenye mashambulizi makali na kisha wenzake wamwache apigwe hadi kufa.
Yoab akafanya hivyo na baada ya muda wa maombolezo ya kifo cha Uria kwisha, Daudi akamchukua Bath-sheba na kumfanya mke wake ndani ya jumba lake na akamzalia mtoto.
Mungu akamtuma Nathan na kumwambia Daudi, “Palikuwa na wanaume wawili waliokuwa katika jiji moja, mmoja alikuwa tajiri na yule mwingine alikuwa maskini.
Yule mwanamume tajiri alikuwa na kondoo na ng’ombe wengi sana; lakini yule mwanamume maskini hakuwa na chochote isipokuwa mwana-kondoo jike mmoja, aliye mdogo, ambaye alikuwa amenunua.
Naye alikuwa akimhifadhi hai, na huyo kondoo alikuwa akikua pamoja naye na wanawe, wote pamoja. Kondoo huyo alikuwa akila tonge lake, na kunywa kutoka katika kikombe chake, naye alikuwa akilala kifuani pake, na kondoo huyo akawa kama binti kwake.
Baada ya muda, mgeni akaja kwa yule mwanamume tajiri, lakini hakuchukua kutoka kati ya kondoo zake na ng’ombe zake ili kumwandalia yule msafiri aliyekuja kwake. Kwa hiyo akachukua yule mwana-kondoo jike wa yule mwanamume maskini, akamwandalia yule mtu aliyekuja kwake.”
Ndipo hasira ya Daudi ikamwakia sana yule mwanamume, naye akamwambia Nathani: “Kama Yehova anavyoishi, mtu huyo aliyefanya hivyo anastahili kufa Na kuhusu yule mwana-kondoo jike, atamlipa mara nne, kwa sababu yeye amefanya jambo hili na kwa sababu hakuwa na huruma.”
Ndipo Nathani akamwambia Daudi: “Wewe mwenyewe ndiye yule mwanamume!
Basi Daudi akamwambia Nathani: “Nimemtendea Mungu dhambi.” Kwa hiyo Nathani akamwambia Daudi: “Yehova naye ameacha dhambi yako ipite. Hutakufa. Ingawa hivyo, kwa kuwa bila shaka hukumheshimu Yehova kwa jambo hili, pia yule mwana, uliyemzaa, atakufa hakika. Kisha Nathani akaenda zake nyumbani kwake.
Na Mungu akampiga yule mtoto ambaye mke wa Uria alikuwa amemzalia Daudi, akawa mgonjwa.
Mfaleme daudi akafunga akilala chini na kumwomba Mungu amponye yule mtoto huku akilia na hata wafanyakazi wake walipotaka kumnyanyua yeye alikataa akiendelea kuomba kwa siku kadhaa.
Siku moja watumishi wake wakawa wananong'onezana jinsi ya kumwambia daudi kuwa mtoto yule amekufa. Wakasema kama wakati akiwa hai aliomboleza vile itakuaje kusikia amekufa?
Daudi akagundua wakiwa wananong'onezana akawauliza amekufa? wakajibu ndio... ndipo akanyanyuka na kwenda kuoga, akavaa mavazi mapya , akaenda nyumba ya bwana kusujudu na kisha akaomba aletewe mkate wale watumishi wakashangaa na kumuuliza,
“Ni nini maana ya jambo hili ambalo umefanya? Ulifunga na ulikuwa ukimlilia mtoto alipokuwa hai; na mara tu mtoto alipokufa ukasimama, ukaanza kula mkate.”
Daudi akajibu, “Nilifunga, nikawa nikilia mtoto alipokuwa bado hai, kwa sababu nilisema,
‘Ni nani anayejua kama Yehova huenda akanipa kibali, na hakika mtoto aishi?’ Sasa kwa kuwa amekufa, kwa nini nifunge?
Je, ninaweza kumrudisha tena? Mimi nitakwenda kwake, lakini yeye hatarudi kwangu.”
Na Daudi akaanza kumfariji Bath-sheba mke wake. Na zaidi ya hayo, akaingia kwake, akalala naye. Baada ya muda akazaa mwana, naye akaitwa jina lake Sulemani. Na Yehova akampenda mwana huyo. Basi akamtuma Nathani na kumwita jina lake Yedidia, kwa ajili ya Yehova.
Funzo
*Hakuna kitu kibaya kama tamaa ya kutaka kutamani mali isiyo yako na kuichukua kwa hila kama mfalme daudi alivyoweza mpokonya mke wa uria na kisha kuamuru Uria awekwe mstari wa mbele katika mapigano ili afe
*Mungu akiamua kukuumbua huwezi jificha hebu fikiri jinsi Daudi alivyoamua kutumia ujanja wa kumrudisha Uria ili alale na mkewe na mimba ionekane yake lakini bado ikashindikana na pia jinsi alivyomtuma Nathani na kwenda kumpa daudi mfano uliogua tukio lake
*Mungu pia huchukizwa na dhami za tamaa kama alivyoweza kumadhibu daudi na kumuua yule mtoto
*Kwa kula anguko ni muhimu sana kumrudia mungu wako kama vile daudi alivyolitambua kosa lake na kisha kuomba msamha kwa Mungu wake wa kweli
*Ni vizuri kuacha mambo yapite na kutoyakumbuka kama vile mfalme daudi baada ya mtoto kufa alivyosahau na kuanza maisha mapya na kisha kuja kupata mtoto sulemani ambaye pia Mungu alipendezwa naye na baadae alikuja kuwa mfalme mwenye hekima
Ni vyema tuutumie mfano huu wa Daudi kusahihisha maisha yetu na jinsi tunavyoishi na jamii inayotuzunguka na matendo yetu kwao.
Kama umeelewa comment Amen na kisha share

TIMING IN LIFE, HAKUNA MAJIRA YADUMUYO



Moja kati ya vitu ni muhimu kwako kuelewa ni kwamba hakuna majira yanayodumu...Leo ipo kwaajili ya kuitengeneza kesho kama jinsi ilivyokua jana kwa leo.Hivyo ni muhimu sana kuutumia wakati na fulsa ulionayo leo kwa makini na uaminifu ili ifikapo kesho uwe na akiba ya matunda ya jana.
Moja kati ya vitu vigumu kwenye maisha ni kwa mtu aliekua juu kushuka chini tena kwa ghafla,inaumiza sana. Moja kati ya vitu vinavyosababisha hili kutokea ni kuto kuyatambua majira yako kwamba hayatadumu milele......kama jinsi usiku unavyoiandaa asubuhi na asubuhi kufika haraka ndivyo ambavyo hicho kipindi cha kibali na mpenyo kitapita kwako hakika hakitakaa milele.
sasa wakati huo ukipita kuna matokeo mawili makubwa
1:Kufurahia
2:Kujuta zaidi
KUFURAHIA
Hili litakuja tu kama ulitumia muda wako vizuri na kufanya kazi kwa bidii ukitambua kwamba ule ni msimu maalum kwako kwa kuvuna na kuweka akiba si kutapanya....kwasababu kuna kesho yako inakuja ambayo hutakua na nafasi au nguvu ya kufanya tena kama sasa kwasababu wakati wako wa masika(kukubalika,ku heat,kukimbiza)utakua umekwisha watu wengi tunawaona leo bado majina yao yako vizuri lakini kimsingi wakati wake ulikwisha kinachompa heshima ni ile akiba alioweka na nguvu kubwa ya kufanya kazi alioitumia wakati bado anaushawishi kwa jamii.Hivi ndivyo vinafanya mtu kuufurahia wakati wake hata kama umepita kwasababu anayaona matunda ya kazi yake.
2:KUJUTA
Hakuna wakati mgumu sana katika maisha kama wakati wa kushuka kwa mtu aliekua juu...Hii inasababishwa na matumizi mabaya ya wakati wako(MAJIRA)Hapa ninamaanisha ni ule wakati ambapo mtu unakua na ushawishi kwa jamii husika mfano:nyimbo zako zinachezwa sana redioni,umekua mwanasiasa ambae unaushawishi mkubwa,Ni mtumishi ambae kwa wakati huo Mungu kakupa kibali kwa watu au biashara zako zinakwenda vizuri.
Watu wengi wakifika msimu huu hua wanasahau kama kuna kesho ambayo yupo mtu mwingine atachukua nafasi hiyo, na kwasababu wengi wameutumia muda huu vibaya yaani badala ya kukusanya wanatapatanya na badala ya kutumia wanafuja wengi wao hua wanakuja kustuka tayari muda ushakwisha na matokeo yake ni kujuta.kujuta hakutakusaidia lolote kwa sababu ni mara chache muda au bahati hujirudia
MUHIMU
Inawezekana kwa kutokujua umechezea muda kitu nachotaka utambue ni kwamba......
Hautakua maarufu milele
Hauta baki juu milele
Biashara yako haitakua juu milele
Hautafanya kazi ofisi hiyo milele
Kuna siku isiyo na jina utampisha mtu kwenye hiyo nafasi uliopo......Baada ya wewe kuondoka hapo ulipo je heshima yako itaendelea kuwepo? Jibu la swali gli litatokana na mchango wako ulioacha nyuma na akiba ulionayo mkononi.
Uamuzi wa kujuta au kufurahia uko mikononi mwako unapopata nafasi hiyo weka malengo tembda katika malengo tumia gharama kubwa katika kuwekeza sio matumizi...LIPA GHARAMA LEO UWE WA GHARAMA KESHO
MAJIRA HAYADUMU...!FANYA UKIWA UNAJUA LEO IPO KWAAJILI YA KUIKAMILISHA KESHO

To complete any task Use ALL your strength ; Wonderful story

Inspirational story ,short story,father son story
A young boy and his father were walking along a forest path. At some point, they came across a large tree branch on the ground in front of them.
The boy asked his father, “If I try, do you think I could move that branch?” His father replied, “I am sure you can, if you use all your strength.”
The boy tried his best to lift or push the branch, but he was not strong enough and he couldn’t move it.
He said, with disappointment, “You were wrong, dad. I can’t move it.”
“Try again,” replied his father.
Again, the boy tried hard to push the branch. He struggled but it did not move.
“Dad, I cannot do it,” said the boy.
Finally his father said, “Son, I advised you to use all your strength. You didn’t.
You didn’t ask for my help.”
~~~
Some reflections on this story…
We haven’t used all our strength until we have recognized, appreciated and galvanized the strength and support of those who love and surround us, and those who care about our purpose.
Our real strength lies not in independence, but in interdependence.
No individual person has all the strengths, all the resources and all the stamina required for the complete blossoming of their vision.
That requires the inspired collaboration of many like-hearted beings.
To ask for help and support when we need it is not a sign of weakness, it is a sign of wisdom.
It is a call for the greater strength that lives in our togetherness.
When we ask for help and we are refused, it just means we have to ask at another time, or ask in another way, or ask another person.
It helps to remember SWSWSWSW.
Some will, some won’t, so what, someone’s waiting!
When by yourself
You cannot manage
To complete any task
Use ALL your strength
Turn around and ASK!
Inspirational story , – Inspirational Quotes, Pictures and Motivational Thoughts.