Maajabu ya FaceBooK
Maajabu ya FaceBooK katika Comments...
1. Andika hivi <+(")
2.Ondoa alamaya + ,
3. Hakikisha huachi nafasi.
Utaona muujiza
MAMBO YANAYOWAKERA WAKE
1. Wababa wenye madaraka kuyapeleka madaraka nyumbani
2. Wake kuwajibika na mambo ya nyumbani kwa vile wana mishahara minono
3. Wababa kutotenga muda wa kutosha kukaa na wake zao ili kuongea yanayowahusu
4. Mume kumwachia mke kulea watoto hasa wakati wa usiku
5. Mume kutomtia moyo mke wakati wa ujauzito
6. Mume kumchanganya mama na watoto wa kike wanapokosa
7. Mume kutokuwa na maandalizi mazuri wakati wa kukutana kimwili na mkeo
8. Mume kujijari mwenyeweMume kusaidia ndugu zake bila mke wake kujua
9. Mume kubagua watoto
10. Mume kuwa na upendo na ukaribu au kucheka na binti waishio nao huku yupo mke wake
11. Mume kutomshirikisha mkewe katika huduma yake ya ili aweze kumwombeaKutoonesha shukrani wala kutokuwa na msamaha
12. Mume kutomtazama mkeo usoni mkiwa chumbani.
Japo maisha ni kusaidiana ni aibu na fedheha mwanaume ku........................
1. Japo maisha ni kusaidiana ni aibu na fedheha mwanaume kulishwa na mkewe.
2. Ni aibu na fedheha mwanaume kuhamia kwenye nyumba ya mkeo ukakala ukakoroma na taulo ukafunga..
3. Ni aibu na fedheha kuendesha gari la mkeo wakati wewe hujawahi kumiliki gari alafu unawaka wivu juu yake.
4. Ni aibu na fedheha kuishi na mwanamke ambaye wakwe zako wanajua kuwa anakuzidi uwezo.
5. Ni aibu na fedheha kumuoa mwanamke ambaye anamiliki uchumi wa familia hata watoto anasomesha yeye wewe unajivunia uume mkubwa au urefu wa kimo
6. Ni aibu na fedheha kila likizo unaenda kijijini kwa mkeo na watoto wote kisa yeye anazohela
7. Ni aibu na fedheha kukaa miaka mingi unamlaumu mkeo kuwa hazai wakati wewe huna hata mtoto wa kusingiziwa
8. Ni aibu na fedheha kumrudia mwanamke aliye kuacha yeye mwenyewe kipindi kirefu na akaamua kukurudia yeye mwenyewe tena kwa masharti kutoka kwake.
9. Ni aibu na fedheha kupewa zawadi ya kiwanja na wakwe zako siku ya send off.
10. Ni aibu na fedheha kujenga kwenye kiwanja cha mkeo wakati wewe hujawahi kumiliki kiwanja
11. Ni aibu na fedheha kulelewa mtoto wako na baba wa kambo wakati wewe upo unaishi na unajiita kidume
12. Ni aibu na fedheha kukaa kwenye nyumba yenye fenicha zoote kanunua mkeo
13. Ni aibu na fedheha kusimamia ujenzi wa nyumba ya mkeo wakati wewe huchangii hata shilingi mia
14. Ni aibu na fedheha kulea mtoto ambaye sio wa kwako kwa kisingizio cha kitanda hakizai haramu wakati mkeo anajua mtoto yule sio wa kwako.
15. Ni aibu na fedheha kulala kimapenzi na mwanamke ambaye anajua kuwa wewe unajua na unaushahidi wa michepuko yake
16. Ni aibu na fedheha kumbembeleza mwanamke anayejua kuwa anakukosea kwa makusudi
17. Ni aibu na fedheha kumaliza makanisa ukiwahadithia wachungaji tabia mbaya na usaliti wa mkeo
18. Ni aibu na fedheha mkeo kukunyima unyumba ukaenda kumshitaki kwa wazazi wake wakati unajua cha kufanya
19. Ni aibu na fedheha v mara kukopakopa kwa wakwe zako tena waliostaafu kazi..ni aibu ni aibu kubwa.
20. Ni aibuu na fedheha kwenda baa na mke baa au sehemu za starehe kila siku ikija bili unapewa wewe nawe unampa mkeo alipe kazi kukuna tu kidevu na kwenye wallet umejaza business card na viwembe vya kugushi nyaraka mitaani
Hizo ni baadhi tu ya aibu za wanaume waliowengi karne ya leo. Sambasa kwenye ma group wajijue na wamuombe Mungu awafungulie milango nao wawe wanaume katika nyumba zao
Nataka kukuambia siri moja muhimu angalia
1. Nataka kukuambia siri moja muhimu angalia namba 5.
2. Siri hiyo ni.... angalia namba 11.
3. Usipanic angalia namba 15.
4. Punguza hasira, wewe angalia namba13.
5. Angalia namba 2.
6. Usiwe na hasira kiasi hicho angalia namba 12.
7.Nilitaka kukuambia kuwa kamwe umaskini hautayakabili maisha yako na kama una muda comment AMEN!
8. Kingine nilichotaka kukuangalia . JIBU LAKE NI NAMBA 14.
9. Kuwa mpole angalia namba 4.
10. Hii ni mara ya mwisho kukutania angalia 7.
11. Naamini hutakuwa na hasira tena nikisema angalia namba 6.
12. Samahani angalia namba 8.
13. Acha hasira zako angalia namba 10.
14. Sijui nisemaje ila naomba angalia namba 3.
15. UTakuwa umefura kwa hasira angalia namba 9......
USILOLIJUA KUHUSU KUJAMBA... ...............
Kujamba kunasababishwa na kubanwa kwa hewa,ambayo inaweza kutoka mwilini kwa njia nyingi.Baadhi ni hewa tuliyoimeza wakati wa kula au kunywa.
Hewa ingine husababishwa na gesi kuingia kwenye utumbo wetu kutoka kwenye damu,na baadhi ya gesi huzalishwa na kemikali katika utumbo au bakteria.
Kwa kawaida "ushuzi" unakua na asilimia 59 ya gesi ya nitrogen, asilimia 21 ni hydrogen,asilimia 9 ni carbon dioxide,asilimia 7 methane na asilimia 4 ni oygen.
Asilimia moja tu ya "ushuzi" inaweza kuwa hydrogen sulfide na mercaptans,ambayo ndio ina sulfur ndani yake,sulfur ndo hufanya "ushuzi" utoe harufu mbaya Kujamba huambatana na sauti,hii ni kutokana na "vibration" katika njia ya haja kubwa.
Ukubwa wa mlio wa kujamba hutegemea "presha" inayosukuma gesi itoke nje na pia ugumu wa misuli ya njia ya haja kubwa.
Harufu mbaya ya ushuzi hutegemea na ulaji wa mtu,vyakula vyenye sulfur kwa wingi ndio husababisha hili.Vyakula vyenye sulfur kwa wingi ni kama maharage,kabichi,soda na mayai.
Kwa Baadhi ya Tamaduni,Kujamba Sio Ishu
Wakati tamaduni nyingi zikichukulia tendo la kujamba lifanywe kistaarabu,kuna baadhi ya tamaduni hawaoni haya kujamba hadharani,na pia hufurahia tendo hilo.
Mfano kabila la Yanomami huko America ya Kusini,kwao husalimiana kwa kujamba,na China unaweza kupata kazi ya kunusa ushuzi! Katika Roma ya zamani,Mfalme Claudius akihofia kwamba kujizuia kujamba inaweza kuwa hatari kiafya,alipitisha sheria kwamba ni ruhusa kujamba kwenye "banquets".
Mtu wa kawaida hutoa hata nusu lita ya ushuzi kwa siku.Inasemekana mtu akijamba mfululizo kwa kipindi cha miaka 6,anaweza kuzalisha nishati ya kutosha kutengeneza bomu la atomiki.
BREAKING NEWS !
Mambo 13 ya msingi usiyoyafahamu kuhusu nyangumi (WHALE)
1. Moyo wa nyangumi una kilo 600, ukubwa wake ni sawa sawa na ukubwa wa gari ndogo
2.Mtoto wa nyangumi hunywa lita 400 kila siku akiwa na umri wa miezi 7 tu?
3. Mtoto wa nyangumi ana uzito wa kilo 2700 ambayo ni sawa sawa na kifaru mkubwa size ya mwisho?
4. Uzito wa nyangumi mkubwa unakadiriwa kuwa wa tani 200 hadi 300? Mmoja JIKE alikamatwa na kupimwa alikuwa na kilo 171000kg
5. Ulimi wa nyangumi una uzito wa tani 3 ambao ni uzito zaidi ya Tembo mkubwa?
6.Mdomo wa nyangumi unaweza kuhifazi tani 90 za chakula na maji akiufumbua mpaka mwisho?
7. Chakula kikuu cha nyangumi ni dagaa kamba, ambapo nyangumi mkubwa hula dagaa kamba zaidi ya 4000000 kwa siku, ili nyangumi ashibe vizuri anakula kilo 3600kg?
9. Nyangumi anaweza kuishi mpaka kufikia miaka 80?
10.Baadhi ya mishipa ya nyangumi ni mikubwa kiasi kwamba Binadamu anaweza kuogelea ndani ya mishipa hiyo bila kugusa pembeni
11. Ukubwa wa nyangumi unaweza kulinganishwa na ndege aina ya Boeing 737
12. Urefu wa nyangumi unakadiriwa kuwa wa mita30 mpaka 50, ukimuweka ardhini urefu wake ni sawa sawa na urefu utakaojitokeza baada ya kuyapanga magari 9 ya size ya familia, Aliyekamatwa mara ya mwisho alikuwa na urefu wa mita33.
13. Nyangumi ndio mnyama mwenye sauti kubwa kuliko kitu chochote duniani. Hutoa sauti kali sana ya kipimo cha decibles188 ambayo inaweza kusikika mpaka umbali wa kilomita 848.
Ni sauti kubwa na kali kuliko sauti itoayo ndege kubwa aina ya jet inapopaa ambayo kipimo cha sauti ya jet ni decibles 120
NB: Akijamba ndani ya maji huweza kusababisha kimbunga na mvua za rasharasha katika mpwani mbalimbali
Darasa lolote lile (hasa vyuoni) lazima liwe na wanafunzi wafuatao
Darasa lolote lile (hasa vyuoni) lazima liwe na wanafunzi wafuatao:
1. Mrembo wa darasa.
2. Playboy/playgirl. Hawezi kutembea na msichana/mvulana mmoja mara mbili.
3. Group ya marafiki watatu. Kila mara wako pamoja.
4. Mtu mwenye maswali ya kuudhi/kukera.
5. Msongolist kimeo. Huyu huwa anasoma sana bt hana bahati ya kufanya vizuri. Yani msuli tembo, bt matokeo sisimizi.
6. Mlafi. Huyu huwa hakatai offer.
7. Mtoro wa kudumu. Haji darasani hata km hana sababu.
8. Mchelewaji wa kudumu. Anakuja kipindi kiko katikati au kinakaribia kuisha.
9. Miss/Mr.Misifa. kila mara ataeleza the way nyumbani kwao walivyo matajiri.
10. Less talkative bt kiwembe. Jamaa mkimya bt unakuta ametembea na karibu wasichana 15 hapo class.
11. Handsome boy ambaye hana mpango na wanawake.
12.Chips addicted. Hawa wanaweza kula chips asubuhi mchana na jioni. Jumatatu hadi jumatatu.
13. Back benchers. Hawa huwa watundu sana na ni watu wa jokes. Huwa hawajibu swali, but wanasubiri wakati wa kushangilia waongeze bezi.
14. Wambea. Hawapitwi na kitu darasani na washazoea kufeli.
15. Mchungaji/Mtumishi wa Mungu,
16. Waimbaji/Wasanii,
17.Walevi
18.Mabishoo.
19. Team popo. Hawa wawe na hela wasiwe na hela wanakesha club,
20.Mwenye aibu kusimama mbele za watu. Wakati wa Presentation anakimbilia kusimama nyuma ya wenzie,
21. Viherehere. Hawa mara nyingi hutokea kupendwa sana na waalimu.
22. Wanaosoma ili kushindana kwny GPA.
23. Kupe. Huyu boom likitoka atawaganda wenzie hadi ziishe, halafu yeye anaanza kula zake alone.
24. Wise man/woman. Huyu huwa ni mtu anayeaminika na kila mtu darasani. Hutumika sn kushauri pale mambo yanapoenda mrama. Mara nyingi huwa ni mtu mzima.
25.Fix man. Huyu atakuomba jero, akafuatilie dili la milioni kumi town, kumbe hana hela ya chai.
26. Photocopy machine. Huyu ukimuonesha majibu kwny mtihani anaweza kucopy hadi jina lako.
Je wewe ulikua namba ngapi??
SOMA HII NA CHEKA KWA KUONGEZA AFYA
*SOMA HII NA CHEKA KWA KUONGEZA AFYA.*
*Mwerevu na Mjinga walienda ktk usaili, walipofika kabla hawajaingia wakakubaliana aanze Mwerevu kisha akitoka ampe majibu Mjinga ili wote wapate kazi.*
*Basi Mwerevu akaingia na maswali yakawa hivi:-*
*Msaili:- Tanzania ilipata Uhuru mwaka gani?*
*Mwerevu:- ilitakiwa iwe mwaka 1960 ila ikasogezwa mpaka 1961 kutokana na sababu mbalimbali..*
*Msaili:- Nani hasa alihusika na upatikanaji wa Uhuru huo?*
*Mwerevu:- Kuna watu wengi walihusika ila Mwl. J.K. Nyerere ndiye alikuja kumalizia.*
*Msaili:- Inasemekana katika sayari ya Mars kuna viumbe wanaishi, je ni Kweli?*
*Mwerevu:- Watu wengi wanasema hivyo lakini haijathibitishwa na wanasayansi.*
*Baada ya Mwerevu kutoka basi Mjinga akapewa majibu yote..*
*Kuingia ktk usaili maswali yakawa hivi:-*
*Msaili:- Tuambie ulizaliwa mwaka gani?*
*Mjinga:- Ilitakiwa iwe mwaka 1960 ila ikasogezwa mbele mpaka mwaka 1961 kutokana na sababu mbali mbali.*
*Msaili:- Mungu Wangu, BABA yako anaitwa nani?*
*Mjinga:- Kuna watu wengi walihusika ila Mwl. J. K. Nyerere ndiye alikuja kumalizia .*
*Msaili:- Hivi wewe ni chizi?*
*Mjinga:- watu wengi husema hivyo lakini haijathibitishwa na wanasayansi*😂😂😂😂😂😂
Chemsha akili kidogo
*Chemsha akili kidogo...!!
Najua nina marafiki vichwa hasa...😊.
Naomba mnipe jibu . nguo inauzwa 10,000/= huna pesa ukaendakukopa kwa dada 5,000/= na kaka 5,000/= jumla 10,000/= ukaenda dukani ukaomba upunguziwe ukauziwa 9,700/= ukabakiwa na 300 ukapunguza deni kaka yako ukampa 100 dada ukampa 100 ukabaki na 100 jumla kaka akawa anakudai 4,900 na dada 4,900 ukijumlisha unapata 9,800/= ukiongeza na 100 yako uliyobakinayo unapata 9,900/=je? 100 iko wapi? Yani ukinijibu wewe mkali*
tabasamunafuledi.blogspot.com
Siku nilipogundua kwamba bangi sio mchicha,,, usiisome
Siku nilipogundua kwamba Bangi sio mchicha ni ile ambayo nilitoka ndani kwenda kutoa pesa kwa m- pesa na Remote ya TV simu nikaacha ndani..... Nilipofika kibanda cha m-pesa name rimoti ya tv mzee akniangalia na ktingisha kichwa....... Ikanibidi nirudi home nichukue simu, nilipofika nikakuta giza nikachukua simu kwenye meza na kuwasha tochi ili nitafute simu yangu lakini sikuiona...... Ikanibidi nimpigie mama ili anibip kwenye namba angu simu nijue iko wapi....... Akanijibu Siku ukiacha bangi ndio utajua simu yako ndio unatumia kunipigia...
Wanaume someni hii inawahusu
Watanzania akili zetu zipo mikiani sijui
Watu wanavituko
Watu wanavituko...
Some parents will write *BEWARE OF DOGS* at their gate when their daughter is 18yrs old...
But when she reaches 30yrs without getting married they change it to *TUNAUZA MAJI*
VITU SITA (6) USIVYOTAKIWA KUFANYA KABLA YA KULALA.
1 - USILALE UKIWA UMEVAA SAA. Saa ya mkononi ina madhara iwapo utaivaa kwa muda mrefu, wanasayansi wanashauri sio sahihi kulala ukiwa umevaa Saa(ya mkononi)
2 - USILALE UMEVAA SIDILIA(wanawake wanayovaa kwenye matiti ). Wanasayansi wa America wamegundua kuwa wanaovaa sidilia zaidi ya masaa 12 Wako kwenye hatari zaidi ya kupata Kansa ya matiti.
3 - USILALE NA SIMU IKIWA KARIBU. wanasayansi wanashauri usiweke simu pembeni kwasababu ya mionzi ya simu sio salama hasa ukiwa umelala, ni vizuri ukaizima kama ni lazima ukae nayo karibu.
4 - USILALE UKIWA UMEWEKA MAKE - UP (usoni). Hii usababisha ngozi kutopumua vizuri na kutopata usingizi kwa haraka.
5- USILALE NA CHUPI- Hili kuwa huru na kulala ni vyema ukalala bila kubanwa na kitu chochote, chupi haitakiwi. KITU CHA MWISHO NA CHA MUHIMU KULIKO VYOTE NI ....
6 - USILALE NA MKE/MUME WA MTU. wanasayansi wanasema jambo kama hili linapotokea na ukabainika linaweza chukua uhai wa mtu, ni vizuri ukawa makini sana hapa!...
Unaruhusiwa kukomenti kama unachakusema kuhusu hizi mambo.
FUATA SHERIA BILA SHUTRUTI...
wali Je, nimshtue Mchungaji au ndio muujiza alioniombea umetokea?
Mdanganye mwanamke na utaona jinsi atakapoyafanya maisha yako kuwa magumu zaidi ya jehanamu hapa duniani
2. Usimpe maneno ya kumnyanyasa
3. Usimfanye aone kudharauliwa
4. Usimfanye aone hapendwi
5. Usimbake
6. Usimdanganye na kuwa na wanawake wengine
7. Usiichukie au kutoipenda lugha yake ya
mapenzi.
Mpe utofauti atakupa upendo
Mpe tabasamu atakupa furaha
Mpe moyo wako atakupa maisha yake
Mpe nyumba atakupa familia bora
Mpe wazo lako atakupa mpango wa kutimiza
wazo lako.
Mfanye malkia atakufanya mfalme
Mpe mapenzi naye atakuwa wako tu
Ila mdanganye na utaona jinsi atakapoyafanya
maisha yako kuwa magumu zaidi ya jehanamu
hapa duniani
KAMA HUKUPITA KATIKA MOJA YA SHULE HIZI JUA WEWE NI KILAZA
Ilboru Secondary
Kibaha Secondary
Tabora Boys Secondary
Tabora Girls Secondary
Msalato Secondary
Kilakala Secondary
Pugu Secondary
Minaki Secondary
Azania Secondary
Tosamaganga Secondary
Mkwawa Secondary (Casino)
Milambo Secondary
Mazengo Secondary
Tanga Technical Secondary
Galanos Secondary
Magamba Secondary
Kibiti Secondary
Shycom
Kigoma Secondary
Sengerema Secondary
Kantalamba Secondary
Jangwani Secondary
Malangali Secondary
Forodhani Secondary
Nsumba Secondary
Bwiru Boys Technical
Bwiru Girls Secondary
Nganza Secondary
Mwanza Secondary
Arusha Secondary
Umbwe Secondary
Machame Girls
Weruweru Girls
Moshi Technical
Iyunga Technical
Ifunda Technical
Kigonsera Secondary
Songea Boys Secondary
Bihawana Secondary
Mwenge Secondary
Shybush Secondary
Mwanza Secondary
Mara Secondary
Musoma Alliance
Tarime Secondary
Ihungo Sekondary
Usagara Secondary
Old Moshi Secondary
Kwiro Secondary
Same Secondary
Tambaza Secondary
http://tabasamunafuledi.blogspot.com/p/advertise-with-us.ht…













