Showing posts with label Malezi. Show all posts

Baada ya kila dhoruba kali nuru huonekana

Nilikulia katika kijiji kimoja kusini mwa Tanzania na mama yangu yeye alikuwa mwalimu wa chekechea wa kujitolea katika shule hiyo ya watoto wadogo pale kijijini.
Mtu niliyeambiwa kuwa ni baba yangu alikuwa ni mlevi wa kupindukia pale kijijini na fundi selemara aliyemiliki sehemu ndogo ya kufanyia kazi kama ofisi yake ya kujipatia kipato ambacho alikitumia kwa kununulia pombe na kubaki katika maisha duni sana.
Baba huyu alikuwa mkali akimpiga mama na mimi kila siku na sitaki kukumbuka jinsi kila siku mama alivyonikumbatia na tukasaidiana kulia tukimwomba Mungu ambadilishe baba huyu ambaye pia alikuwa na wake wengine wawili na kunifanya kutambua kuwa mama yangu alikuwa ni mke wa nje wa baba.
Nililia na kumwomba Mungu ayabadilishe maisha yetu kila siku na nilifurahi sana kila siku jumapili nilipomwona mama akiimba kwa furaha katika kwanya pale kanisani na kunifanya kufurahi kila ifikapo jumapili ambapo ndio nilimshuhudia mama yangu akiwa na furaha ya ajabu na kuyasahau magumu ya nyumbani na kumshukuru Mungu.
Mama alinifanya kuona kuwa kanisani na kumwomba Mungu kipindi hicho ndio ilikuwa faraja yetu kubwa na alinisisitiza kuwa nitafanikiwa na kuwa mtu mkubwa katika maisha haya na kunifundisha kusamehe.
Somo la kusamehe lilinikaa sawa sawa na kumsamehe baba yangu kwa kila alichomfanyia mama na kusababisha maisha yetu kuwa magumu hasa baada ya kumpa mama ujauzito uliomfanya aishie kidato cha tatu na kusitisha masomo ili anikuze mimi huku familia yake ikimtenga na kuanza maisha yake.
Nilimsamehe na miezi michache baadae alifariki baada ya kupata tatizo la mapafu yaliyoharibiwa na uvutaji wa sigara na kufa kwa kukosa fedha za kumfanya atibiwe katika hospitali kubwa pamoja na jitihada za kuuza ardhi yetu na baadae maisha yetu yakazidi kuwa magumu.
Nakumbuka kila siku asubuhi nikiwa naenda shuleni jinsi mama alivyonipa nguvu na maneno ya ujasiri yenye uthubutu kuwa nitakuja kufanikiwa na kuitunza familia yetu na pia nakumbuka jirani yetu mama fred ambavyo yeye naye aliwahi kunipa zawadi ya viatu pamoja na ufukara wake ambao ulilingana na ule wetu na kuniambia kila nivaapo vinifanye niamini nitafanikiwa kuyakanyaga maumivu yote na kusonga mbele kufuata sauti ya ushindi na kuja kuwa mtu mwenye mafanikio.
Kila nilipovivaa viatu vile nilihisi kuwa yale maumivu ya mama na maumivu ya ufukara wetu wa kutisha pale kijijini kuna siku ningekuja kuyakanyanga na kumvalisha mama viatu vya furaha na kuja kumfanya maisha yake yote yawe ya furaha na tabasamu kama awapo kwenye kwaya yake siku za jumapili, kwa kweli nilikuwa nikisikia sauti za mafanikio zikiniambia nijitume..
Siku moja tukiwa shule ya sekondari tumekaa kando ya barabara tunacheza na kufurahi mbele yetu alikuja baba mmoja akiwa kashika begi mkononi na mkono mwingine kashika fimbo na miwani jambo lilinifanya nihisi kuwa mzee yule alikuwa ni kipofu.
Akaomba kwa sauti "wanangu naomba mnisaidie kuvuka barabara!"
Hakuna aliyemsikiliza zaidi ya watu kumcheka pale na kuendelea kucheza, mimi nikaamua kusimama na kwenda kumsaidia na nilipofika pale nikamwambia
"naweza kukusaidia?"
Akajibu "ndio"
Nikamwambia naomba nishike bega langu la kulia na nikamvusha na kumbe alikuwa anakuja pale shuleni kwetu na baada ya kuniuliza ni sehemu ipi anaweza kukaa na kumwonesha basi akalifungua lile begi lake na kutoa pipi na biskuti na kuzitandaza juu ya kitambaa chake na kuanza kuziuza na mimi akiniambia,
"mwanangu Mungu atakubariki sana na nitatamani siku nifungue macho yangu kuona mafanikio yako kwani sauti yako tu inanionyesha una hekima na huruma"
Nilimwangalia kwa dakika kadhaa nikiwa pembeni huku akiuza pipi, chocolate na biskuti zake kisha machozi yakanitoka na kushindwa kuyahimili na kuondoka zangu kurejea kwa wenzangu.
Tuliendelea kuwa marafiki na kila siku muda kama ule nilimsaidia kumvusha pale baada ya kuniulizia dan niko wapi, kusikia sauti yangu na mara nyingine alinikuta namsubiri nimvushe pale.
Kuna siku nilifika pale kituoni na kugundua hajafika nikakaa pale kwa dakika kadhaa nikiwa nimejificha sehemu na alipofika nikaaendelea kukaa pale na hakumwita mtu mpaka watu wakaondoka nami nikamsogelea na kukaaa kimya kwa dakika bila kuongea kitu na baada ya watu wachache kupita akaniita "DAN"
Nikaitika nakusema "NAAM", umejuaje kuwa nitakuja na kwanini hujamwomba mtu yoyote akusaidie kuvuka?
Akaniambia " Niliamini kuwa utakuja kwa kuwa wewe ni rafiki na kuna sauti iliniambia lazima utakuja nami nikakusubiri"
Nilishangaa wala sikuongea kitu chochote na kumsaidia kuvuka kisha tukaenda na nikamwacha akiuza nami nikaingia darasani.
Alikuwa rafiki kwani kuna nyakati nilimsaidia hasa pale wanafunzi walipokuwa wakimlipa shilingi mia tano badala ya alfu moja wanunuapo vitu na kunifanya mimi kuwa na maadui wengi pale shuleni zaidi ya marafiki na ikafika kipindi nahitimu pale aliniita na kunipa yeye aliyoiita zawadi ya kuwa
"mwanangu utafanikiwa kama nawe utaisikia sauti ya mafanikio kama mimi nilivyokuwa na imani kuwa kila mara ungenisaidia na ukawa hivyo"
Nilimjibu amen na kuondoka ingawa nilihisi nampoteza rafiki ambaye alinijenga sana.
Miaka miachache baadae kwa jitihada za mama yangu nilifanikiwa kuhitimu chuo kikuu na kupata kazi katika kampuni moja ya kutengeneza vitabu na kipata mwanya wa ufadhili na nikaandika historia ya maisha yangu niliyoiita "Maisha ya Salome na Mwanae Dan" kitabu ambacho kikauzika sana na kunifanya mimi kuweza kumtunza mama.
Nilirudi mpaka ile shule na kumulizia rafiki yangu yule ambaye alikuwa kipofu na kwa bahati mbaya niliambiwa alifariki kwa ajali ya gari baada ya kujitahidi kuvuka barabra kwa kukosa msaada na kugongwa na gari. Nililia sana na kuishia kubaki na yale aliyoniambia na mpaka sasa mimi na mama tuna shirika la kusaidia wajane na walemavu wa macho liitwale "fuata sauti yako foundaton"
Kwa nini nimetaka kuandika kisa hiki cha kufikirika?
Kila mtu ana historia ya mapito magumu katika maisha yake na pengine hata sasa una wakati mgumu sana na hujui nini cha kufanya.
Hebu fikiri wakati mama yangu ananyanyasika na kufanya kazi kwa taabu ili kunipa maisha mimi aligundua kuwa ana tone la furaha na kulitumia ipasavyo hasa zile nyakati za kwenda kanisani na kuimba na wenzake na kusahau maumivu ya muda na kujipanga kuona atayakabili vipi.
Mama Fred yeye hakuwa na fedha sana na alikuwa ni maskini kama sisi lakini vile viatu ambavyo alinunua na kunipa pamoja na yale maneno mazuri vilinihamasisha kufanya vizuri. Je wewe umekuwa msaada kwa wenzako hata kama na wewe unaona huna kitu? Umewapa maneno ya faraja au umekuwa ukifurahia magumu yao?
Yule kipofu aliomba msaada na wengi wakawa wakimwangalia na kumcheka je ni mara ngapi na wewe umeomba msaada na watu na kuchukulia ni utani na kuja kujutia baada ya kugundua kuna mtu ulishindwa kumsaidia katika nyakati aliyohitaji msada wako?
Ni mara ngapi umewasamehe wale waliokufanyia mabaya na hata kuwafanyia mabaya wale uwapendao mbele yako kama nilivyomshuhudia baba akimnyanyasa mama na mwisho wa siku nikamsamehe ingawa alifariki baadae hata kabla ya kuja kula mafaniko ya mwanae?
Ni mara ngapi umesaidiwa na kuwa na shukrani hata ya maneno mazuri kama vile yule kipofu alivyomfanyia dan na hata kujenga imani ya kuwa huyo mtu aliyekusaidia unahitaji kumwamini na kuuthamini mchango wake?
Ni mara ngapi umerudi kuwashukuru wale waliokusaidia nyakati za shida au ulivyowahitaji wakusaidia na wakakusaidia?
Katika kufanikiwa kwako au katika jitihada za mafanikio yako umefuata sauti liyomo ndani yako kuwa utafanikiwa na ukaishi kwa ndoto zako huku ukijituma na kujikabidhi kwa mungu ?
Baada ya kila dhoruba kali nuru huonekana ....... nakutakia wiki hii kuwa ya mafanikio kwako......AMEN-------------> share ------------>

MUHIMU KUJIKUMBUSHA HAYA KUHUSU MFALME DAUDI

Siku moja mfalme Daudi akiwa katika moja ya vyumba vyake kupitia dirishani alimwona mwanamke mmoja nyumba jirani akiwa anaoga.
Daudi akampenda sana na kuwatuma watumishi wake wakatafute habari zake nao waliporudi wakamwambia kuwa yule ni Bath-sheba mke wa Uria ambaye ni jemadari wa vikosi vya israel.
Mfalme Daudi akaomba binti yule apelekwe katika jumba la kifalme na akalala naye.Baada ya siku kadhaa yule binti akapeleka ujumbe kwa mfalme Daudi kuwa alikuwa na mimba yake.
Daudi akapeleka ujumbe kwa mkuu wa vikosi vilivyokuwa vitani Yoab kuwa amwambie Uria arudi mara moja. Uria akafika na baada ya kuulizwa hali ya vita mfalme Daudi akampa baadhi ya zawadi na kumruhusu aende nyumbani akijua angelala na mkewe na mimba ikawa yake.
Asubuhi akashangaa baada ya kuamka na kuambiwa Uria na watu wake hawakwenda majumbani mwao ila walilala mlangoni pake.
Mfalme akamwita Uria na kumuuliza kwa nini hukwenda kulala kwako? Naye akajibu kuwa kamwe nisingeweza kwenda kulala na kufurahi nyumbani wakati kuna watu wako vitani wakiumia.
Wakalala pale na siku ya pili Uria akaondoka kurudi vitani bila kwenda kwake na ndipo mfalme Daudi akatuma ujumbe kwa yoab kuwa uria apangwe mstari wa mbele kwenye mashambulizi makali na kisha wenzake wamwache apigwe hadi kufa.
Yoab akafanya hivyo na baada ya muda wa maombolezo ya kifo cha Uria kwisha, Daudi akamchukua Bath-sheba na kumfanya mke wake ndani ya jumba lake na akamzalia mtoto.
Mungu akamtuma Nathan na kumwambia Daudi, “Palikuwa na wanaume wawili waliokuwa katika jiji moja, mmoja alikuwa tajiri na yule mwingine alikuwa maskini.
Yule mwanamume tajiri alikuwa na kondoo na ng’ombe wengi sana; lakini yule mwanamume maskini hakuwa na chochote isipokuwa mwana-kondoo jike mmoja, aliye mdogo, ambaye alikuwa amenunua.
Naye alikuwa akimhifadhi hai, na huyo kondoo alikuwa akikua pamoja naye na wanawe, wote pamoja. Kondoo huyo alikuwa akila tonge lake, na kunywa kutoka katika kikombe chake, naye alikuwa akilala kifuani pake, na kondoo huyo akawa kama binti kwake.
Baada ya muda, mgeni akaja kwa yule mwanamume tajiri, lakini hakuchukua kutoka kati ya kondoo zake na ng’ombe zake ili kumwandalia yule msafiri aliyekuja kwake. Kwa hiyo akachukua yule mwana-kondoo jike wa yule mwanamume maskini, akamwandalia yule mtu aliyekuja kwake.”
Ndipo hasira ya Daudi ikamwakia sana yule mwanamume, naye akamwambia Nathani: “Kama Yehova anavyoishi, mtu huyo aliyefanya hivyo anastahili kufa Na kuhusu yule mwana-kondoo jike, atamlipa mara nne, kwa sababu yeye amefanya jambo hili na kwa sababu hakuwa na huruma.”
Ndipo Nathani akamwambia Daudi: “Wewe mwenyewe ndiye yule mwanamume!
Basi Daudi akamwambia Nathani: “Nimemtendea Mungu dhambi.” Kwa hiyo Nathani akamwambia Daudi: “Yehova naye ameacha dhambi yako ipite. Hutakufa. Ingawa hivyo, kwa kuwa bila shaka hukumheshimu Yehova kwa jambo hili, pia yule mwana, uliyemzaa, atakufa hakika. Kisha Nathani akaenda zake nyumbani kwake.
Na Mungu akampiga yule mtoto ambaye mke wa Uria alikuwa amemzalia Daudi, akawa mgonjwa.
Mfaleme daudi akafunga akilala chini na kumwomba Mungu amponye yule mtoto huku akilia na hata wafanyakazi wake walipotaka kumnyanyua yeye alikataa akiendelea kuomba kwa siku kadhaa.
Siku moja watumishi wake wakawa wananong'onezana jinsi ya kumwambia daudi kuwa mtoto yule amekufa. Wakasema kama wakati akiwa hai aliomboleza vile itakuaje kusikia amekufa?
Daudi akagundua wakiwa wananong'onezana akawauliza amekufa? wakajibu ndio... ndipo akanyanyuka na kwenda kuoga, akavaa mavazi mapya , akaenda nyumba ya bwana kusujudu na kisha akaomba aletewe mkate wale watumishi wakashangaa na kumuuliza,
“Ni nini maana ya jambo hili ambalo umefanya? Ulifunga na ulikuwa ukimlilia mtoto alipokuwa hai; na mara tu mtoto alipokufa ukasimama, ukaanza kula mkate.”
Daudi akajibu, “Nilifunga, nikawa nikilia mtoto alipokuwa bado hai, kwa sababu nilisema,
‘Ni nani anayejua kama Yehova huenda akanipa kibali, na hakika mtoto aishi?’ Sasa kwa kuwa amekufa, kwa nini nifunge?
Je, ninaweza kumrudisha tena? Mimi nitakwenda kwake, lakini yeye hatarudi kwangu.”
Na Daudi akaanza kumfariji Bath-sheba mke wake. Na zaidi ya hayo, akaingia kwake, akalala naye. Baada ya muda akazaa mwana, naye akaitwa jina lake Sulemani. Na Yehova akampenda mwana huyo. Basi akamtuma Nathani na kumwita jina lake Yedidia, kwa ajili ya Yehova.
Funzo
*Hakuna kitu kibaya kama tamaa ya kutaka kutamani mali isiyo yako na kuichukua kwa hila kama mfalme daudi alivyoweza mpokonya mke wa uria na kisha kuamuru Uria awekwe mstari wa mbele katika mapigano ili afe
*Mungu akiamua kukuumbua huwezi jificha hebu fikiri jinsi Daudi alivyoamua kutumia ujanja wa kumrudisha Uria ili alale na mkewe na mimba ionekane yake lakini bado ikashindikana na pia jinsi alivyomtuma Nathani na kwenda kumpa daudi mfano uliogua tukio lake
*Mungu pia huchukizwa na dhami za tamaa kama alivyoweza kumadhibu daudi na kumuua yule mtoto
*Kwa kula anguko ni muhimu sana kumrudia mungu wako kama vile daudi alivyolitambua kosa lake na kisha kuomba msamha kwa Mungu wake wa kweli
*Ni vizuri kuacha mambo yapite na kutoyakumbuka kama vile mfalme daudi baada ya mtoto kufa alivyosahau na kuanza maisha mapya na kisha kuja kupata mtoto sulemani ambaye pia Mungu alipendezwa naye na baadae alikuja kuwa mfalme mwenye hekima
Ni vyema tuutumie mfano huu wa Daudi kusahihisha maisha yetu na jinsi tunavyoishi na jamii inayotuzunguka na matendo yetu kwao.
Kama umeelewa comment Amen na kisha share

Dondoo 9 muhimu sana kwa Wazazi na Wazazi watarajiwa wote

Dondoo 9 muhimu sana kwa Wazazi na Wazazi watarajiwa wote
1. Mkanye mtoto wako wa kike kuhusu kukubali kupakatwa hovyo, bila kujali ni nani anampakata, hata kama ni mjomba wake.
2. Usivue nguo mbele ya mwanao pindi akifikisha miaka 2 au zaidi. Jifunze kumwomba akupishe.
3. Usiruhusu mtu yoyote amwite mwanao “Mchumba”, “Mke wangu” au “Mme wangu”.
4. Kila wakati mwanao anapoenda kucheza na wenza ke, hakikisha unafuatilia kujua wanacheza nini, siku hizi hata watoto wanafundishana michezo michafu.
5. Kama mwanao ameonyesha kutopenda kwenda mtu fulani usimlazimishe, pia chunguza kwa ukaribu ili kujua sababu.
6. Inashauriwa kupitia kwanza mwenyewe movie yoyote kabla ya kuruhusu mwanao waiangalie.
7. Mwanao anapofikisha umri wa miaka 3 anza kumfundisha jinsi ya kusafisha sehemu zake za siri mwenyewe, na umuonye asiruhusu mtu yoyote kumshika sehemu hizo. (Hata wewe mwenyewe)
8. Mfundishe mwanao thamani ya kuishi bila kufuata mkumbo.
9. Mwanao akilalamika kuhusu mtu fulani, usikae kimya.

Kama unadhani Dondoo hizi ni Muhimu, usisahau ku Share na wenzako. Kutokana na sociology tips nadhani itasaidia plz take care katika malezi ya mtoto wako na waliokuwa hawana wamuombe Allah awape kizazi chema tulizo la macho yao

TAHADHARI!!!!!!!!!!!!!!!!!! Kwa wazazi wote wanaopenda kuwaonesha watoto wao katuni... hii inawahusu




Good evening Parents.

THIS IS AN IMPORTANT ALERT!!! Nickelodeon CARTOON LOUDHOUSE (DStv) has launched a new series featuring a Married gay couple!!! Let us be vigilant what our children are watching on cartoon networks for their betterment. This is a way of making homosexuality acceptable to our children later in life!!
Have a blessed day and spread the news.

Soma zaidi HAPA