HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU " Season 7
HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Season 7
ILIPOISHIA JANA
Sikuwaza yeye kuchukua simu lakini hofu yangu ilikuwa ni ifikapo saa sita nini kingejiri.Mida ikazidi kusogea na ilipofika saa sita kasoro dakika tano.......................... .............................. .............................. ................
Endelea
SIKUWAZA yeye kuchukua simu lakini hofu yangu ilikuwa ni ifikapo saa sita nini kingejiri.
Mida ikazidi kusogea na ilipofika saa sita kasoro dakika tano akili ikanituma nichukue kidonge kimoja cha valiamu dawa ya usingizi na kumchanganyia kwa siri katika juice yake.
Kwa kweli siku hiyo nilijifanya mwenye mapenzi ya kweli na kumjali ila moyoni mwangu nikijua nini nilikihitaji.
Basi nilimbembeleza na kumpa ile juice na kweli alikunywa na zilipita dakika kadhaa nikagundua alikuwa kalala fofofo.
Hapo nikapata mwanya wa kuichukua ile simu ili niweze kuiweka ile vocha na kuipiga ile namba.
Kweli nikaipiga ile namba ila iliita kwa dakika kadhaa bila kupokelewa na nikaamua kutoipiga tena ila kichwani nikiawa na mawazo.
Wakati natafakari kwanini simu haijapokelewa na iweje nimefikia hatua kumwekea mke wangu dawa ya usingizi aina ya valium, na je ni kweli mimi ni mtu wa kuchangaywa na simu ya mtu ambaye simfahamu?
Wakati nayatafakari hayo ilikuwa mida ya saa saba usiku na usingizi ukiwa umenipotea.
Nikaamua kutoka nje na kukaa pembezoni mwa ziwa nikiwa natafakari peke yangu mambo yaliyojitojeza katika maisha yangu pasipo na jibu sahihi.
Nikiwa na dimbwi la mawazo mara nikashtushwa na mkono ulionigusa niliposhtuka alikuwa ni muudumu akisema.
" vipi ndugu mbona uko peke yako usiku huu wa manane hapa nje?"
Nikamjibu kwamba, " nimeamua tuu kuja hapa nje baada ya kugundua ndani kuna joto sana.'
Mhudumu alitabasamu na kuniambia, " hili eneo ulilokaa sio salama, maana mara nyingi nyakati za usiku kuna vitu vya ajabu hutokea hivyo haturusu watu kukaa hapa mida hii"
Wakati tukiondoka kutoka eneo hilo huku tukijadili mambo mawili matatu mhudumu akagundua mambo mawili matatu na pomoja na hayo una matatizo.
Kweli nikatamani nimweleze nini kinachonisibu ili nipate ahueni ila nilishindwa na kubaki kumwambia hakuna shida.
Wakati twakaribia mlango wa chumbani wangu mara ulisikika mlio wa zimu kutoka kwenye chumba cha mhudumu na ule mlio ukanishtusha sana.
Mhudumu akakimbia na kwenda katika chumba chake ili apokee ile simu
Huku nyuma akaniacha nikiwa niko kwenye mawazo sana kuwa nini kitatokea hivyo nikawa nasubiri kuona nini kingejiri kama mgonjwa wa ukimwi.
Kweli baada ya kupita dakika 3 nikamwona mhudumu akitoka na kuja kwangu kila hatua aliyozidi kuja kwangu tumbo langu nalo likazidi kuvurugika.
Nilitamani nikimbie ila nikavumilia na kumwacha afike. Kweli neno la kwanza alilosema lilinifanya nihisi dunia ikipasuka.
Kwani alisema hivi.....................
MAONI SHARE WHATSAPP 0713317171
0 comments: