HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU " Season 8

07:47:00 Unknown 0 Comments



HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Season 8
ILIPOISHIA 
Huku nyuma akaniacha nikiwa niko kwenye mawazo sana kuwa nini kitatokea hivyo nikawa nasubiri kuona nini kingejiri kama mgonjwa wa ukimwi.
Kweli baada ya kupita dakika 3 nikamwona mhudumu akitoka na kuja  kwangu kila hatua aliyozidi kuja kwangu tumbo langu nalo likazidi kuvurugika.
Nilitamani nikimbie ila nikavumilia na kumwacha afike. Kweli neno la kwanza alilosema lilinifanya nihisi dunia ikipasuka.
Kwani alisema hivi.....................
Endelea
ALIFIKA na kusimama  kwa  sekunde kadhaa bila kusema neno lolote huku akiniangalia usona kama abiria aliyebanwa na tumbo la kuhara katikati ya mbuga za wanyama pale mikumi na uwezekanao wa basi kusimama haupo.
Neno la kwanza alilolisema lilisema , " Umemfanya nini mkeo?" 
kwa kweli nilishtushwa sana na swali hilo na kujua kapata wapi hizo taarifa? Imekuaje wakati tukio nalifanya nilikuwa peke yangu?
Ikanibidi nimhoji kama sijui nini kinaendelea muda huo, " Binti kwa nini umeniuliza swali hilo? Mbona mke wangu kapumzika muda huu au unajifunza umbea?"
Na wakati huu nilijifanya kucharuka lakini wakati nimebadilisha sura maneno yaliyofuata yalinifanya niwe mpole kama paka aliyemwagiwa maji. Binti alisema hivi, " Simu niliyopokea imeniambia kila kitu kuhusu wewe"
Majibu haya yalinishtua zaidi na kunifanya nilegee kama mlenda wa iyunga, basi bwana kila kitu kilinibana kuanzia haja kubwa mpaka haja ndogo na jasho likaanza kulinyemelea paji la uso na kuona pombe zote zilizokuwa kichwani kutoweka.
" Sauti ya kike ilisema kuwa wewe umemfanya mkeo alale ili wewe ufanye mambo yako kinyume na makubaliano yenu hivyo sasa amesema kuwa mkeo akiamka upige simu na usirudie ujinga ufiofanya mbona yeye anakupigia mkeo akiwa macho?" aliongeza kusema binti yule
uuuuh, kwa kweli ukiyastaajabu ya musa utayaona ya tabasamu na fuledi, basi bwana sikutaka kujadiliana naye nikatimka na kurudi chumbani haraka na kujifunika kitandani gubigubi huku nikitetemeka kama simu ya mchina.
Nilipitiwa usingizi mzito na baada ya kufumbua macho kulikuwa kumekucha na mke wangu akiandaa mabegi kwa ajili ya safari ya kurudi nyumbani.
Sikutaka kamwe kwenda kuaga zaidi ya kumwomba mke wangu aende kuwaaga kwani nilihisi nigepewa ujumbe wa kunifanya nibaki pale jambo ambalo ningeamsha malaria ambayo nilihisi ikininyemelea.
Tulianza safari tukiwa wenye furaha huku nami nikijitahidi kujisahaulisha mikasa yote na kucheza na mwanangu pachu huku mama pachu akituendesha na tulipofika kiwira tulishuka na kufanya manunuzi ya vitu vya nyumbani kwani hatukuwepo kwa muda mrefu na tulihitaji pia kumsalimia rafiki yetu pale.
Muda wote huo nilikuwa nimeizima simu yangu ili kutunza chaji maana ilibaki jiwe moja na nilihitaji nikifika niandike kisa cha kupost tabasamu na fuledi pamoja na kuchati na marafiki wajue niko maeneo gani.
Namshukuru Mungu tulifika nyumbani salama na huwezi amini nyumba ilikuwa chafu sana tukaanza kushusha mizigo na baadae nikamwacha mama pachu akifanya usafi nami nikaingia bafuni kuoga na niliporudi nikachukua simu yangu na kuelekea sebuleni ili niwashe simu yangu na kuangalia TV nione yapi yamejiri kwa siku hiyo.
Nilipowasha simu ziliingia meseji kadhaa kutoka kwa marafiki zangu nikawa nazisoma moja moja na kuzijibu, laaah haula!! moja kati ya meseji zilizoingia nashindwa hata kukuambia............................................................................................................................................. Je ni ni kiliandikwa katika meseji hiyo? usikose kuungana nami kesho muda kama huu 

You Might Also Like

0 comments: