HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU " Season 6
HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Season 6
ILIPOISHIA JANA
Tukaruhusiwa muda mfupi baadae na kuelekea hotelini ambako tulipofika hotelini mhudumu wa hotel aliniita na kuniambia kuwa nina ujumbe wangu.
Ujumbe huo ulitoka kwenye namba ilele na baada ya kuzisoma zile namba nikagundua ni namba ile ile ambayo hunipigia
Ujumbe ule ulisema hivi, .....................................................
Soma mwendelezo wake
UJUMBE usilisema hivi, " Nimekutumia vocha ya shilingi elfu 10, sasa leo naomba wewe unipigie saa sita kamilia.... USIKOSE" Sikutaka yule dada agundue kitu, hivyo nikatabasamu kwa uoga..... nakuanza kuondoka.
Kwa kuwa nimechanganyikiwa na ule ujumbe bila kujua amefahamu vipi namba ya yule mhudumu na kama haitoshi kwanini atume pesa na ni mpigie bila kukosa? na wakati yeye akipiga tu nahisi kuzimia..... nikahisi roho yangu ingeweza kutoweka muda wowote.
Wakati natafakari hayo nikashtushwa na kelele za mlango uliogongwa na mke wangu kumbe nilikuwa nimejifungia na kusahau kama nilikuwa na familia. Nikakimbia haraka na kuufungua mlango na halafu nikarudi kwa spidi kuenda katka eneo ambalo kila habari mbaya ikinikuta huwa mtetezi wangu (chooni).
Mke wangu akaanza kupatwaq na mashaka kwani mara kwa mara aliona tabia yangu imebadilika na kwa muda huo nilishaingia chooni kama mara tatu. Akaniuliza, " kuna kitu nahisi kinaendelea na hutaki kunishirikisha"
Kwanza siku hizi unapigiwa sana simu nyakati za usiku kuanzia saa sita, nas ukipokea akili yako huonekana imechanganyikiwa baada ya kupokea hiyo simu.... Nini tatizo baba Pachu?
Nikashtuka na wazo la kwanza likanijia kuwa leo saa sita usiku natakiwa kupiga simu na mama pachu kagundua mida hiyo huwa napokea simu, sasa leo sipokei tena ila natakiwa kupiga na tena sio kwa iyari bali lazima kutokana na uzito wa ile sms na nikizingatia shimfahamu.
Kweli nilizidi kuchanganyikiwa kiasi cha kwamba sikuelewa tena maneno ya mama pachu aliyoongea baadae. wakati nikiwa pale mra nikashtushwa na mlio wa simu bila kujua ni ya nani kati yangu na mama pachu.
Nikaikimbilia na kuichukua haraka sana kukimba nayo chooni nilipofika chooni nikagundua ni ya mama pachu nikarudi haraka na kumpa mama pachu kumbe ilikuwa ni ya baba mkwe akiulizia hali ya mjukuu wake.
Mama pachu alikuwa akiongea na simu huku akinitazama na macho yake yalionesha kuwa mama pachu hakuwa akinielewa tena wakati huo nilikuwa nikizunguka huku na kule bila kujua nini nitamjibu mama pachu baada ya kuonge ana simu.
Baada ya kukata simu mama pachu akachukua simu yangu na kusema sasa atakaa nayo kwa ili kujua nini naendelea nacho maana alihisi nimeanza nimechanganyikiwa ingawa hakuwahi kuikuta sms yoyote mbaya kutoka kwa michepuko.
Sikuwaza yeye kuchukua simu lakini hofu yangu ilikuwa ni ifikapo saa sita nini kingejiri.Mida ikazidi kusogea na ilipofika saa sita kasoro dakika tano......................................................................................................
Je ilipofika saa sita maajabu gani yalitokea?
Itaendelea kesho muda kama huu
Nakutakia jioni njema
Share kama umeipenda
0 comments: