HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU " Season 11
HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "Season 11
ILIPOISHIA
Alishangaa sana na kunilaumu kwa kukaa kimya kwa muda wote huo na kuniomba nimpe meseji hizo ili azisome mwenyewe na kuhakikisha maana aliona ni kama filamu, eti kudume mimi natishiwa mpaka nanusurika kugongwa tako na bodaboda kisa ujumbe wa simu???? Haikumwingia akilini.
Aliichukua simu ile na alipoifungua meseji ya kwanza alishtuka na kuniambia.................................................................................
Endelea
ALIICHUKUA simu ile na alipoifungua meseji alishtuka na kuniambia, " Kaka vipi mbona hii meseji inanihusu mimi" alinisomea ile meseji na ilisomeka hivi, " Unajifanya kumtafuta mwakibubu? Tena huyo ndio nilikuwa namtafuta sana ana yake naye ya kujibu"
Mwakibubu alinirudishia simu na kunihoji , " Hiki ni nii? au umekuja kunitania????
Mara ya kwanza sikumwalewa nikaanza kuhisi kachanganyikiwa nikaichukua ile meseji na kuisoma mwenyewe.
Kweli iliandikwa vile na wakati naitafakari ile meseji na mwakibubu akijifuta futa jasho la uoga simu iliita na safari hii haikuwa ya kwangu tena bali ilikuwa ni ya mwakibubu.
Mwakibubu aliichukua ile simu na kuipokea huku akitoka nje akiniacha mimi nikimtazama bila kujua nini kinaendelea muda huo na imekuaje ile namba mpya inamjua mwakibubu na kajuaje ninakuja kumfuta mwakibubu?????
Kwa kweli nilizidi kuumia ila moyoni nikaona nina unafuu kwani tupo wawili sasa ambao tunatafutwa na kitu tusichokijua na kama wasemavyo wahenga kifo cha wengi ni sherehe.
Wakati naendelea kutafakari mwakibubu alirudi akiwa anahema na hakuongea kitu zaidi ya kuchukua begi lake la laptop na kuondoka kwa kasi ya ajabu.
Pamoja na kumfuata huku nikimwita hakugeuka na akaingia kwenye gari lake na kutoka mbio akiniachia vumbi pale.
Vumbi lile lilinisababishia kikohozi kizito ambacho kilisindikizwa na kicheko nikijiuliza nini kimetokea na kapewa maelezo gani yaliyomfanya aondoke spidi kama kafumaniwa. Nilitazama kushoto na kulia kujua labda alikimbizwa lakini hakukuwa na chochote zaidi ya bango la Gracious House of Cakes.
Nikarudi na kuonana na Manca ambaye ni meneja wa pale na kumuuliza tunadaiwa kiasi gani ingawa swali kubwa aliloniuliza ni yapi yamemsibu bwana mwakibubu.Sikumjibu lolote zaidi ya kumjibu kwa tabasamu la kuonyesha hakuna baya lolote lililotokea na kisha nikamlipa na kuondoka.
Nikiwa njiani nilipokea simu ya mwakibubu akiongea kwa jazba, " Tusionane tena wewe fala mpuuzi, unajua umenihamishia matatizo yako???? Napigiwa simu napokea hiyo namba na huyo dada ananikaripia kama ana nidai vile yaani sitaki kuamini hili suala kabisa baba pachu na kasema kazi ndio inaanza, kwani una nini naye huo?"
Wakati nataka kumjibu bwana mwakibubu akakata simu na kunitumia meseji " Kaka nitakupigia simu baadae hapa nimebanwa na tumbo la kuhara"Nilicheka sana mpaka nikasahau kama na mimi ni mhanga wa ile simu lakini kwa mwakibubu nikaona kali ya mwaka.
Nilifika nyumbani na kweli siku hiyo nikajisikia angalau nina unafuu hivyo nikaingia kuoga na kisha nikamwambia mama pachu aniandalie chakula nikawa naendelea kuperuzi peruzi kwenye blog ya tabasamu na fuledi ili kidogo nicheke na kusahau mikasa ya siku hiyo.
**********************************************************************************************
Nyumbani kwa mwakibubu
**********************************************************************************************
Mwakibubu akiwa chumbani kwake kajifunika gubigubi na hataki hata kusikia sauti ya mtu huku akitetemeka ghafla simu iliita kwa bahati mbaya mwakibubu familia yake ilikuwa imesafiri na kumfanya abaki peke yake mle ndani.
Ila safari hii mwakibubu alipokea simu kutoka na bila kutazama jina mwakibubu alianza kufoka, " Ukome, Uniache , Mfuate huyo huyo baba pachu mimi huniwezi na sio mrahisi hivyo"
Mara sauti ya mke wake ikamshtua, Baba Amigo!!!! Baba Amigo!!!! Baba Amigo!!!! unamwambia nani maneno hayo?
Yaani mimi niende kwa shemeji baba pachu?
Mwakibubu akamjibu mke wake kuwa " mama amigo nakutania tu nilkuwa nafanya maigizo ili ujue na mimi ninakipaji, hebu nipe maksi zangu hapo"
Ila moyoni nikajua nimebugi, basi mama amigo alinielewa na kunipa maski 90 nilijichekesha ila moyoni nikahisi sio muda nitakuwa kichaa. Tuliongea kwa muda na mama amigo alikuwa akinisalimia na kunitaarifu kuwa wamefika salama na watachelewa kurudi kwani mavuno yameanza.
Habari ya kuchelewa kwao kurudi ikanistua na kuanza kuona nyumba yangu itageuka na kuwa sehemu ya maigizo ya filamu za kutisha kila kukicha.
Kesho yake asubuhi nilijiandaa na kuelekea kazini wakati nipo njiani meseji ikaingia iliyosema, " Kaka umelalaje?" sikujibu kwa hasira nikajua ni baba pachu aliyeniletea kesi na kujifanya kunijulia hali, nikaendelea na safari kwenda kazini.
Nilipofika kazini secretary aliniletea kinoti kalichokuwa na ujumbe ndani yake ulionitaka ...................................................................................................................................
JE ni ujumbe gani huo na nini hatma ya mwakibubu katika sakata hili? Je wana ubia gani na baba pachu? Usikosde kisa hiki kesho jioni
Unaweza kuwa mdhamini wa kisa hiki cha kusisimu na chenye funzo kubwa kwa vijana wa sasa katika masuala ya mapenzi.
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu kwa udhamini wa Gracious HOUSE of CAKES watengenezaji maarufu na waliobobea wa keki za aina mbalimbali kwa hafla mbalimbali waliopo jijini Mbeya na wanapatikana kwa namba 0767218014
Nawe waweza kuwa mdhamini wa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo
share, like na comment
UTAJIRI AU FEDHA ZA NDAGU AU MAJINI KWA MUDA MFUPI
ReplyDelete(Kwanza kabisa nataka kukwambia kwamba hakika utajili ni azina kutoka kwa mwenyezi mungu na pia kuna viumbe alio wapa mamlaka na nguvu ya kumiliki mali)
MPAKA MASAA 72(SIKU3) PAPO HAPO KWA MASHARTI MAALUM KIKUBWA UWE MWAMINIFU, JASILI NA UWE NA UTAYARI WA KUPOKEA MASHARTI YA KUTUNZA SIRI HII SIO MZAHA......
KUMBUKA MALIPO NI BAADA YA KUFANIKIWA
kwa maelezo kamili piga namba +255742162843
(KWANINI USUMBUKE,HACHA KUTANGATANGA, NA MAISHA NI MAFUPI PUUZA UONGOFU WA KUWA MTU KUWA TAJIRI NI DHAMBI WAKATI AKUAMBIAE YEYE NI TAJIRI (Tumia ufahamu kujinasuaUTAJIRI WA NDAGU(MASHARTI) NDANI YA MASAA 72(SIKU TATU) PAPO HAPO KIKUBWA UWE MWAMINIFU, JASILI NA UWE NA UTAYARI WA KUPOKEA MASHARTI YA KUTUNZA SIRI HII SIO MZAHA......
NAITWA DR, MDIRO piga 0742162843. KAMA UNAITAJI PESA ZA MAJINI AU NDAGU YA MALI AU ULINZI KWA MALI YAKO
(HUSITUME SMS PIGA SIMU KUHEPUKA MATAPELI)
MATIBABU MENGINEYO NI KAMA UTULIVU KATIKA NDOA, AU KUMVUTA UMPENDAE, KUONDOA MIKOSI, MABALAA, KUOSHA NYOTA, KUITAMBUA NYOTA YAKO NA ASILI YA KAZI YAKE, KAMA UNASUMBULIWA NA MAJINI MAHABA NA SHIDA YA UZAZI.
NIPIGIE 0742162843. KIKUBWA NI KUSIKILIZA NA KUFATA MASHARTI. ANGALIZO USITUME SMS PIGA NA UWE NA NIA.
(kuhusu utajiri au pesa) KABLA YA KUPIGA SIMU ZINGATIA YAFUATAYO
1. uwe una umri wa miaka 18+
2. uwe tayari kupokea masharti yote
3.uwe na uwezo wa kutunza siri
4. uwe jasiri wa kupokea taarifa yoyote
KARIBU SANA KWA SHIDA NYINGINE PIA ULIYONAYO AMBAYO SIJATAJA INSHAALAH ITATATULIWA IKIWA NDANI YA UWEZO WANGU.
ingependeza zaidi ikawa kwa njia ya sauti
ReplyDeletemm inashia sehemu ya 16
Deleteumepata mwendelezo wake