RIWAYA: MKONO WA JASUSI - 01

15:23:00 Unknown 3 Comments


01

DAR ES SALAAM – Miezi Sita ilopita…

“KAMANDA Amata,” sauti iliita kutoka nyuma yake. Akageuka na kumwona Madam S akiwa na faili moja mkononi. Alikuwa amesimama katika sehemu ya mbele ya nyumba kubwa huko Gezaulole, mkono wake ukiwa na bandeji kubwa. Akageuka na kumtazama Madam S.
“Yes Mom,” akaitikia na kuitoa miwani yake usoni.
“Mheshimiwa Rais anakupongeza kwa kazi ulioifanya, anakubali sana uwepo wako hapa nchini na hususan katika idara nyeti kama hii, nimetoka kuzungumza naye sasa hivi, tumekubaliana jambo moja,” akamkabidhi lile faili ambalo juu yake lilikuwa limeandikwa Rhobinson Quebec na chini yake maandishi mazito ‘Wanted’, akatalizama na kumwangalia Madam S.
“Roho yake tu wala hatumwitaji akiwa hai,” kisha akageuka na kuondoka.
T.S.A MAKAO MAKUU – 1999
“Unakunywa chai au kahawa?” Gina alimuuliza swali Amata aliyekuwa ametingwa, macho kodo kompyutani akiperuzi hiki na kile.
“Swali lako hilohilo kila siku, na jibu langu lilelile kila mara,” akamjibu na wote wakacheka kwa sauti.
“Nyie kuna nini huko?” Madam S aliuliza akiwa tayari kasimama mlangoni.
Wote wakasimama kumpa heshima yake, “Karibu Madam, umeingia kama kivuli!” Kamanda akatania.
“Hata kivuli huonekana, sema kama hewa!” akajibu kisha wote wakacheka tena, “Kamanda Amata, uje ofisini baada ya mambo yako kuna jambo nikueleze na ulifanyie kazi,” akaondoka. Amata akamtazama Gina kisha wakaendelea na vicheko vyao na mabishano ya chain a kahawa.
“Madam anakuita ofisi, kuna kazi au?” Gina akaanza uchokozi.
“Hapana, kungekuwa na kazi angenikurupusha na ninyi nyote mngekuwa katka hekaheka ya kupanga kazi hiyo, itakuwa anataka kuniuliza kama nakuoa au la,” Amata akajibu.
“Mmmmmhh! Hiyo ndoa ya mi na wewe itakuwa ndoano,” Gina akaendeleza mazungumzo na kumpa Amata kikombe cha Kahawa.
Mbele ya kompyuta hiyo, Amata alikuwa ametingwa bila kuongea na mtu yeyote, hakuna aliyejua ni nini anakitafuta isipokuwa ni yeye peke yake. Alipokuja kumaliza kazi yake na kuinua macho alijikuta peke yake na kahawa iliyopoa mezani. Akainua walkie talk yake na kuita.
“We, njoo huku, tupo kwenye chumba namba tano,” Gina akamwita Amata hata kabla hajaambiwa lolote.
§§§§§
Ndani ya chumba hicho kulikuwa na watu wane, Madam S, Gina, Jasmine na Amata, waliketi wakitazama moja ya muvi nzito ya kipelelezi ambayo kwa roho yako nyepesi huwezi kuitazama mara mbili. Kwao muvi hiyo iliwafunza mengi sana hasa katika ukachero wa ndani na nje.
Ilikuwa ikionesha hatua thelathini na tisa za Kijasusi, kila mmoja alikuwa katulia kimya akifuatilia muvi hiyo ambayo kwayo ilikuwa na mafunzo mengi sana. Ilipomalizika baada ya dakika tisini, kila mtu alishusha pumzi ndefu na kumtazama Madam S aliyekuwa ameketi kimya mkono wake ukiwa umekuwa egemeo la kidevu chake. Akainuka akawatazama wote.
“Nakaribia kustahafu mama yenu, umri umenitupa mkono, kaeni tayari kwa lolote kutoka sasa. Kamanda njoo ofisini,”
Amata akainuka na kumfuata Madam S mpaka ofini kwake, ofisi pana yenye nafasi ya kutosha, ilikuwa na viti sita vya vono safi, meza kubwa ya mpingo iliyochongwa na vijana wa Suma J.K.T ilipendezesha ofisi hiyo. Ukutani kulining’inizwa picha kubwa ya Hayati Baba wa Taifa, na pembeni sana kulikuwa na picha ya mtu mmoja mwenye macho angavu yaliyoonekana kujua mambo mengi sana. Ukiitazama picha hiyo unaweza kuiuliza swali lakini ilikuwa picha. Kamanda Amata ijapokuwa alikuwa ni T.S.A 1 lakini bado katika ofisi hii aliingia mara chache sana. Picha iliyokuwa hapo ilimkumbusha Mogadishu alipokutana na mtu huyo The Chamelleon, alitamani kumwambia Madam S juu ya hilo lakini bado agano lake na marehemu bandia huyo lilikuwa ni kutunza siri.
Madam S akazunguka nyuma ya meza hiyo, akasimama mbele ya bendera kubwa ya taifa iliyokuwa kulia kwake na kushoto kwake kulikua na nembo kubwa ya T.S.A, nembo iliyobeba ngao ya Taifa na kunakshiwa kwa dhahabu safi kwenye kingo yake, juu yake kulitokeza kichwa cha Twiga ambacho kilitanguliwa na barafu ya mlima Kilimanjaro. Chini kabi say a nembo hiyo herufi tatu yaani T.S.A zilibebwa ju ya mikuki miwili iliyofanya alama ya X.
“Saa kumi jioni ya leo, kuna kikao nyeti Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, nitakwenda pale, lakini nataka nionane na wewe mara tu nikitoka, kama kuna lolote tofauti nitakushtua, uwe tayari muda wote,” Madam akamwambia akiwa amesimama wima.
“Yes! Madam, daima nipo tayari,”
“Kuna kazi kubwa Amata, ngumu sana mbele yako, itakayoweka maisha yako rehani kuliko siku zote, lakini huna budi kuifanya, nasi tutakuwa bega kwa bega na wewe,”
“Yes, Madam,” akajibu kwa ukakamavu.
“Sasa nakwenda kuonana na Mheshimiwa Waziri kisha nitakuita kiofisi ili tuone tunafanya nini katika hili, kwa maana hata mimi bado sijui ila nimedokezeaa tu juu yake,” Madam alimaliza maelezo yake.
§§§§§
Jioni ya siku hiyo ilimkuta kamanda Amata D.D.C Kariakoo akipata moja mbili baridi, akili yake ilizunguka kama pia, alijikuta akishikwa na donge kubwa la kujua nini kinataka kujiri katika ofisi yao. Alikwishazoea kuwa kazi zote huwa anaambiwa moja kwa moja na Madam S na kuianza muda huohuo lakini alishangaa kwa sasa Madam S anampa dokezo na kumwambia nitakuita baadae.
Bia ilishuka taratibu lakini haikuleta matata yoyote katika ubongo wa kijana huyo, ilishuka kama maji na kumtaka kwenda haja ndogo mara kadhaa. Muziki wa Kitanzania uliokuwa ukiporomoshwa na bendi ya Msondo ulimfanya japo kupoteza mawazo yake kwa nukta tu na si sekunde. Aliburudika kwa kuimba kidogo lakini mawazo yaliporudi katika lile analolisubiri kwa hamu. Aliitazama saa yake tayari ilitimu saa kumi na moja na nusu jioni, jua lilikuwa limeuacha mji na ukiliangalia lilichwea katika milima ya Pugu. Akanyanyuka na kupenya katikati ya watu, moja kwa moja akatoke kwenye lango la kutokea nje, akateremka ngazi na kuliendea gari lake aliloliegesha jirani kabisa na duka la Mhindi.
Alipoketi tu kitini simu yake ikaita, akainyanyua na kuichungulia, Chiba, akaifyatua na kuiweka sikioni.
“Vipi kijana, likizo imeisha?”
“Aaa ofisi zetu hazina likizo, dili likitokea popote na muda wowote unajiongeza man,” Chiba akajibu.
“Niambie!”
“Vipi hali ya hewa hapo ulipo?” Chiba akauliza.
“Pako shwari nimejificha kibandani, nyunyiza tu,” Kamanda akamwambia.
“Kaka kuna nini huko? Maana Madam kanambi nirudi, hapa nilipo tayari niko Uwanja wa Ndege wa Mauritius narudi,” Chiba akaeleza.
“Aaah! Huyu bibi naona anazeeka sasa, mi mwenyewe kanambia nisubiri ataniita,” Kamanda akamjuza.
“Ok, saa nne zijazo nitakuwa Dar kaka,”
“Na motto wa Ki-Mauritius?” Kamanda akatania.
“Hapana, mwenyewe tu, hayo nayaacha hukuhuku, over!” Chiba alimaliza kuongea, kwa kusema neno hilo over alimaanisha maongezi yasiendelee.
“Tuonane Ruvuma mpaka Maputo dakika 500 zijazo, over!” Kamanda akakata simu na kurudisha mahala pake, kisha taratibu akaingiaza barabarani na kuondoka eneo hilo. Daima hakupenda kukaa eneo moja kwa muda mrefu. Alaiingia barabara ya Msimbazi na kuelekea Faya, pale akakunja kulia kufuata barabara ya Morogoro mpaka karibu na Chuo cha Ufundi cha Dar es salaam akakunja kushoto akachukua barabara ya vumbi ya Ally Khan, akapita Zanaki na kuendelea mpaka mgahawa wa Red Carpet, akaegesha gari yake nje na kuteremka, akaangaza macho huku na kule kisha akaufunga mlango huku funguo ya gari akiwa kaiacha ndani.
§§§§§
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
“Madam S,” Mheshimiwa Francis Kifaru aliita kwa sauti yake nzito iliyoelemewa na unene uliopita kiasi. Daima alikuwa akiketi kama anayesinzia kutokana na umri uliopitiliza. “Wazee kama hawa wastahafu tu, wanang’ang’ania madaraka mpaka wafie maofisini, ndio maana nch haiendelei” Madam aliwaza.
“Ndio Mheshimiwa,” akaitika.
“Kama nilivyokuambia, hilo na hao jamaa wametuomba kuwasaidia na si kama tuwaombavyo basi ni zamu yetu, naamini idara yako itafanya vizuri,” Yule Mzee alitoa maelekezo na kumpa Madam S kabrasha lenye karatasi kadhaa ndani yake juu likiwa na maandishi Siri Nzito, akalitazama haraka haraka na kuliweka vyema.
“Ok, kazi imefika mahala pake na itatekelezwa,” akajibu na kumuaga mzee huyo, kisha akatoka nje.
Alipoketi garini, akatulia kwanza, “safi sana, sasa kazi ni moja tu, nilikuwa namuwaza sana mshenzi huyu” Madam S akajiwazia huku akiondosha gari yake maegeshoni.
§§§§§
Musanda, Pretoria - a.kusini
DUMISAN SAJAK MBEKHI, kiongozi mkuu wa Idara ya Kijasusui ya Afrika ya Kusini (N.I.A) alitulia tuli kama aliyegandishwa na barafu katika meza yake kubwa hapo ofisini. Giza lilikuwa tayari limeutawala mji huo wa Pretoria mju wenye amani na utulivu katika miji ya Afrika ya Kusini.
Akiwa bado katika fikra nzito, mlango wa ofisi yake ulisukumwa, na mwanadada mwenye mwili wa kati, sio mrefu sio mfupi aliingia akiwa katika mavazi ya kijeshi, aliposimama mbele ya mwenyeji wake, huku wakitenganisha na ile meza kubwa, aliiachua kofia yake mabegani na kuivaa kichwani pake kisha akasimama kiukakamavu.
Dumisan akasimama akionekana wazi amefura kwa hasira na kisasi.
“Debra, sina haja ya kupoteza muda, nimekuteua wewe kwa kuwa najua wasifu wako jeshini, unapaswa kuondoka usiku huu na ndege ya Uingereza, uende Canada pale kuna mtu unatakiwa ukaitoe roho yake kisha urudi mara moja. Nataka ukamuue na si vinginevyo, nategemea majibu mazuri kutoka kwako, asante.” Dumisan akaketi. Debra akapiga saluti na kutoka katika ofisi ile, hakutakiwa kujibu lolote kwani hiyo ni amri alichotakiwa kufanya ni kutekeleza aliloambiwa tu basi.


2
MIEZI MIWILI ILIYOPITA
ILIKUWA HALI YA SINTOFAHAMU katika machimbo ya dhahabu huko Mashariki mwa Johanesburg, Afrika ya kusini. Katika moja ya mashimo makubwa ya tajiri maarufu, Khumalo, wafanyakazi takribani kumi na tano waliokuwa wakifanya kazi kwa ukaribu sana na mtu huyo aliyeuawa miaka kadhaa nyuma nao waliuawa na maiti zao kukutwa ndani ya mashimo hayo.
Machimbo ya dhahabu ya The Great Khumalo yalifungwa kwa muda ili kupisha uchunguzi wa mauaji hayo yaliyotokea ndani ya siku moja lakini haikujulikana ni nani hasa aliyeyatekeleza hayo.


ITAENDELEA !



You Might Also Like

3 comments:

  1. Habari zenu. Ilikuwa ngumu sana kwangu wakati mpenzi wangu aliniacha kwa mwanamke mwingine. Niliharibiwa kihisia, nilivunjika moyo na sikujua la kufanya ili kumrudisha. Nilihangaika kwa miezi mingi na niliendelea kutafuta msaada kutoka kila mahali hadi nilipopata kujua kuhusu DR DAWN. Niliwasiliana naye na kumweleza shida zangu. Alikuwa tayari kunisaidia na kunisisitiza nifuate taratibu ili aweze kurejesha penzi kati yangu na mtu wangu na pia kuhakikisha tunarudiana wote wawili. Nilipata mahitaji yote na ilifanya kazi hiyo. Baada ya saa 48, nilipata ujumbe kutoka kwa mpenzi wangu akiniuliza tarehe. Sasa tuko pamoja tena na shukrani zote kwa DR DAWN. Anaweza kukusaidia kumrudisha mpenzi wako,
    Anaweza kukusaidia na uchawi wa ujauzito,

    Anaweza kukusaidia kuponya aina yoyote ya ugonjwa.

    ikiwa uko tayari kuamini na kubaki na matumaini. Watumie barua pepe tu kupitia: dawnacuna314@gmail.com
    WhatsApp: +2349046229159

    ReplyDelete
  2. Halo watu wote, jina langu ni Marvelyn Larry. Kwa muda mrefu, mume wangu alikuwa akiishi katika ghorofa nyingine kutokana na shinikizo la kazi na tulifurahi sana pamoja ingawa alikaa mbali nasi kwa miezi kadhaa. Sikujua mwenzangu wa kazi tayari alikuwa na uhusiano naye jambo ambalo lilimfanya mume wangu anipe talaka bila kutarajia. Nilijua kuna kitu kibaya kwa sababu hatukuwahi kupigana au kubishana kiasi hicho ili kumfanya aondoke. Nilikuwa na kiwewe na natafuta msaada wa kukabiliana na hali hiyo iliyonipeleka kwa DR DAWN kutokana na sifa walizomwagiwa na watu mtandaoni. Tulizungumza kwa kirefu na aliniambia kila kitu nilichohitaji kujua kuhusu kile kilichotokea na utaratibu unaofaa wa kurekebisha matatizo. Alitimiza ahadi zake na kumrudisha mume wangu kwangu na mchakato wa talaka ukafutwa. Sasa mume wangu amerudi nyumbani kwetu na tuna furaha pamoja. Inashangaza sana jinsi watu wanaweza kusaidia watu wengine wakati wanahitaji. Anaweza kukusaidia pia. Mtumie tu ujumbe kupitia WhatsApp: +2349046229159
    Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com

    ReplyDelete