HADITHI YA KWELI NA YA KUHUZUNISHA JINSI NILIVYOBAMBIKWA MKE NA BABA MKWE KATILI ZAIDI DUNIANI
Mara yangu kumwona binti huyu ilikuwa ni jumamosi moja nikiwa mtaani kwetu nje ya duka moja la jumla la kuuzia filamu zinazosambazwa na kampuni ya Smart Ideas Communications.
Nilivutiwa na jinsi alivyokuwa mbichi mbichi, pia msafi na mwenye kuonekana kama ni binti ayajuaye maisha na mwenye uelewa wa maisha na mstaarabu pia tofauti na mabinti wetu wa pale mtaani.
Nasema tofauti na mabinti wa mtaani kwani wao ilikuwa pamoja na kuwasifia kwa uongo kuwa ni wazuri ila kwao salamu au hata kuongea nasi vijana wenzao ilikuwa ni mwiko na pengine unaweza kuambulia matusi zaidi ya yale uyasomayo kwenye baadhi ya page za facebook.
Nakumbuka kipindi hicho ndio nilikuwa nimefauli mtihani wangu wa kidato cha sita na nikawa nimepewa zawadi ya simu moja matata sana iliyonipa uwezo wa kuingia facebook na kumia mitandao mingine
Nilimuuliza jina lake akaniambia anaitwa Linda Fred na ni mgeni mtaa huo baba yake kahamishiwa pale kikazi na yeye anasoma kidato cha tano katika shule moja ya wasichana iliyopo mikoa ya kusini mwa Tanzania.
Tukajikuta tukiwa marafiki na mara kwa mara tukawa tukiwa pamoja nikimsindikiza library kusoma, mara kanisani na kuna wakati alipenda sana filamu hivyo nikaanza nami kupenda kwenda kutazama filamu katika kumbi mbalimbali za filamu alizozipenda.
Mpaka inafika siku ya kurudi shule ili sasa aende kuuanza mwaka wa mwisho yaani kidato cha sita tayari tulikuwa wapenzi na mambo yetu yale tulishafanya zaidi ya mara nne na kiukweli wote tukawa tumemezwa katika dimwi la mahaba pamoja na familia yangu kunikataza ila nikafunga masikio.
Pamoja na kuwa shule yake haikuwa na simu ila tulizidi kuwasiliana sana kwani kila weekend alinipigia na tuliongea nae kwa furaha na kufarijiana sana nami wakati huo michakato ya kwenda chuo ikianaa kwa mimi kutuma maombi vyuo mbalimbali vya nje na ndani ya nchi.
Jumatatu moja katika hali isiyoyakawaida nilipigiwa simu ya Linda na kuniambia kuwa alikuwa amelazwa akisumbuliwa na homa, nikamfariji kuwa atapona na nikaendelea kuwasiliana nae.
Siku chache baadae mawasiliano yakapotea na nikaaa zaidi ya wiki mbili bila kujua nini chendelea na sikuwa na uwezo mwingine wakupata taarifa. siku mbili baadae nilipokea ujumbe kutoka namba ile ile ya linda kuwa Mpenzi ukiweza kimbia usiku huu.
Kwa hofu na mshangao nikaanza kuipiga ile namba haikupokelewa na kisha kuzimwa kabisa... mkojo ukanibana na haja kubwa ile ya hofu ikanibidi nitoke na kwenda vyoo vya nje.
Nikiwa pale nje nikaona mwanga kuashiria kwa mbali kuna gari linakuja uelekeo wa nyumba yetu. Akili ya haraka ikaniambia nipande juu ya mti mmoja mkubwa uliokuwa ukileta kivuli pale kwetu ili kuona kuna nini.
Gari lilisimama pale na wa kwanza kushuka alikuwa ni Linda akiwa na baba mmoja aliyeonekana kashiba kimazoezi na kwa haraka nikamtambua kuwa ni baba wa linda tu. wakagonga mlango na baba na mama wakafungua na yule mzee hakusema neno zaidi ya kusema nina shida na mtoto wenu tu yuko wapi???
Baba akamuuliza, mzeee mwenzangu kuna tatizo gani? baba yake linda akasema nina shida na mtoto wenu tu ndio mtajua nini shida iliyonifikisha hapa. baba akamwambia mama aende chumbani aniite lakini bahati mbaya wakasema hayupo ila alikuwepo humu ndani muda sio mrefu.
Baba yake linda akampiga vibao linda na kusema wewe mpuuzi umemwambia kuwa tunakuja??? kisha akawageukiwa baba na mama akawaambia kuwa mwambieni nitarudi na hana pa kujificha wala kukimbilia kisha akawasha gari na kuondoka.
Mama na baba wakakaa pale kwa dakika kadhaa wakibishana kuwa inaweza kuwa nimempa mimba au kuna mchezo gani na je nimekimbia ua nilijua wataku?? Nikahakikisha wamengia ndani nikashuka taratibu nikanyata mpaka dirishani nikamgongea dogo akanipa koti na suruali yangu na waleti na kibegi kidogo na moja kwa moja nikaondoka.
Niliondoka nikiwa sijui naenda wapi lakini nikawa najipa matumani kuwa nitapata sehemu ya kulala na mfukoni nilikuwa na shilingi elfu 33,000/- nikaingia hoteli moja na kulala kisha saa kumi na mbili nikakimbia na kwenda stendi nikakata tiketi ya kwenda chombe bila kujua naenda kwa nani.
Muda huo simu zote zimezima na nina kadi ya mama ya bank ambayo aliifungua ili tuweze kuwa tunaweka fedha za mradi wetu wa kuku wa mayai pale yumbani na kwenye akaunti kulikuwa na zaidi ya milioni moja hivyo nikasema mtaani nakimbia.
Jioni yake nikiwa njombe nikakawa tayari nimempigia jamaa mmoja ambaye mdogo wake nilisoma naye na akawa amenipokea na kunikaribisha na kisha kuniweka nyumbani naye akaendela na kazi zake nami nikatumia mwanya huo kumpigia Rafiki yangu mmoja ambaye nilipompigia tu simu nilishangazwa kusikia akilia na akanza kunilaumu sasa ona ulichotufanyia umempa mimba Linda baba yake katuchapa leo na hapa nipo nyumbani kwake kasema sitoki mpaka wewe uje.
Muda huo huo zikaingia zaidi ya sms 40 kutoka kwa baba, mama na baadhi ya ndugu wengine wakisema usirudi na wengine umefanya nini sasa? Nikampigia mama na kumuuliza mambo yakoje maana mama alinipenda sana, akasema kuwa Linda kafukuzwa shule kwa kuwa ni mjamzito na baba yake ni mwanajeshi na mwenye cheo kikubwa sana na kasema atanisaka na pia yeye hataki mtu yoyote zaidi ya mimi tu.
Pia akaongeza kuwa baba amejaribu hata kuchukua baadhi wazee ili waende kuyaweka mambo sawa ila wameshindwa na baba kachukia ananitafuta. Nikamwambia mama sasa nitakutafuta mimi tu. Nikazima simu zote na kuvunja zile laini na kununua laini mpya ya simu na kisha muda wa kulala ukawa umefika nikalala.
Asubuhi nikaendelea kumsaidia kaka yangu pale na nilifanikiwa kukaa pale kwa wiki zima bila kumpigia mtu simu, kuingia facebook wala kumpa mtu namba yangu lakini maajabu ya yule baba wa linda alinipigia kwenye simu yangu.... akiniambia kuwa nisifikiri njombe nimejificha nirudi au muda muafaka atanidaka..Nilitetemeka pamoja na ile baridi ya njombe nikajihisi nina joto.
Nilikuja kugundua sijavaa shati nikiwa nakaribia Mbeya baada ya konda kudai akague risiti nikajipapasa nikijua iko kwenye shati kumbe sio shati... Nilifika mbeya na kulala hoteli kisha nikampigia simu mama baada ya kutowasiliana naye kwa muda wa wiki, akaniambia ni bora nibaki hukuhuku kwani kule baba naye kachoka anataka kunitafuta sasa wasije nichinja bure nami nikatumia mwanya huo kumwambia nina kadi yake ya benki akasema nitulie kwanza.
Nilishakaa mbeya zaidi ya mwezi na sijawahi wasiliana na linda na hata hamu ya kumwona imesisha wala hakuna mtu wa familia zaidi ya mama aliyejua na sasa ilimbidi amshirikishe baba maana baba alipigiwa simu na baba linda kuwa hata wakiniweka mbeya bado sijakimbia matatizo zaidi nitapoteza fedha kwa mchezo wa kujificha huku naonekana na yeye anajua nyendo zangu zote.
Baba na mama kwa siri wakanipigia simu na kusema kwa hali ile siwezei tena kuwa salama wakanitumia nauli na kuniamba nipande basi tukutane Arusha maana hata baba naye sasa alichoshwa maana katumia jitihada za usuluhishi bila ya mafanikio na mzee akinitaka mimi tuu.
Nilifika arusha usiku na kulala pale asubuhi naiwasha simu ikaingia sms kutoka kwa baba linda akisema karibu arusha usije fikiri kama hapa umejificha sana .
Tumbo la kuhara likanianza na muda mama na baba wanaingia nilishakuwa mdogo nikasema hapa sasa naweza kufa muda wowote au mzee ana wapelelezi wake????????
Baba na mama wakakaa na mimi na tukaenda mpaka kijiji kimoja karibu na loriondo kuna mzee akasema yeye anadawa ya vijiko yaani vijiko viwili tuu sitaonekana tena na baba linda na wala hatajua nipo wapi.
Nikanywaa dawa ile na kimila na siku ya pili tukaanza safari ya kurudi dar ili niendelee na michakato ya kujiunga na chuo kwani sasa ile dozi ya vijiko isingemruhusu baba linda anione tena.
Nililala sana tulipokuwa kukikaribia mrogoro nilipokea ujumbe kutoka kwa baba yake linda akisema karibu sana naona sasa uko morogoro......... Nikamwambia baba simamisha gari maana tulikuwa na usafiri binafsi nikawaonyesha sms wote tukaduwaa na nikasema mimi sijipeleki dar kwa mtindo huu wataniua kabisa na yule mganga na vijiko vyake ni feki
Baada na mabishano marefu wakakubali nibaki pale kwa shangazi yangu nami nikaa pale ila siku ya pili nikiwa na ujasiri ambao sijawahi kuupata niliondoka na kwenda mpaka dar na nilipofika mida ya saa nne hiyo jumamosi nikamwomba baba na mama na baba yangu mkubwa na mdogo twende nyumbani kwa baba linda.
Tulikaribishwa pale nyumbani na kupelekwa chumba kimoja tukakaa wakati huo mimi nilishasali zaidi ya mara saba na kutaja majina ya Mungu kwa zaidi ya kugha kumi na zaidi huku nikisema basi kama nitapigwa risasi au kukuwekwa lupango basi sitakwepa kamwe.
Alikuja baba linda baada ya dakika kama tatu akiwa na uso wa furaha tofauti na nilivyofikiria akamwita linda na kumweka pale ndani na kuuliza swali moja "Linda huyu ndiye mwenye mimba yako?" Linda akajibu ndiyo.
Kisha aksema wazazi wenzangu mnisamehe kwa jinsi nilivyofanya nilitaka kumpata huyu kijana ili nijue na kusia kwa masikio yangu nanyi msikie pia wao wana mpango gani baada ya kupeana mimba?... wazazi wakawa wameduaa na baba mdogo nikaona sasa anajilaumu kwa nini alichukua kisu na kukificha kama kungezuka ugomvi.
Mimi na Linda kwa pamoja tukasema sisi tunapendana na tulishapanga hata chuo tusome chuo kimoja... na kuanza maisha yetu... mzee akasema sasa mimi sitaki mahari nasikia wewe unategemea kujiunga na chuo? kama ndio wewe na familia yako mtasaidiana na sisi kumtunza hapa na pia baada ya miezi mitatu atatakiwa kuanza mpango wa kurudia masomo yake ili naye aje kuanza chuo mapema.
Tulifanya hivyo nami nikafanikiwa kuanza chuo nikiwa mwaka wa tatu Linda alikuwa mwaka wa kwanza na sasa ni zaidi ya miaka mitatu tangu tuoane na Linda na juzi nimepata baahati ya kukaa na baba mkwe (baba Linda) nikamuuliza alikuwa anapate taarifa ya juu ya kila mahali nilipofika?
Jibu likanifanya nijione mpuuzi... Mimi na linda wote kwenye simu zetu tuliweka softiware moja ambayo kama tungebadili namba za siku au hata kufanya lolote tungepata sms ya sehemu ambako mtu huyo yupo na kwa msaada wa network ingeonyesha na location na namba mya iliyowekwa kwenye simu... hivyo mzee kwa kuwa aliinyang'anya simu ya linda basi alipata taarifa zangu kila nilipobadili laini....
Kila nikikumbuka kisa hiki huwa naishia kusema kila mtu ana kibonde wake.
Kisha waweza pitia HAPA na kunipa maoni yako
Duuu mbona kichwa cha hadithi hakisadifu yaliyomo
ReplyDelete