Naomba ushauri wenu marafiki
Hello Fuledi,
Naitwa Lucy na ninasoma chuo fulani hapa nchini.
Wazazi wangu wote wawili walifariki na ajali ya basi wakiwa wanatoka dar kwenda arusha mwaka jana. Baada ya hapo nilichukuliwa na mjomba angu ambaye anaishi na familia yake ya mke m1 na watoto wa2.
Mjomba aliubeba mzigo wa kunilea na kunisomesha kama mwanae kwa kunilipia kila kitu chuoni na kunipatia ninachohitaji kama bado nipo na wazazi wangu. Ni miezi mitano mpaka sasa toka mjomba anichukue baada ya wazazi wangu kufariki.
Siku moja nilikuwa nimelala chumbani kwangu wakati wa ucku nikasikia kuna mtu anabisha hodi huku ananiita jina langu nilikuwa ni muoga sana kuitika,nilitega masikio na kugundua kuwa alikuwa ni mjomba. Mjomba alianza kujivunjia heshima na kunitamani kimapenzi wakati mkewe yupo kwao amekwenda kujifungua.
Hali ile ckuipendelea hata kidogo kwani kila cku nilijifanya nimelala kwani nilijua nikifungua hapatatosha chumbani kwangu. Juzi nilienda chooni kuoga wakati wa ucku kumbe huku nyuma mjomba aliingia chumbani kwangu,nilitoka kuoga na kuingia chumbani kwangu cna hili wala lile kama mjomba yupo chumbani.
Niliitoa kanga iliopo kifuani mwangu na kubaki kama nilivyozaliwa na kuanza kupaka lotion mwilini. Nilimaliza nikachukua bikini na kuvaa ghafla nilivamiwa na kuangushwa kitandani na mjomba nae kuniminya mikono kutaka kunibaka . Nilikuwa mbishi sana mpaka nikafanikiwa kumsukuma mjomba akaanguka chini.
Mjomba alipokuja mara ya pili kwa pupa nilimtegeshea kigoti na kukiangukia katika sehemu zake za siri. Hakika alilala pale chini na kuanza kugaragara kama mtoto.
Akili ilinituma nikachua kanga na kuvaa haraka nikatoka nje kukimbia moja kwa moja kwa rafiki yangu ambaye mpaka sasa amenistiri kwao. . .
Kichwa kinaniuma nikifikiria kuhusu maisha yangu yatakuwaje kwani tegemezi langu nalo limekuwa na kigeugeu kwa tamaa za kimwili. Sijui pia masomo mwishilio wake kwani naumia sana moyöni mwangu. . .
Nikifikiria kurudi kwa mjomba roho inasita kwa kitendo alichotaka kunifanya. . .
Jamani naombeni ushauri wenu kwani hapa nimechanganyikiwa sana. . .

0 comments: