Punda wee

13:20:00 Unknown 0 Comments



Siku moja punda alienda kwa SIMBA mfalme wa mbuga,kushitaki mashitaka jinsi wenzake wanavyomcheka,na kumwita PUNDA.

Jina hilo punda hakulipenda kabisa kwa kuwa wenzie humwambia kuwa jina hilo linawakilisha ujinga mwingi alionao, ndio maana anaitwa punda.

Mazungumnzo yao yalikuwa hivi:

SIMBA: ngoja nikupe mtihani mdogo wa kupima akili yako,kama kweli wewe ni mjanja na mwerevu...ukiushinda mtihani huunitakuita farasi.

PUNDA: nipime ujanja wangu na utanikuta mwerevu sana kuliko wenzangu.

SIMBA: nenda mbio home kwangu kaangalie kama nipo huko au sipo

PUNDA: kazi rahisi sana hiyo,nisubiri nitarudi sasa hivi.
basi punda akatoka mbio hadi nyumbani kwa mfalme..... aliporudi mambo yakawa hivi:

SIMBA:vipi umenikuta?

PUNDA:mh! haupo...sijakuona kule!

SIMBA: basi ndio hivyo utaendelea kuwa punda kutokana na akili yako kuwa ndogo,sasa umeenda kwangu kunitafuta vipi,wakati umeniacha hapa?..haya potea haraka hapa..punda we!...kuanzia leo jina lako litaendelea kubaki ivo ivo...............punda we!

You Might Also Like

0 comments: