Daaaah !!!! Mambo mengine bwana....

06:49:00 Unknown 0 Comments



Juzi nilipita pale Sinza darajani nikielekea home nikaona mfuko umetupwa, kuuangalia ndani nikakuta mil. 5 na vikoro koro kibao.... 

Niwe mkweli woga ulinishika nikaangalia kushoto na kulia nikaona watu hawanioni nikachukua ule mfuko na kwenda haraka home....

Nilipomwaga kila kitu nikakuta vitambulisho, kadi za ATM, makaratasi mengi na iPAD nilitaka kuzima simu nitoe sim kadi lakini nikaacha roho ikanisuta kuwa mwenye mali anaweza akanipigia!!!!

Na kweli baada ya muda si mrefu simu ililia kupokea ALIKUWA MMAMA FULANI na kwa maelezo ikawa wazi mali zile ni za aliyepiga... Nikamuelekeza niliko yule mmama fulani wa makamo akaja kuchukua mzigo wake na kila kitu lakini akanipa zile mil. 5 nichukue...

Nikakataa kistaarabu pamoja na kunikazimisha saaana, ila mwisho wa siku yule mama akachukua namba yangu ya simu akaondoka....

Jana akanipigia simu kuwa yuko nje ya nyumba yangu alikuwa kaja na RANGE SPORTS mpya... Akanipa ufunguo kanambia ni yangu na kuna nyumba kaninunulia MASAKI akanipa na brief case imejaa hela kwa ajili ya kufungulia biashara!!!!

Daah, kwa furaha bila kuamini nikaingia kwanza kwenye lile VOGO nilitest... Ile nawasha tuuu si nikasikia,
'Baba, babaaaaa, amka chakula tayari....!!!!!'

"MTOTO WA BRO ANANIAMSHA GHETTO...!!!!!!!"

You Might Also Like

0 comments: