Dada aliyetaka kuupima upendo wa mpenzi wake kwake hatimaye aumbuka kimya kimya
Mdada mmoja alitaka kujua kiasi gani
anapendwa na mume wake, hivyo akataka kujua
mumewe atafanya nini endapo ataamua
kuondoka na kumuacha!
Mwanamke huyo akaamua kuandika barua
inayosema "Samahani mume wangu, nimeamua
kuondoka na kwenda kuanza maisha mapya
mbali na wewe"
Barua hiyo akaiweka juu ya meza iliyokuwa
chumbani.
Baadaye jioni, muda wa Mumewe kurudi
mwanamke huyo akajificha chini ya uvungu wa
kitanda mule chumbani
Mume alipoingia chumbani akakuta ile barua
juu ya meza, akaisoma kisha, akaandika
maneno fulani kwenye ile ile barua, harafu
akaanza kuimbaimba kwa furaha huku akipiga
miluzi na akiwa anavua nguo.
Akapiga simu na akasikika akisema hivi "hello
mpenzi, nina raha sana leo.. yule mwanamke
nuksi amesalenda mwenyewe kaondoka na
kutuachia uwanja, jiandae nakuja"
Muda huo huo Mume akaondoka.
Mwanamke alipokuwa uvunguni akawa anatoka
lakini amenyong'onyea na amelowa mashavu
kwa machozi.
Akasogea pale ilipo barua na akataka kujua
mumewe aliandika kitu gani kwenye ile barua.
Akakuta maneno haya "nimeona miguu yako
uvunguni, tafadhali andaa chakula nina njaa
sana mumeo, ila nimetoka kidogo nafuata
maziwa nilisahau
kupitia. Nakupenda mke wangu"
0 comments: