Jinsi binti wa chuo alivyonifanya nipoteze fahamu kwa wiki kadhaa bila huruma

16:04:00 Unknown 0 Comments



Nakumbuka ilikuwa ni wiki ya mwanzo nikiwa ndio kwanza nimejiunga na chuo kikuu nilipofahamiana na Gloria ambaye yeye naye alikuwa mwaka wa kwanza akichukua masomo ya biashara na mimi nikiwa upande wa sheria.

Siku hiyo niliamka mapema na kufua nguo zangu na baada ya hapo nikajivuta mpaka sehemu ya chakula ambako baada ya kuagiza chakula changu nikakaa sehemu na muda mfupi baadae alifika huyo mrembo na kukaa nami kisha nikaanza kumchokoza kwa maneno shirikishi.

Masomo yakazidi kutubana na siku kwenda mbele kabla ya kuja kushuhudia uhusiano wangu na Gloria ukiwa umechukua sura mpya. Tuliporudi semista ya pili tukaanza kukaa wote kwenye chumba kimoja kama mtu na mpenzi wake na maisha ya chuo yakisonga.

Baadhi ya marafiki wakanishauri kuwa nakosea kujiingiza kwenye mahusiano ya namna ile hasa ukizingatia huwa hayana ukweli wowote na pia nakaa na mtoto wa watu na vipi kama ingetokea akapatwa na matatizo na kama hiyo haitoshi sio busara kuanza kukaa maisha ya ndoa badala ya kufuata shule.... 

Lakini mimi nikajiridhisha kwa kusema si nafuu mie nina mmoja huyu kuliko wenzangu ambao walikuwa na wapenzi zaidi ya sita na bado wakasema wao ni wasafi.

Tulipendana sana na huwezi amini kwamba ilifikia wakati tukawa kama wapenzi wa mfano kwa wenzetu kwa jinsi ambavyo tuliishi kwa furaha, kutoka pamoja na kuchukuliana kama marafiki jambo lililowapa wanafunzi wengi ujasiri wa kuja na kutuambia live kuwa kamwe tusiwasahau kwenye harusi yetu mara tukihitimu masomo.

Mwaka wa mwisho ulipoanza nasi tukaanza kuumia kuwa tutaachana kwa muda na kuumia kwani tulipenda baada ya kuhitimu tu tuendelee kuishi pamoja lakini tukajipa imani kuwa sasa tutasaidiana kutafuta kazi ili tuwe karibu kabisa ukizingatia mimi nilitokea mbeya na yeye ni mtu wa mwanza.

Muda ulipofika baada ya kukamilisha taratibu zote za chuo tukawa sasa tunasubiri siku ya mahafali ambapo mimi kwa siri niliandaa surprise party ya kumvalisha pete ya uchumba Gloria ambaye ni rafiki na mke mtarajiwa.

Siku moja kabla ya mahafali wazazi wake wakaja akaniomba nisionane nao kwani bado asingependa wanijue muda huo kwani haukua muafaka, na kuongeza kuwa ni vyema niende nyumbani kwao hivyo mimi nikawa mpole na kumwacha akiwa na familia na kwamba siku ya pili jioni baada ya mahafali nitamtoa out.

Siku ya pili niliwahi kusimamia kumalizia kupamba ukumbi kwa ajili ya surprise na kurudi chuoni kujiandaa tayari kwa mahafali. 

Tukiwa ukumbini kwa mbali nje nikamwona Gloria akiwa na baadhi ya ndugu zake na nikiwa nimemtupia macho kuona alivyopendeza na lile joho mara nikaona gari moja la thamani sana likipaki na kuna kijana akafungua malango na kushuka.

Yule kijana alivyoshuka alirukiwa sana na Gloria na kupeana kiss ambazo zikanifanya nihisi kama huyu jamaa anaweza kuwa sio ndugu bali nae ni mjanja mjanja wa mjini na anataka kuniibia mpenzi wangu.... Nikamwomba Mary ambaye alikuwa rafiki na dada yangu kuwa afuatilie na kujua nini kipo.

Nikawa busy na mahafali na mahafali yalipomalizika nikatoka mbio nje nimcheki Mary aniambie kuna nini kwani muda wote huo simu yake Gloria haikupatikana...Mary akanishtua kuniambia kuna muda walikuwa wakiweka mizigo na kusema wanaeda mjini walikofikia.

Nikakimbia kama kichaa nikiwa na lile joho mpaka hoteli walipofikia, nikaambiwa kuwa wameondoka nikiwa sijui nini na nini kinaendelea nikaona gari lao likiwa linapita kwenda bar moja maarufu sana kwa ugali nyama choma nikajua wanaenda kula na kupata moja baridi na moja moto.

Huwezi amini baada ya kufika pale  Gloria alinitambulisha kwa yule jamaa kuwa mimi ni kaka yake wa chuo na yule kaka akasema nashukuru sana kwa kukaa na mke wangu matajiwa vyema ningepeda tukae na kuongea zaidi ila tunaondoka leo muda huu...

Sikuongea chochote zaidi ya kuvuta picha juu ya yale maandalizi ya kumvisha pete na jsini nilivyoalika watu, na kama haitoshi mtu niliyekaa naye mika mitatu eti kumbe alikuwa akipoteza muda nami na huko kwao ana mme.... ??????

Fahamu inanijia nikaona nimezungukwa na marafiki na manesi wakiniambia nina siku nne nipo pale hospital baada ya kuletwa na msamaria aliyenikuta nikiwa nimeanguka njiani na  sijitambui.

Baada ya kukaa pale hospitali kwa wiki zaidi ya mbili, kumbukumbu zikaanza kunijia na nikaanza kukumbuka kisa cha Gloria na yule jamaa kilichonisababishia shinikizo la damu..

Ilinichukua zaidi ya miaka sita kuja kuanza kuwaamini wanawake wote.

Nikikumbuka mkasa huu wa Surprise party iliyosababisha mimi  kulazwa huwa siishi kusema  ........... Mapenzi ya chuo yana mambo

share na comment mtazamo wako juu ya habari hii kwa kubofya hapa

Usisahau kuangalia na kutoa maoni yako michezo hii hapa chini







You Might Also Like

0 comments: