JINSI YA KUISHI NA MWANAMKE MWENYE HASIRA

10:25:00 Unknown 0 Comments



1 Tafuta sababu ya yeye kukasirika. Angalia hiyo hasira yake imesababishwa na nini. Labda ni wewe ndiyo umesababisha kutokana na kukosekana na maelewano mazuri baina ya kitu anachohitaji na unachohitaji wewe kifanyike. Kaa naye na zungumza naye kwa upole si hasira kwa hasira italeta hali mbaya baina yenu. 

2 Omba msamaha bila kujali nafasi yako ya uanaume. Kama umekosea usikatae kosa muombe msamaha nakiri kosa lako kuwa hutarudia tena. Usimfanye akapandisha hasira zaidi na kuongea visivyofaa mkafika mahali ambapo hutaweza kuhimili.

3. Kuwa mpole katika kipindi ambacho unamuona kuwa mpenzi wako amekasirika. Kwa sababu akiongea na wewe ukaongea kwa hasira hakutatokea maelewano bali makwaruzano zaidi

4. Mtumie ujumbe wa mapenzi zaidi ya zile jumbe alizozowea kuzipata kutoka kwako. Msifie mara kwa mara na ajisikie vizuri pale ambapo ana maumivu ndani ya moyo wake.

5. Mtanie tanie utani wa kumrudisha katika hali ya kawaida ili ajisikie afadhali na kupunguza hasira zake.

... Mada yeyote tutumie inbox tutaijadili pamoja ...

Share and hit like if u ove it

You Might Also Like

0 comments: