Kumbukeni haya wapendwa dada zangu
1} Kamwe usimtegemee mpenzi wako wa kiume kama baba yako, jaribu kumwonyesha ajue kuwa kabla ya kukutana ulikuwa unajiweza na hata ukiachana nae utaendelea kujiweza.
2} Usimkane mpenzi wako kwa kuwa yeye ni masikini sasa, kwani tajiri wa leo ni masikini wa kesho na mtu hawezi kuwa fukara maisha yake yote, Utajiri ni sawa na vitambaa vya meza vinabadilishwa kila siku
3} Usiseme kuwa hakuna wanaume wa ukweli katika maisha yako wakati wewe kila kitu kwako ni feki, Kumbuka utampaka mtu kulingana na wewe ulivyo na maisha yako, ukiwa feki utakutana na feki mwenzako... kuwa real
4} Usiseme wanaume wanautaka mwili wako tuu wakati mavazi yako yanauonyesha mwili wako kila sehemu zikiwa wazi. Jinsi unavyo vaa ndio watu wanavyo kuthaminisha na kukulinganisha na tabia zako.
5} Usilalamike kuwa umekaa nae kwenye mahusiano kwa muda mrefu lakini bado hataki kuyafanya mahusiano yafungue ukurasa mpya wa kuwa mme na mke, Dada yangu sio kila mahusiano ni lazima yaishie kwenye ndoa.
6} Usiseme wanaume wote wako sawa baada ya kuumizwa, Kumbuka hata vitabu vya dini vinasema: kama ambavyo nyuso zetu zatofautiana ndivyo hata tabia zetu zinavyotofautiana.
7} Usiyachukie mahusiano kwa kutokana na kumbukumbu zilizopita, zaidi kumbuka kila mahusiano yana funzo la kukupa, na usifunge macho kwa kuogopa kuona mambo magumu kwani unaweza kuja kufumbua macho na kugundua kuna mazuri yalipita na bila wewe kuona... Usikate tamaa katika mapenzi
8} Usikimbilie katika kuolewa kwani kama Mungu ajuavyo siku yako ya kuzaliwa na ya kufa hivyo hivyo anafahamu kila mipango juu yako kwani sisi ni kama sisimizi machoni mwake, Muda wako wa kuolewa utafika kwa wakati kama ilivyo kwa kifo kinavyokuja bila hodi.
9} Unasema wanaume hawako siriazi na wewe, wakati historia yako na matukio yako ya nyuma yako kwenye vyumba vya hotel, simu za wanaume mabali mbali na hapa facebook una marafiki 5000 na kila picha yako inaonyesha jinsi ulivyo na wasifu mbaya, kila gari wewe umefanya gesti na pia kila mtandao upo na una wanaume wengi wengi umejianika vya kutosha, Kitu ambacho kinauonyesha umma kuwa umeathirka kifikra na msimamo
10} Kila siku mbukuka mambo yanatokea vile Mungu atakavyo....
Share na like Tabasamu na Fuledi
0 comments: