Majanga mengine ya fesibuku

08:19:00 Unknown 0 Comments


Wanandoa wawili waliokuwa wakifichana tabia zao zao za kupenda kuibanjua amri ya sita nje ya viao vyao vya ndoa jana wameipata ya mwaka baada ya siri zao kuwa hadharani.

Mme aliamua kufungua account mpya hapa fesibuku kwa jina lingine biloa kujua mke nae alikuwa na account nyingine maarufu sana iliyokuwa ikimpatia mabwana pamoja na vijisenti kutoka kwa wanaume wenye uchu wa kuchumbia kupitia fesibuku.

Basi jamaa baada ya kuona account hiyo yenye picha taamu za kimahaba ikambidi aombe urafiki na kukubaliwa bila kujua ni yule my wife wake akiwa am,eweka picha taamu alizozip[ata kutoka mtandaoni.

Baada ya kuchati kwa takribani wiki kadhaa huku akiwa kashanyoyolewa vijisenti vichache ambavyo huuma sana kama ungeambiwa umsaidie mtu asijejiweza, jamaa alifanikiwa kumshawishi binti huyo wakutane.

Binti akawa kesha mwambia kuwa anaishi dar na angependa kuja Mbeya kwa ajili ya weekend tuu na kurudi dar ambako anafanya kazi pia katika ubalozi mmoja maarufu hapa nchini na kuwa asingeweza kuja kwa basi hivyo jamaa ajipange kumfanyia utaratibu wa usafiri wa anga.

Baada ya jamaa kumtumia fedha kwa ajili ya usafiri wa anga jamaa akaamua kumdokeza mkewe kuwa atasafiri kwenda dar kikazi, mke akaona sasa isiwe taabu hatamwambia kuwa nae anasafiri atachofanya ni kuondoka kimya kimya ili akakutane na hilo buzi.

Basi majira ya saa nane jana mchana binti akampigia mupenzi mpya na kumwambia alishafika na yupo kwenye hoteli moja maarufu sana hapa mjini Mbeya, na jamaa akamuahidi kuwa nusu saa ijayo wangekuwa pamoja.

Nusu saa baadae jamaa alifika hotelini hapo na kumpitiliza moja kwa moja chumbani...

Sina ubavu wa kuendelea kuandika yaliyotokea hapo.....Tafadhali kama waweza kuwa mtabiri basi andika nini kilichofuatia

You Might Also Like

0 comments: