Ndugu usomaye unafikiri huyu dogo akasome wapi?
Dogo mmoja anasoma darasa la tatu.
Dogo:mwalimu mimi nataka kusoma darasa la nne maana hili la tatu halinifai,nina akili sana
Mwalimu:mmh hebu nikuulize maswali
Dogo:sawa
Mwalimu:kwenye ndege kuna matofali 20 ukidondosha moja chini yanabaki mangapi?
Dogo:hili swali rahisi mno,yatabaki 19
Mwalimu:nipe hatua za kumweka tembo kwenye fridge
Dogo:unafungua fridge,unamuing iza tembo kisha unafunga friji
Mwalimu:nipe hatua za kumweka nyani kwenye fridge
Dogo:unafungua fridge na kumtoa huyo tembo uliyemweka kwanza kisha unamuingiza nyani
Mwalimu:simba anasherehekea siku yake ya kuzaliwa,wanyama wote wapo kasoro mmoja
tu, Ni nani na kwa nini?
Dogo:ni nyani kwa sababu tumemuweka kwenye fridge
Mwalimu:bibi kizee amevuka mto wenye mamba na viboko wengi,aliwezaje ?
Dogo:amevuka kwa sababu wanyama wote walikuwa kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa
ya simba
Mwalimu:sawa,ingawa bibi alivuka
mto,mwishowe alifariki,unadhani kwa nin?
Dogo:alikufa kwa kudondokewa na tofali kutokakwenye ndege,kwenye yale 20 tulopakia na baade kudondosha moja chini
Mwalimu:Ndugu usomaye unafikiri huyu dogo akasome wapi?
0 comments: