Utafiti waonesha kuwa zaidi ya 90% ya kina dada wanaomiliki magari aka mikoko hawana kadi orijino za magari yao.
Utafiti uliofanywa na ukurasa huu feki wa Tabasamu na Fuledi umegundua ya kuwa asilimia zaidi ya 90 (90%) ya kina dada wanaomiliki magari aka mikoko hawana kadi orijino za gari hizo.
katika uchunguzi uliofanywa na wanahabari wetu wenye viherere na ambao wanaumia kwa nini wao hawana magari sehemu mbali mbali hapa nchini, uligundua ya kuwa mabinti walio wengi wao hupewa zawAdi za magari toka kwa shuga dadz kwa masharti ya kutopewa orijino kadi ya gari kama njia ya kulinda wasiwe wasaliti.
Aidha kina dada hao nao wao wamekuwa wakijisikia fahari sana kumiliki magari na kuonekana nayo sehemu mbali mbali za starehe wakiwa wanaendesha wao na haitakiwi kupanda mtu yoyote mwenye jinsia ya kiume maana mkoko unaweza dakwa na kurudishwa kwa mfadhili mara moja.
" yaani huwezi amini hata kaka yake huwa hapewi lifti kwani kaka huyu alikuwa kijijini wakati yeye anapewa gari, na siunajua lazima upeleke pasipoti au picha za kaka zako au ndugu watakao panda gari hilo ili mtoa gari akiwaona asijue anachakachuliwa na viserengeti boyz?" aliongea shuhuda mmoja ambaye hakutaka jina lake liwekwe hadharani.
He he he hehe wewe unadhani kadi inisaidie nini mimi?, kama akija kuchukua gari lake poa mimi si nitakuwa nimewapa jeuri wale wenye roho mbaya za kutopenda mafanikio ya watu na wanajua nilishawahi kumiliki gar na haijalishi nilipataje... Aliongea mmiliki mmoja wa gari lisilo na kadi.
Kwa upande mwingine mwandishi wetu alinusurika kupata makofi baada ya kumuuliza kaka mmoja, "mzee yaani wewe mimi nakufahamu sana tangu utotoni na najua huna kazi, sasa umewezaje kumiliki gari ukiwa mwaka wa pili hapa chuoni?' Fala sana wewe acha kufuatilia maisha ya watu mzurshi sana wewe hivi una nini wewe????? tuache na maisha yetu kama vipi timuka kabla sijapata kesi ya mauaji.... Aliongea kijana huyo kwa hasira kali sana
Umbwe la wanawake na baadhi ya wanaume kupenda magari huku wakiogopa kujituma katika kazi halali kumeibuka kwa kasi ya kimbunga hapa nchini na kusababisha badhi ya kina kaka kuwa kina kameruni (shoga) ili wapate magari kutoka kwa wadhamini na baadhi ya kina dada kuwapenda watu ambao walishaapa kamwe kuto wapenda na wenye umri zaidi ya babu zao ili tuuu waweze onekana mtaani wakiwa na mikoko.
Na kama haitoshi basi kuna jamaa wao wameamua hata kuwa wezi wa roba ili ndoto zao ziweze kukamilika.
Wakati tunaendelea na uchunguzi wa habari hii feki basi tunaomba kupata experience kutoka kwa wewe rafiki yangu kuhusiana na habari hii.
Habari hii haina ukweli wowote wanawake wanaweza na sasa ndio wenye kumiliki mali nyingi kutokana na uwezo wao mkubwa wa kuwa na matumizi mazuri ya fedha
Endelea kusoma hapa
0 comments: