Barua ya kusikitisha kutoka kwa rafiki wa tabasamu na fuledi..........Soma

17:39:00 Unknown 0 Comments





Hello Fuledi, 

Nakuandikia barua hii ili upate kuwapa na marafiki zako waone jinsi watu wasivyo na roho njema.

Nilibahatika kuolewa na kaka mmoja ambaye tulipendana sana na kweli alijionyesha kwa kila hali na nakumbuka kipindi hicho yeye hakuwa na kazi na ikabidi mimi nimsaidie kwa kuitunza familia yetu na huku nikimsaidia kutafuta kazi.

Alibahatika na kuja kuwa meneja uhusiano wa kampuni moja maarufu hapa dar, tulifurahia na mafanikio yakaanza kwenda safi na nikamshukuru Mungu kwa kitendo hicho.

Furaha ile ilikatishwa baada ya mimi kupata ajali ya gari na kisha kupata matatizo ya kiuno na kunifanya nikae hospitali zaidi ya miezi sita na kisha kurudishwa nyumbani.

Nilikuwa wa kuhitaji msaada kwa kila nitakacho si kuanzia uani mpaka kulala kuvaa na kila kitu.

Nikaanza kuona mwenzangu anabadilika na kurudi nyumbani usiku akiwa amelewa na sasa naweza kukaa na kujisaidia haja zozote nilipo bila hata ya msaada wowote, hali ile ilipozidi nilimpigia mdogo wangu na kuja kunitunza ingawa nikawa upande mmoja nimeoza.

Nililia sana usiku na mchana na kumwomba Mungu japo ikiwezekana niweze kufa na kuachana na shida hii na nakumbuka mwanangu alikuwa akilia sana kuniona vile lakini asingeweza kufanya kitu kwani alikuwa na umri wa miaka 5 tu.

Mambo yakaanza kuchukua sura mpya baada ya yeye kuanza kuingia na wanawake na kulala nao chumba nilichopo na baadae kuniweka chumba cha nje, baada ya kuona yale niliamua kurudi kwetu na nakumbuka baba na mama walinipokea na kunilea upya kama mtoto mchanga.

Miaka miwili baadae nilifanikiwa kuangaliwa upya na kuonyesha kuwa kuna dalili za kuweza kupona nikifanyiwa upasuaji. Nikakubali na sasa nimepona na nimerudi kwenye majukumu ya kawaida.

Namshukuru sana Mungu kwa mtihani huu alionipa na nimejifunza mengi sana na sasa najua usiseme mtu anakupenda mpaka pale mtakapoweza kuvuka vizingiti vingi mkiwa pamoja tena kwa imani, mapendo na furaha ile ile.

Mme wangu sasan kafukuzwa kazi baada ya kugundulika alikuwa akijihusisha na ubadhilifu wa fedha na pia nimesikia nimgonjwa wa kifua kikuu najisikia kuwa na roho nguvu nisimsaidie lakini namwomba Mungu anipe nguvu ya kumsaidia matibabu apone kwani kwa sasa nami nina plani zangu na mwanangu na sifikirii tena kuja kuishi na mume............ 

Asanteni wazazi wangu mmenionyesha kuwa nyie ndio marafiki wa kweli.

You Might Also Like

0 comments: