Habari ya motoooo!!!!: Binti apewa sapraiz ya mwaka ashindwa kukataa aolewa bila kutarajia..... Marafiki waandamana.....Mbeya kuna mambo walai tena

19:59:00 Unknown 0 Comments

Nakumbuka nilikuwa natoka kazini majira ya saa kumi jioni nikipita katika mtaa mmoja kuelekea nyumba njiani nikakutana na kijana mmoja akiwa kakaa kinyonge sana.

Akaniambia dada je utaweza kunisaidia japo 2000 niweze kupata chakula?

Kama ilivyo kawaida ya vijana wa mjini ambao hawapendi kazi na mwishowe kuwa omba omba au kutaka kulelewa nikaona isiwe taabu nikampa.

Alinishukuru sana mpaka nikajawa na huruma kidoogo nimwongeze ila akili ikanikumbusha suala la chuma ulete na baadhi ya matapeli wa mjini ambao nao hujifanya kuwa wanashida kumbe ni matapeli.

Kijana huyu alikuwa kama ana miaka mitatu au minne zaidi yangu na kiukweli alionekana nadhifu sana.

Ikawa haipiti siku mbili kila nikipita pale lazima atanisalimia na muda ulivyozidi kwenda nikaona nazidi kuwa karibu naye.

Ukaribu ule uliendelea mpaka nikamkaribisha nyumbani kwangu na akawa rafiki wa karibu sana pale mtaani.

Lakini kuna jambo likawa linaniumiza kichwa juu yake kwani kila nilipotaka kuomba niende kwake alikataa kata kata na hata kukosa raha.

Nikaanza kuhisi asije akawa sio mtu mzuri hivyo nikaanza kumwekea mitego ya kupajua kwake ili niiridhishe nafsi yangu kuhusu ukweli wa maisha yake.

Nilifanikiwa siku moja kumnasa akiwa anaelekea kwake na nikamnyemelea mpaka nilipofanikiwa kuingia kwake.

Aliduwaa kwa mshangao na hakuonyesha kupenda mtu afike pale kwani alikuwa akilala chini na chumba kilionekana kitupu zaidi ya nguo kadhaa pamoja na kagodoro kadogo, begi na kajiradio kalikokoroma badala ya kuliwaza na kukifanya chumba kiwe na kelele.

Hakuweza kuongea kitu na ilimchukua siku kadhaa mpaka alipokuja kunipa ukweli juu ya maisha yake.

Jina lake halisi anaitwa Morgan na  aliishia kidato cha nne na kusomea udereva baada ya kukosa wa kumsomesha na hakubahatika kuajiriwa mpaka pale alipoamua kuja mjini kutafuta maisha.

Pamoja na mambo mengine ya kutoifahamu familia yake yaani baba na mama yake nikakuta naanza kuumia na kuingiwa na moyo wa kumsaidia.

Wakati huo mimi niliajiriwa katika kampuni moja nikiwa kama secretary hivyo nikawa najaribu kumpa sapoti ya mahitaji machache na kuangalia kama ningeweza kumsaidia apate ajira.

Muda ulivyozidi kwenda nikaja kujikuta tayari nina uhusiano na Morngani na bila hata ya kushangaa nikaona upendo unazidi zaidi na zaidi ni kuwa hakuwa kijana wa makuu wala mwenye kuniomba msaada mpaka pale mimi nilipohisi ana uhitaji jambo ambalo ni nadra kwa vijana wa digital.

Tulizidi kupendana na wakati huo alikuwa amepata daladala ya kuendesha ingawa mimi nilikaa na kufikiri kisha nikaona ni bora  nichukue mkopo pale ofisini wa milioni tatu ili nimpe aanzishe biashara.

Baada ya kuomba mkopo na kumpa siku hiyo alifurahi sana na siku ya pili yake tukakubaliana aende kulipia chumba na kununua mzigo ili duka lake lianze kazi na mimi nikarudi nyumbani.

Usiku ule hakuwa mfupi kwani
niliona masaa hayaendi ili muda ufike nitoke kazini nikashuhudie duka la mpenzi wangu likiwa tayari kwani sehemu ya kuchukulia mzigo haikuwa mbali na pale na hatimaye asubuhi ikafika na nikaenda kazini.

Niliwahi siku hiyo kutoka kazini na moja kwa moja nikaenda katika kile chumba cha duka na kukishuhudia kikiwa kimefungwa wazo la haraka likanijia kuwa atakuwa amechoka yuko nyumbani.

Nikapitiliza mpaka nyumbani kwake ambako niliishiwa nguvu baada ya kuona macho yake yakionyesha kuwa alikuwa akilia na pia nguo yake imechanika na ana vumbi.

Nilichoka na hata sikutaka kuuliza kitu zaidi ya kumwambia pole...

Akaitikia ki shingo upande na kunisimulia kuwa alivamiwa akiwa anaelekea kulipa pango kabla ya kwenda mjini kununua mizingo ya duka.

Nilimwelewa na ikapita miezi kama mitano hivi tukiwa tunashirikishana mipango ili tujue tutaishije na wakati huu sasa akawa amepata kazi ya kuendesha gari la watoto wa shule moja pale mtaani na tukawa tunaishi kwa furaha kila mtu akimpenda na kumwamini mwenzake na huku tukiahidiana ya kwamba baada ya kujiweka vyema tutaanza taratibu za ndoa.

Siku moja nikiwa kazini nilipigiwa simu na rafiki yake Morgani aitwaye Fred kuwa morgan amepatwa na ajali akiwa kazini na hivyo amesafirishwa kupekekwa makao makuu ya mkoa ambayo yalikuwa umbali wa takribani kilomita 300 na kitu kutoka pale tulipokuwa na hivyo anakuja kunichukua twende haraka.

Nikatoka ofisini baada ya kuomba ruhusa na kwenda mpaka nyumbani ambako nilichukua akiba ya fedha na wakati huo fred alikuwa kaja na gari pale.

Aliendesha gari lile na baada ya masaa matano tulifika pale na muda huo ilikuwa ni saa kumi na moja ya jioni na gari likaingia hospitali moja kubwa pale na kupaki.

Alikuja mtu kutupokea na kutupeleka chumba kimoja lakini chumba hiki kilikuwa kama ni ofisi vile na dada mmoja akaja akitaka kutupa kahawa.

Nilikataa kwa kuwa nisingeweza kula au kunywa chochote bila kujua morgan wangu anaendeleaje..... Hivyo dada akaondoka.

Robo saa baadae alikuja dada mmoja aliyevaa kitambulisho cha secretary akatuita kuwa tunaitwa na boss wa hospital.....

Wakati huo machozi nilishayafuta zaidi ya mara sita na sasa kwikwi zilianza kwa chinichini nikiamini tunaenda kupokea taarifa za msiba wa kipenzi changu Morgan.

Ulifunguliwa ule mlango mwili ulichoka pale nilipokutana uso kwa uso na Morgani akiwa amekalia katika kiti cha mkurugenzi na kabla hata sijatamka neno nilishangaa kuona picha za mimi na yeye zikiwa mle ofisini.

Nilishindwa kuongea wala kusema kitu zaidi ya kuishiwa nguvu na kutaka kuanguka kabla ya kudakwa  na baada ya kusaidiwa kunyanyuka nililala usingizi mzito na kuamka siku ya pili yake.

Niliamka na kushangaa nipo kwenye jumba la kifahari na wafanyakazi wakiniita mama, nikauliza hapa ni wapi wakaniambia ni nyumba ya Morgani..... Nilishangaaaa

Morgani wakati huo alikuwa ameondoka na aliporudi alikuwa yuko na wazazi wake na baadhi ya ndugu na jamaa na ndio wakaanza kunisimulia kisa cha mimi kudanganywa kuwa morgan ni kijana fukara.

Morgani anatoka katika familia ya kitajiri sana pale mkoani na katika maisha yake kila mwanamke aliyekuwa nae kwenye mahusiano hakuwa na mapenzi zaidi ya fedha huku wengi wao wakipandikizwa na maadui wa familia ili kuiba utajiri wao.....

Baaada ya kuumia vya kuyosha morgan akapatwa na wazo la kwenda mbali na kujifanya maskini na kisha kunipata mimi na sasa anahisi kwa zaidi ya mwaka na zaidi tulioishi wote nafaa kuwa mke.

Siku ya pili yake alinipa ile fedha aliyosema imeibiwa na nikarudi ofisi na kufanya utaratibu wa kuacha kazi na kuhama kule kijijini kwenda kukaa na morgan na sasa naitwa mama morgan na wengi wanapenda kuniita salome morgan

Na niliolewa kwa namna hii na sasa nina miaka 6 ya ndoa...........

Share nawe story yako.

Whatsapp 0713317171


You Might Also Like

0 comments: