Anayetaka Kuoa na Anayewinda kuolewa wote wana AGENDA,ziwe za siri au za waziwazi...

11:03:00 Unknown 0 Comments




Vikao vya Harusi huwa na AGENDA...
Vikao vya Bodi huwa na AGENDA
Bila Agenda,hakuna umuhimu wa kikao...
Anayetaka Kuoa na Anayewinda kuolewa wote wana AGENDA,ziwe za siri au za waziwazi...
Agenda za Mwenyekiti wa Kikao lazima ziwekwe wazi kwa Wajumbe ili waweze kuchangia na kukubaliana au kukataa utekelezaji wa Agenda tajwa!
USIKUBALI!NARUDIA USIKUBALI! Usikubali Mtu atimize Agenda zake kwa kupitia mgongo wako...USIKUBALI!!
Wewe una AGENDA ya kuolewa ili uanze familia na utulie kwa sababu UKO TAYARI,anayekuoa ana AGENDA ya kuoa kwa sababu amechoka kula baa,anatafuta mfuaji wa nguo asiye na gharama,anaoa aridhishe wazazi wanaomuuliza sana kuhusu Ndoa...Agenda yake itatimia kwa mlango wako...Kwake ni DEAL DONE,kwako ni MAJANGA LOADING
Wewe una AGENDA ya kuoa coz UKO TAYARI, Mke unayemuoa ana Agenda ya kuwaziba midomo mashosti waliochonga ataolewa lini na kutoa gundu kwamba na yeye ana Pete....Kwake DEAL DONE,kwako MAJANGA LOADING!
Ndoa zinakufa fasta coz AGENDA ZENU HAZIFANANI,mmoja ana Agenda za Siri na wewe unamsaidia kuzitimiza ukijua unatengeneza Mbingu duniani kumbe mwenzio KAKUTEGA..
Kabla hujasema NDIO kwenye Kikao,hakikisha Agenda za Kikao zinaku-favour wewe na sio kumfavour mwingine huku wewe unagugumia
Ukinielewa Ubarikiwe sana

Ujumbe huu umeandikwa na Mtume na Nabii Seth kutoka Facebook Church Of All Nations-



You Might Also Like

0 comments: