Mke wangu nae kapimwa na ameonekana na mambukizi ya ukimwi na wote tumenza dozi.

05:45:00 Unknown 0 Comments

Kwa muda wote huo mke wangu hakujua hela zilikuwa zinatoka wapi za  kuilisha familia na kuiresha ile furaha iliyotoweka pale nyumbani.

Muda wote nikiwa pale nyumbani nilijitahidi kufurahi na kuwafanya wote waweze kuamini kuwa sasa maisha yalirudi na kuwa safi kama mwanzo.

Nikakumbuka mwaka mmoja niliokaa bila kuwa na kazi maisha magumu bila ya kuwa na uwezo wa kutambua kesho itakuaje.

Ikakumbuka nilivyilokuwa nikiwaza kama ingetokea mtoto akaumwa usiku nikaishia kutoa tabasamu dogo na kisha kuchukua glass na kuweka grants na kuanza kunywa.

Nilikaa kwa zaidi ya saa moja nikinywa pombe yangu ile kabla ya kushtushwa na mlio wa meseji ya simu na baada ya kuinyanyua nikaona na meseji ya mama dear.

Nikaisoma ile meseji na kuanza kufikiri mambo mengi na ukizingatia muda huo nilitakiwa kwenda kumpeleka mke wangu na watoto waende sokoni na kisha tupate wakati wa kwenda kula chakula cha jioni hotel moja maarufu pale mtaani.

Niliwaza jinsi ya kumuaga mke wangu na kumwambia naondoka lakini hakukuwa na jinsi nikaondoka baada ya kumweleza nina dharura na kwa kuwa hana matatizo mimi nikaondoka na kuendelea na safari.

Nikiwa ndani ya gari machozi yalinitoka kwa kuwa hali ya kuwa mtumwa wa ngono ilianza kunichukiza na kutaka kuachana nayo lakini sikuwa na jinsi baada ya kufikiri ningepata wapi tena fedha za kuifanya familia ifurahi.

Baada ya kukutana na mama dear akaniambia kuwa ana safari ya ghafla ya kwenda kampala kikazi na kuwa amenikatia ticket na tunatakiwa kuondoka usiku huo.

Sikuwa na la kusema zaidi ya kuchukua simu na kumpigia mke wangu kuwa natakiwa kusafiri na ningerudi baada ya wiki.

Mama dear alijaribu kunifanya nifurahi lakini machoni nilionyesha kuwa na furaha lakini moyoni nikawa sina raha hasa nikiamini kama nisingejifanya kufurahi basi angenyang'anya kila alichonipa.

Mama dear na mimi tulifahamiana miezi mitatu baada ya kufukuzwa kazi na yeye ni mfanya biashara maarufu pale mkoani na alinitaka kumapenzi na kuamua kuwa naye kwani aliniahidi kunipa maisha mazuri mimi na familia yangu baada ya kuupata mkasa mzima wa maisha yangu.

Tangu hapo nikawa sina neno zaidi ya kumsikiliza na kufuata kila asemalo na hatimaye kuwa mtumwa wa mapenzi kwani kama ningekataa kitu basi angechukua gari lake na hata kukatisha fedha alizonipa kila mara na kila mwisho wa mwezi kiisaidia familia yangu.

Tukiwa pale kampala mida ya usiku tuko bar moja tukiwa tunakunywa kujiandaa na siku ya pili kufanya kazi, nakumbuka ulitokea ugomvi baada ya kuja kaka mmoja aliyejitambulisha kama ana mahusiano na mama dear.

Baasa ya ugomvi ule mimi nilipigwa risasi ya begani na baada ya matibabu tulirudi Tanzania

Niliuguza kidonda kile bila ya kupata unafuu na wakati huo habari zikawa zimemfikia mme wa mama dear ambaye alikua akikaa nchini Botwasa na kumchukua mkewe na kumpeleka huko nchini botwsana.

Kidond hakikupona na nikazunguka sehemu mbalimbali bila ya mafanikio kabla ya kugundua kuwa pia niliambukizwa HIV  na kwa kuwa kuna baadhi ya madeni katika nyumba niliyokuwa nikikaa ilinibidi niuze magari na kuokoa familia.

Mpaka sasa sina la kufanya wa kusema zaidi ya kuumia na kuulaumu uamuzi wangu wa kuwa na mahusiano na mama dear badala ya mimk kujituma kufanya kazi na kuiokoa familia

Mke wangu nae kapimwa na ameonekana na mambukizi ya ukimwi na wote tumenza dozi.

Vijana wenzangu maisha ni kujituma na kuwa imara nyakati za shida na sio kutafuta njia rahisi kutatua au kuyajibu maswali magumu

You Might Also Like

0 comments: