Furaha huja na huzuni

13:54:00 Unknown 0 Comments

Mara ya kwanza kukutana nae ilikuwa ni eneo la posta jijini mbeya, nilikuwa katika mizunguko yangu ya kutafuta riziki za hapa na pale.

Kwa kweli sikuwahi kuwaza wala kutegemea kuwa kuna siku hali kama hii ingekuja kunitokea kwani kutokana na hali yangu ya maisha na majukumu niliyokuwa nayo nisingeweza kufiria wala kuwaza hiki kitu ambacho siamini hadi muda huu kuwa kimenikuta.

Mboni zangu zilizojaa huruma na ukarimu na mwili wangu ulishiba nguvu na ujasiri na roho ya kutokata tamaa ndio vitu ambavyo siku zote nilijivunia ingawa sikuwa na mafanikio makubwa.

Basi nilipozidi kusogea akili yangu ilibadilika nikawa mtu tofauti kabisa kiasi cha kwamba nilijiona mtu mpya kabisa katika dunia hii. Moyo wangu uliojaa machungu, huzuni na kero za maisha ulibadilika ghafla na kuwa kama mtu ambaye amezaliwa upya.

Mdomo wangu uliobarikiwa kuwa na maneno mengi kwa kweli siku hiyo ulibakiwa na neno moja tuu "NAKUPENDA"

Mkono wangu wenye nguvu na misuli liyojengeka ulibadilika na kuwa kama mkono wa mtoto mchanga kwani nilishindwa hata kuunyanyua wa kuita.

Basi, natamani macho yangu yangekuwa ya kwako ushuhudie kile nilichokishuhudia mbele yangu siku hiyo.Gauni moja refu jeupe, viatu vyeusi, skafu ya blue, nywele za singa singa , macho ya gololi, vidole vyembamba kama peni aina ya speedo, kope nzuri mfano wa manyoya ya tausi pamoja na tabasamu.

Kwa ujumla vyote hiliumba kiumbe mmoja wa ajabu sana ambaye katika maisha yangu yooote sikuwahi kutegemea kama mboni zangu zingeweza kuona na kushuhudia uumbaji huo.

Nilipaza sauti kwa ujasiri na kusema , " Ha ha ha Dada habari!" baada ya hapo nikajisogeza na kumshka mkono. Kwa kweli hali niliyohisi baada ya kumshika ule mkono shida na matatizo yangu pamoja na mawazo vilipotea.

Ama kweli, niaamini ule usemi usemao "mapenzi yana run dunia". Nisiongee sana nini kilitokea nakumbuka hadi mwisho wa siku mimi na yeye tulikubaliana kuwa wapenzi.

Zilipita wiki kadhaa tukiwa tunawasiliana na kupanga mipango mbalimbali na ukweli niliougundua ni kwamba tulipendana kwa dhati.

Mwaka mmoja ulipita nilijitambulisha kwao na mipango ya harusi ikaanza na yakabaki masaa kadhaa kbala ya kufunga ndoa yetu ambayo hayo masaa sitaki kabisa kuyakumbuka  katika maisha yangu kwani  mimi na familia yangu tulitangulia kanisani tukiwa na furaha na moyo wangu ukiwa umejawa na amani kwani niliona ile ndoto ya kuja kuishi na salome.

Nikiwa kanisani nikimsubiri afike huku mapambio yakiendelea nilimwona padre akija huku akionekana kuwa na uso wenye majonzi. Sikuelewa kwa mara ya kwanza ila jinsi alivyozidi kunisogelea niliwaza vitu vingi sana kuwa nini kimetokea.

Aliniita na tukatoka nje kisha akaanza kuniambia,  "kijana, nasikitika kukuambia kuwa nimepokea simu kutoka kwa mmoja wa waumini ambao walikuwa wanakuja kanisani kuwa kuna ajali mbaya imetokea karibu na sokoni upande wa kujia kanisani. Na taarifa zinasema kuwa waliokuwepo kwenye gari lile wote wamefariki papo hapo. Kati ya hao waliofariki mmoja wapo ni salome"

Niliona dunia inapasuka na sikuamini alichokuwa akikiongea na nikatamani nimmeze au hata kumjeruhi ili ajifunze kuacha utani wenye majonzi  nyakati za furaha. Ila kweli alichoongea kwani nilimwona baba mkwe akilia na mama mmkwe akiwa amezimia.

Nilibanwa na mkojo na baadae nilipoteza fahamu kabisa, nilipozinduka nilitamka neno moja tuu " Kweli furaha huja na kuondoka, binadamu hupanga ila Mungu hupanga zaidi"

Nakuombea wewe ambaye unaisoma habari hii Mungu apange kila mpango wako na kuusimamia na siku zote kumbuka kuwa furaha huja na kuondoka, hivyo basi wakati wa furaha mshukuru Mungu na wakati wa huzuni pia jikabidhi kwake.

Comment ASANTE MUNGU nipo hai na nina furaha kisha share habari hiii

kumbuka kusoma mwendelezo wa kisa cha simu ya ajabu leo jioni kupitia ukurasa wake wa Simu ya Ajabu

You Might Also Like

0 comments: