HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU " Season 13

14:14:00 Unknown 0 Comments

HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

Season 13
ILIPOISHIA JANA

Kupokea kumbe alikuwa ni secretary akiniambia mbona umechelewa kuna kikao unasubiriwa wewe, kutazama saa ilikuwan ni saa sita kasoro nikakurupuka na kuingia bafuni kisha nikajiandaa na kwenda haraka kazini.

Nilipofika pale nikasalimiana na watu, katikati ya kikao simu iliita nikaomba nitoke nje ili niipokee. Daah daaah daah haki ya nani hii simu ilinifyanya .............................................................................

ENDELEA
NILIPOFIKA pale nikasalimiana na watu, katikati ya kikao simu iliita nikaomba nitoke nje ili niipokee. Daah daaah daah haki ya nani hii simu  ilinifanya nipoteze mood ya kikao na kuanza kuongea peke yangu kama mtu aliyekuwa akijiandaa kwenda kuhutubia.

Simu hii iliniambia kuwa kabla ya kuondoka kuna mtu mtu ataniletea bahasha yenye maelezo na kuwa natakiwa kuyasoma na kuyaelewa kabisa na kuhakikisha sifanyi mzaha na kusisitiza nisichelewe.

NilirudI kwenye kikao na nakumbuka kila kilichojadiliwa mimi niliitikia kwa kichwa na kana kwamba yananiigia lakini hakuna kilichokuwa kikiniingia wakati huo zaidi ya kuwaza juu ya hiyo bahasha.

Saa kumi kasorobo muda wa kuondoka na kila mtu akiondoka mimi nilijifanya busy pale ofisini ili tu nisubiri hiyo bahasha. Ingawa nina uoga lakini hamu yangu kuu ilikuwa ni juu ya hiyo bahasha na yaliyomo ndani yake.

Nikiwa katika dimbwi zito la tafakari mara nikashtushwa na sauti ikiita, Mwakibubu!!!, Mwakibubu, baba Amigo!!! bado uko ndani?????

Nilikaa kimya na kujishusha kutoka kwenye kiti ili niweze kujivuta na kumtazama kwa ukaribu huyo aliyekuwa akiniita. Alikuwa ni bwana Tembo muuza chipsi maarafu pale karibu na ofisi akiwa na bahasha mkononi.

Nikaitika na kutoka nje na akanipa bahasha na kusema kuna mtoto amepita na kunipa hii bahasha akawa hajui mwakibubu ni nani, sasa mimi nikaambiwa uko ndani nimeona nikuletee... Vipi leo nikuwekee mishkaki mingapi??

"Achana na mishkaki kaka, niko busy kidogo nipe hiyo bahasha halafu siku nyingine angalia mood ya mtu sio kila muda ni mishaki, mbona huniambii unanipa bia... wewe wa ilolo nini?" 
Tembo aliduwaa kwa sekunde kadhaa na kuondoka huku akiivaa vizuri suruali yake kama mtu aliyepigwa kibuti na binti aliyemsubiria apite sehemu hiyo kwa muda mrefu na kuishia kupata cha mbavu.

Nikajivuta kwa haraka kutoka eneo hilo baada ya kufunga milango ya ofisi na kuingia ndani ya gari kisha nikajifungia kisawa sawa na kuifungua ile bahasha ili nione sasa nini kipo ndani.

Ndani ya ile bahasha kulikuwa na ufunguo na malekezo yaliyonitaka kuwa niende hoteli moja iliyo nje ya mji na kuingia katika chumba kimojawapo na kumshubiri huyo mtu anipe maelekezo mengine na alisisitiza nisipofanya hivyo kitakachonikuta sitaweza kukisimulia maana nitakuwa nimekufaa baada shuruba kali.Na akasisitiza polisi au mtu yeyote yule asijue nini kinaendelea....

Hofu ilinijaa na picha kichwani ikanijia ya bonge la jeneza na watu wakiniimbia "tumpeleke mwana huyu kwenye nyumba ya milele."

Wazo la haraka likanijia kuwa kwenye gari langu huwa naweka biblia hivyo nikaichukua na kuanza kusoma bila kujua ni mstari upi ungenipa faraja na ujasiri kwa muda huo na baadae nikaishia kulitia gari moto na kuondoka kwa kasi ya ajabu.

Nilifika pale hotelini na kumwambia mhudumu wa mapokezi kuwa natakiwa kwenda chumba namba 6 east wing. Mhudumu akaniuliza kama mimi ndio bwana mwakibubu nami nikaonyesha kukubaliana nae kwa kutikisa kichwa na akanichukua kunipeleka chumbani.
NIliufungua mlango ule na kuingia mle chumbani na moja kwa moja nikajitupa kwenye sofa nikiwa na hofu kubwa sana. Chumba kile kilionekana ni cha gharama kubwa sana na sikujua ni mwanaume au mwanamke aliyekichukua kile chumba.

Kwani kama ni mwanamke na ni yule wa kwenye simu basi ilikuwa shida na kama ni mwanaume nikaanza kukumbuka itikadi za saudia kisha nikanyanyuka na kuukaza mkanda wangu vyema kama wasemavyo wahenga, "vita ni maandalizi bwana"

Nikiwa katika hali ya kujiweka sawa kwa mapambano na wakati huu ujasiri ukianza kunijia kwa mbali mara simu ya mezani iliita. 

Nilitulia kama sekunde kadhaa nikihofia juu ya simu hiyo kama ni yangu au la na kisha nikaifuata na kuipokea..Kwa kweli simu hii ilibadilisha kabisa mawazo yangu kwani maneno yaliyoongelewa................................................................

Je simu hiyo ilikuwa na ujumbe gani au ilinitaka nifanye nini?

Usikose kisa hiki kesho jioni


Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu kwa udhamini wa Gracious HOUSE of CAKES watengenezaji maarufu na waliobobea wa keki za aina mbalimbali kwa hafla mbalimbali waliopo jijini Mbeya na wanapatikana kwa namba 0767218014

Usikose kupata tiketi yako sasa ya kuhudhuria Green City A piece of cake party kwa kupiga namba 0654690368


Nawe waweza kuwa mdhamini wa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

share, like na comment

You Might Also Like

0 comments: