NImekusamehe ila sitakusahau mpaka naingia kaburini NEY

08:18:00 Unknown 0 Comments


Jumamosi ile nilikuwa ndio kwanza nimetoka kufurahia baada ya matokeo yangu ya chuo kutoka na kwa kuwa nilikuwa nina kiwango kizuri sana cha maendeleo yangu paale chuoni nilishaahidiwa kazi na kampuni moja inayojishughulisha na masuala ya technology mara matokeo yakitoka.

Rafiki yangu aitwaye Ney yeye kwa bahati mbaya alitakiwa kurudia mwaka na akawa na mawazo sana hivyo akaniomba niende nikamsindikize beach ili aweze kupoteza mawazo.

Nikajiandaa na kwenda kumfuta na kisha tukaenda zetu, tukiwa kituoni akaniambia kuna wenzetu tuwasubiri tunaenda wote. mara ika simama gari dogo aina ya BENZ macho ya panzi na kupaki pale na Ney akasema tuingie.

Nikaanza kupata wasi wasi kwani mle ndani kulikuwa na wazee wawili na nikamtext whatsapp akaniambia nisiwe na noma huyo mzee ni mpenzi wake na anataka akampe hela then tuwe free.

Kweli akatupeleaka pale na kumpa hela Ney na kutuacha tukiwa tunapata raha zetu mpaka tulivyochoka akampigia aje kutuchukua turudi home.

Tukiwa njiani Ney akaniomba nimsindikize kwani mzee anataka waende sehemu waongee. Nikamkubalia kwani asubuhi nilimwona ni kama mstaarabu na ney alinihakikishia hivyo.

Nilipofika pale nikamwona na yule mbaba ambaye asubuhi alikuwa pamoja na mzee wa ney, basi tukakaa pale mie nikawa nakunywa juisi na Ney yeye anazitwanga wine na pombe kali. Nikamtext kuwa nataka niende zangu akaniambia nisiondoke ili yule mzee asimfanye kitu.

Story zikaendelea na baadae nikawa napigiwa simu nikaomba kutoka na kwenda kupokea simu, jambo nalokumbuka ni kuwa nilikuja shangaa kuona naamka nikiwa kwenye ile nyumba tena asubuhi.

Nikaenda bafuni kujikagua nikashtuka kwanza kuona nina maumivu makali sana kwenye makalio yangu na sehemu za siri. Nikaanza kulia kwa uchungu na huku kichwa kikiwa kinaniuma.

Wakati najishangaa pale na machozi yanidondoka akaja yule mzee akiwa na bunda la hela huku kashika bastola tu na kuniwekea hela kitandani na kuniambia hizo zikusaidie kununua sanda, kwa uchungu nikaanza kulia nikiwa bado nimejiinamia pale akaja Ney huku akiwa analia na anashindwa kutembea.

Wakati huo yule mzee ameshaondoka na pale, nikamuuliza kwa nini ulinileta huku NEY???????

NEy akasema nisamehe nami nimefahamiana nae kupitia facebook na ilikuwa mara yangu ya pili kuonana kwani mara ya kwanza alinipigia simu na tulionana nae dakika chache kwani nilikuwa busy sana sikuweza kukaa naye na leo ndio mara ya pili.

Sikuwa na cha kufanya nikaondoka na kurudi nyumbani na kwa kuwa nilikuwa bado nakaa kwenye nyumba niliyopanga hakuna aliyejua chochote.

Miezi miwili baadae nikaenda kupima na sasa nimegundulika ni muathirika.

Nimeumia hasa kwa kuwa rafiki niliyetaka kumfariji siku ile ndiye sasa kanipa majuto ya maisha yangu mpaka nitakapo kufa.

Jamani Facebook ni nzuri ila tuwe makini na watu tunaochati nao.

Nimemsamehe NEy na naamini MUNGU atanipigania

Asanteni marafiki

You Might Also Like

0 comments: