Alipofika karibu na nyumbani kwake alinyata na kutembea taratibu kwa tahadhari ya kutomkurupusha mgoni wake huku akiwa na kitu kizito mkononi mpaka dirisha la chumbani mwake na kusikia minong'ono ya watu wawili wakisema , vua haraka niakuogeshe si unajua nimechoka???
HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Season 29
ILIPOISHIA JANA
Season 29
ILIPOISHIA JANA
Mwakibubu alinyanyuka na kuanza kukimbia akimfuata baba pachu ambaye alikuwa kaishiwa nguvu na pozi wakati mwakibubu akiwa anampa simu mara nae simu yake ikaanza kuita.
Ile anaipokea tu ile simu .............................. ...................
ENDELEA
Ile anaipokea tu ile simu ghafla simu ya mwakibubu ilianguka chini bila kujua namba ya mpigaji na akaiokota na kuiweka mfukoni bila kuiwasha akimsaidia baba pachu kuingia kwenye gari na kuanza safari ya kumrudisha nyumbani.
Walifika nyumbani kwa baba pachu na kumkuta mama pachu akiwa sebuleni na majirani wakiangalia tamthiliya. Baba pachu alifika moja kwa moja na kuwasalimia na kupitilia chumbani ambako alijilaza kitandani huku akianza kuwaza na kufikiri huyo chamdoli anataka kumwambia nini usiku na ni kwanini amwite mpenzi wake.
Haraka akapata wazo na kuanza kupekua kwenye kabati lake la vitabu ili aweze kuona kama kuna kitabu chenye kusimulia habari za zamani kama kuna watu au mtu aliyewahi kutokewa na mambo kama haya.
Aliishia kupekuwa bila ya kupata kitabu na kupitiwa na usingizi mzito uliomchukua kwa masaa matatu na alipokuja kushtuka ilikuwa ni saa mbili na nusu za usiku. Akaamka na kuingia bafuni ili ajiandae kutoka kwenda walikoahidiana na mwakibubu kwa ajili weekend.
Akiwa bafuni kajiwagia maji na huku akiwa na mapovu mara simu yake aliisikia ikiita na alikurupuka kutoka pale bafuni mpaka chumbani na kuidaka haraka simu hiyo na kuiangalia bila kutambua mama pachu alikuwa mle ndani pia.
" Mme wangu una matatizo gani wewe? yaani simu inaita unatoka spidi bila hata ya kujifunga taulo, vipi kama ningekuwa na watoto?
kwani una nini mme wangu siku hizi?" alimaliza kuhoji mama pachu huku akiziandaa nguo za kwenda kuzinyoosha
"aaah ni simu yangu ya hela na huyu jamaa anajifanya busy sana usipopokea inakuwa kiteteo cha yeye kughairi na kuitumia kwa matumizi mengine na mbaya zaidi nimeikuta simu ikiwa imekatika" alijitetea baba pachu huku naye akiingia bafuni na simu mkononi
Mama pachu alitoka mle ndani huku akijisemesha kuwa amemuuliza maswali mengi mno kwani naye bado alikuwa akikumbuka kilichomtokea kwenye simu ambacho bado amekiweka kama siri moyoni mwake lakini sasa alijiridhisha kuwa yawezekana sio simu kama iliyomsumbua yeye.
Baba pachu alimaliza kuoga akajiandaa na kumwanga mama pachu kuwa anatoka kwenda kwa mwakibubu na kuwa angerudi kwa kuchelewa kidogo na baada ya hapo akaanza safari ya kwenda hotel ya msufini.
Robo saa baadae alikutana na mwakibubu na wakanza kutaniana, " aisee unajua wakati umetumiwa ile meseji na mimi nilipigiwa ila hata kabla ya kuiona namba simu yangu ilianguka na kutoka betri na mbaya zaidi hata nilipoiwasha sikuweza kupata kumbukumbu ya namba hiyo na kama haitoshi huyo mpigaji hajapiga tena na sijui ni nani na alitaka nini maana kama ni chamdoli angeshanipigia.... ila wewe mzeee ulilegea ha ha ha ha kama mlenda songea ..." alimaliza bwana mwakibubu
"Kaka huyu chamdoli kuniita mpenzi sio jambo la masihara, hebu fikiri mtu humfahamu na cha kutisha zaidi hujui ni nani na hata akisema akuchukue mpenzi wake mtaenda dunia gani.. kaka huwezi amini nilishikwa na tumbo la kuhara baada ya wewe kuondoka pale home" aliongea baba pachu
"Sasa kaka tufanyeje ili huyu mtu tumshinde maana yale maazimio ya kwanza yalikula kwetu, kwani mpaka muda huu kuna bar tunadaiwa, gari liko polisi na kama haitoshi kazi hatuna yaani sisi ni majobles fulani hivi" aliongea mwakibubu huku akitikisha kichwa kuashiria kuumizwa na hali hiyo
Kaka mimi nina wazo nafikiri kuanzia sasa tuwe karibu sana na kama haitoshi kila mtu akipigiwa simu jambo la kwanza ni kumpigia mwenzie na kushirikishana na ninafikiri tunatakiwa kupata ufumbuzi wa ziada ikiwa ni pamoja na kutafakari kwa kina njia mbadala za kumshinda huyu mtu haiwezekani sauti ya binti itusumbue, kwanza hebu tupige simu huduma kwa wateja na kuuliza kama namba hii imesajiliwa kwa jina gani na yupo mkoa gani" alishauri baba pachu
"Wazo zuri sana baba pachu ndio maana huwa nakufagilia maana nyakati za shida wewe huwa haukosi neno lenye kuleta ufumbuzi" aliongea mwakibubu huku akiinyanyua simu na kupiga namba ya huduma kwa wateja ambayo haikupatikana muda huo
Akiwa bado kashika simu mkononi, mara simu yake iliita na bila kuangalia akanyanyuka na kumwomba rafiki yake kuwa anaenda kuipokea atarudi huku akiwa tayari kaipokea na ipo sikioni.
" Hujambo mwakibubu, naona leo milikuwa na furaha sana na rafiki yako ila nataka kukutahadharisha kuwa huyo rafiki yako sio mtu mzuri kwani anataka kukuua ili akufanye wewe msukule wa kujipatia yeye hela, si unajua hana kazi?, sasa akili kichwani mwako" aliongea chamdoli na kukata simu bila kumpa nafasi ya kuongea mwakibubu.
"Aisee unajua huyu chamdoli unaweza kuwa unamkimbia kumbe ni mtu wa ukweli sana maana anaweza kukuokoa. Lakini kweli mbona baba pachu siku hizi kazidisha mapenzi kwangu, ok ok ok ngoja ndio maaaana siku ile ajali ilitokea!!!!!!!
Atakuwa alitaka kunifanya msukule... duh ulimwengu huu usimwamini mtu yoyote hata awe nani...... duuuuh nimekoma!!!!! Asante CHAMDOLI NAKUPENDA SANA ILA SIO KIMAPENZI MAANA HUELEWEKI, HUKAWII KUBADILIKA" alimaliza kuongea bwana mwakibubu huku akiingia ndani kwa mwendo wa shari
Alifika mezani na kuchukua funguo zake za gari bila ya neno lolote kwa baba pachu na kuondoka kwa haraka eneo hilo akimwacha baba pachu akishangaa na kumwita kwa sauti ya mshangao kaka! kaka! kaka! mbona hivyo?
Lakini sauti hiyo haikusaidia chochote kwani mwakibubu aliingia kwenye gari na kuondoka kwa haraka eneo hilo kama vile alikuwa katika mashindano ya magari.
Baba pachu aliingia ndani na kulipa bili kisha akaamua kubadili eneo huku akijaribu kumpigia mwakibubu ambaye hakuipokea simu yake na badala yake aliizima simu kabisa jambo lililomchanganya zaidi baba pachu.
Mawazo yalikuja kumkata baada ya kuona kibao cha Hodari Pub ambapo alisimama na kuagiza wine na kukaa sehemu tulivu akiwa peke yake. zilipita dakika kadhaa akiwa kwenye dimwi zito la tafakari juu ya kitendo kile cha bwana mwakibubu kabla ya simu ya chamdoli kumshutua.
Alisimama na kujivuta mpaka kwenye gari na baada ya hapo alimsikiliza chamdoli, " Sikia baba pachu, unajua mwakibubu ana mpango wa kutembea na mke wako?
Na pale hotelini aliondoka haraka baada ya mama pachu kumpigia simu? Na unaona siku hizi jinsi ambavyo mwakibubu anashinda kwako? Basi kaa chonjo sio siku nyingi utalizwa" alimaliza kuongea chamdoli na kukata simu.
Baba pachu wakati huu hakuongea neno zaidi ya kutoka eneo lile na kuelekea nyumbani kwake. Alipokaribia na nyumbani kwake alisimama kwa mbali na kushuka kwenye gari lake ili atembee taratibu na kwenda kumfumania rafiki yake wa karibu ambaye sasa alimbatiza jina la mgoni wake.
Alipofika karibu na nyumbani kwake alinyata na kutembea taratibu kwa tahadhari ya kutomkurupusha mgoni wake huku akiwa na kitu kizito mkononi mpaka dirisha la chumbani mwake na kusikia minong'ono ya watu wawili wakisema , vua haraka niakuogeshe si unajua nimechoka???
Baba pachu ali........................... ................
Usikose mwendelezo kisa hiki jumatatu jioni
TUNAKUTAKIA WEEKEND NJEMA
MUHIMU
Neno kutoka kwa mdhamini
Gracious HOUSE of CAKES tunakukaribisha Forest ya zamani.. nyuma ya Green lounge pembeni ya Penge kwenye duka letu. utajipatia Cakes za kila aina. Magic popcorns na suprises cup cakes. tunapokea oda hata za mwakani sababu tanapenda kufurahi na wewe. tunaanda bday party kwajili ya watoto na hata watu wazima kwa bei nzuri tuu.. kaa hunanafasi yakuja pia usipate mawazo sababu tunakuletea utakacho mpaka ulipoo. KARIBUNII SAANAA.
KUMBUKA
Kama unataka kusoma visa vya mwanzo tafadhali tuma Simu ya Ajabukwenda whatsapp namba 0713317171
Share, like Simu ya Ajabu na comment ili kisa kingine kiwahi kuletwa
OMBI
Unaweza kuwa nawe mdhamini wa simulizi hii tamu kwa kuwasiliana nasi kwa kuandika neno UDHAMINI kwenda whatsapp namba 0713317171
MUHIMU
Neno kutoka kwa mdhamini
Gracious HOUSE of CAKES tunakukaribisha Forest ya zamani.. nyuma ya Green lounge pembeni ya Penge kwenye duka letu. utajipatia Cakes za kila aina. Magic popcorns na suprises cup cakes. tunapokea oda hata za mwakani sababu tanapenda kufurahi na wewe. tunaanda bday party kwajili ya watoto na hata watu wazima kwa bei nzuri tuu.. kaa hunanafasi yakuja pia usipate mawazo sababu tunakuletea utakacho mpaka ulipoo. KARIBUNII SAANAA.
KUMBUKA
Kama unataka kusoma visa vya mwanzo tafadhali tuma Simu ya Ajabukwenda whatsapp namba 0713317171
Share, like Simu ya Ajabu na comment ili kisa kingine kiwahi kuletwa
OMBI
Unaweza kuwa nawe mdhamini wa simulizi hii tamu kwa kuwasiliana nasi kwa kuandika neno UDHAMINI kwenda whatsapp namba 0713317171
0 comments: