HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU " 54
HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
54
ILIPOISHIA JANA
Wakati baba pachu na mwakibubu wakiwa njiani kumpeleka mama pachu hospitali huku nyuma bibi gusa unate na nesi mwalikumba nao waliondoka na kuachana. Nesi mwalikumba yeye alirudi nyumbani huku bibi akirudi hotelini kwake.
" Oyaaa wee mhudumu nilitee vyombo maana i had a very rough day....... am real tired.... give me something strong" ilikuwa ni sauti ya bibi ambaye alikuwa akiomba vinywaji
Ilikuwa ni saa kumi na mbili na nusu za jioni na nyumbani kwa baba pachu walionekana...............
MWENDELEZO
Ilikuwa ni saa kumi na mbili na nusu za jioni na nyumbani kwa baba pachu walionekana watu wawili wakiwa wamesimama na wamevalia makoti marefu meusi kama vile majasusi.
Wakati huo baba pachu na mwakibubu walikuwa wametoka hospital na kuamua warudi mara moja ili baba pachu achukue kadi ya bank akachukue fedha za kununulia baadhi ya vitu vya kumpelekea mama pachu ambaye aliachwa hospitali chini ya uangalizi maalamu kwani alikuwa bado hajitambi na wala hajaonesha dalili za kuamka.
Baba pachu alipokaribia kufika nyumbani alishtushwa na watu wale pale mlangoni kwake wakiwa wamevalia magwanda yaliyoashiria shari.
Akashuka na kumwacha mwakibubu akiwa ndani kisha akawasogelea na alipojaribu kuwasemesha hakuna aliyejibu akataka kupiga simu polisi na mmoja wao akaanza kwa kusema
" ndugu sisi hatuna shida na wewe tunamataka huyo mama pachu atoke huko ndani kwani tumeambiwa anakaa hapa na tunshangaa kila tukimgongea hafungui mlango zaidi ya mtoto mmoja kuja na kutuambia mama hayupo na nimempigia simu hata kabla ya kumaliza kuongea kazima kwa makusudi" alimaliza kuongea mmoja kati ya watu wale wawili ambaye koti lake na mavazi aliyoyavaa yalimfanya aonekane kama kijana wa makamo.
" ndugu yangu mke wangu amelazwa na sisi tunatoka hospitali kwani ana nini na nyie mpaka muwe na hasira hivi???"
" Tunaondoka kwa kuwa umethibitisha kuwa anaumwa ila mwambie kuwa ndugu yako amesema atakuja tena" alimaliza mzee tobo bao na kuondoka
Wakati wanaondoka kina tobo bao mwakibubu naye alikuwa ameshashuka na kumsogelea baba pachu ambaye alikuwa kajinamia chini huku akijiuliza kulikoni mke wake akaanza kuwa na mikwaruzano na hawa watu wanaojiita ndugu zake na simu ile ilikuwa na nini? na kwanini alipompigia Munu naye alikataa kabisa kumsaidia tena baba pachu?"""
" kaka mbona umewaacha hao jamaa bila jua wana nini na mama pachu inawezekana wakawa na ajenda ya siri iliyomfanya mama pachu azimie baada ya kuipokea ile simu"
kaka umenena" aliongea baba pachu huku akiwakimbilia kina tobo bao ambao walikuwa wameshafika mbali na wameshachukua bodaboda na kushindwa kuonana nao tena.
"kaka nimewakosa wameshaondoka, hebu tuondoke zetu nipe dakika nikachukue kadi na kumcheki pachu tuondoke zetu" aliongea baba pachu huku akiingia ndani na baada ya muda mfupi akatoka nje na wakaanza kuondoka kuelekea mjini baada ya kuweka mambo sawa pale nyumbani.
Baada ya mizunguko kadhaa wakaishia hospitali na kumwona mama pachu bado akiwa hajitambui kabisa. Walimkabidhi mizigo nesi yule na wakawa wanajiandaa kuondoka kabla ya daktari kumwita baba pachu ofisni kwake
" baba pachu pole sana na matatizo naona asubuhi ilikuwa ni ndugu yako na rafiki yako na sasa mke wako .... je kuna tatizo lolote linalowakabili wewe familia yako na ya rafiki yako??? maana mama pachu mara ya mwisho alilazwa hapa kwa mshtuko na sasa ni mshuko pia kuna nini?"
" Kiukweli mpaka sasa nipo gizani ila nami nalifanyia uchunguzi wa chinichini", alimaliza kuongea baba pachu huku akiagana na daktari huyo baada ya kumalizia malipo ya awali aliyohitajika kulipa na kisha akaondoka na mwakibubu.
Walifika mpaka nyumbani kwa mwakibubu na baada ya kuagana baba pachu aliondoka na kwenda zake nyumbani ambako aliishia kukaa sebuleni kwake kwa muda akiwa kaishiwa nguvu na baada ya kuhakikisha watoto wamelala naye akarudi tena pale sebuleni na kuanza kunywa pombe akiwa na mawazo.
Nyumbani kwa mwakibubu mambo hayakuwa safi kabisa kwani mama amigo alijikaza na baada ya kuona uvumilivu unamshinda akamwomba mmewe amwambie nini kinaendelea kwani tukio la yeye kutaka kujiua kwa kujinyonga, lile la bibi na nesi kuhusu chamdoli na tukio la mwisho la mama pachu kupigiwa simu na akazimia yote yalimfanya azidi kuchanganyikiwa.
Mwakibubu hakuwa na la kusema zaidi ya kulia jambo lililomfanya mama amigo naye ajikute akiachia kilio cha chinichini na baadae nyumba nzima iligeuka na kuwa na vilio kwani amigo alianza kulia baada ya kumwona baba akilia na baadae mtoto mdogo nae akalia kwa sauti kuu jambo lililoifanya nyumba hiyo iwe na huzuni na baadae wote waliishia kulala.
Asubuhi sana mama pachu alizinduka pale hopsitali na akasimama na kujitoa baadhi ya plasta za drip zilizokuwa mkononi na kwenda uani na aliporudi akachungulia kupitia dirishani na kuona nesi akiwa amelala na akajivuta mpaka nje.
Ulipita muda zaidi ya saa moja mama pachu akiwa hajaonekana pale ndani na muda huo baba pachu alikuwa ndio anaingia akashangaa kuona daktari na manesi wakiwa wamejikusanya wakiwa katika taharuki kuu ndani ya chumba cha mama pachu.
" Samahani baba pachu, mama pachu hatujui kaenda wapi na tumejaribu kumcheki kila sehemu hatujui nini kimetokea, na inavyoonesha atakuwa katoroka kwani kaondoka na mkoba wake" aliongea daktari huku akimsihi baba pachu kutulia.
" Mungu wangu kuna nini kinaendelea ?" alihoji baba pachu huku akielekea ofisini kwa daktari mkuu wa hospitali hiyo na kisha wakaondoka kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi.
Mama pachu alifanikiwa kutoka katika eneo hilo la hospitali na kuchukua bodaboda iliyompeleka mpaka nyumba moja bubu ya kulala wageni na kukaa kwa muda kabla ya chamdoli kumtumia ujumbe ukisema, " kukimbia mtatizo sio dawa ya matatizo... sasa nataka kukupa msaada hivyo nitakupigia na kukupa tarehe ili siku hiyo uwe hilo eneo na nikupe msaada wa kujinasua"
Baba pachu akiwa njiani na daktari kulekea kituoni kutoa taarifa za kupotea kwa mama pachu mara simu yake ilipigwa na alipogundua ni namba ya chamdoli akasimamisha gari na kushuka kisha akaipokea, " usihangaike kumtafuta mkeo mimi najua aliko wewe hakikisha unamtafuta yule mtu aliyekuja jana usiku ukae nae chini ana kisa kizima juu ya matatizo ya mkeo"
Alipomaliza kuisikiliza simu aligeuza gari na kumshusha daktari pale hospitali na kumwacha akiwa ameduwaa na baada ya muda mfupi alikuwa kafika nyumbani kwa mwakibubu.
Alipofungua mlango wa sebuleni alishangaa kuona mwakibubu akiwa kalala kwenye kochi yeye pamoja na mkewe huku mtoto wao mdogo akiwa anacheza peke yake kwenye kitanda chake pale sebuleni huku amigo akiwa pembeni akimwangalia..
Aliwaamsha na kuwasalimia na kwa uchovu wakaamka na baada ya kuamka akamvuta mwakibubu nje na kumpa mkasa mzima wa hospitali na juu ya ile simu ya chamdoli na hapo wakaanza kuliwasha gari kuelekea mjini waweke mafuta na kuanza kazi za kuwatafuta wale wageni wa jana yake jioni bila hata ya mwakibubu kujiandaa.
Walipotokezea barabara kuu ya kwenda mjini walishangaa kuona watu wengi wakiwa wamesimama wamelizingira gari moja na waliposimama na kulisogelea kundi hilo la watu baba pachu aliishiwa nguvu baada ya kuona ni ajali iliyotoa uhai wa watu na mmoja wao kati ya hao waliogongwa akiwa ni.............
JE UNAHITAJI NAKALA YAKO YA SIMULIZI HII?
AU
UNGEPENDA JINA LAKO LIONEKANA KATIKA KITABU CHA SIMU YA AJABU NA SIKU YA UZINDUZI UWEPO?
WASILIANA NASI KWA WHATSAPP 0713317171
0 comments: