Kamwe usimjaribu MUNGU kwa hajaribiwi
Miaka mingi iliyopita mfaleme mmoja alikuwa na mtumishi wake ambaye alibahatika kuwa mcha Mungu sana.
Lakini mfalme huyo alikuwa haamini kabisa kuwa kuna Mungu zaidi ya miungu yake aliyokuwa akiiabudu.
Alichukizwa sana na mtumishi huyo hasa alipokuwa akilitaja jina la Mungu kila aliposhukuru au kutaka kuomba ulinzi wa jambo fulani.
Taratibu yule mtumishi akaanza kumwelezea mfalme huyo juu ya Mungu wa kweli lakini mfalme alikuwa mkali na hata kumpa adhabu kali.
Siku moja wakawa wameenda kuwinda na walipokuwa huko waka koswakoswa kuuawa na nyati na yule mtumishi akaanza kusali akimshukuru Mungu lakini mfalme alichukizwa zaidi Na kumwambia mtumishi huyo kuwa Mungu hajahusika hapo zaidi ya wao kuwa hodari wa kukimbia na wakarudi nyumbani.
Siku nyingine wakiwa wanawinda mara simba akatokea na kumdaka mfalme na yule mtumishi akafanikiwa kumuua yule simba ingawa mfalme alijeruhiwa kidole chake kimoja cha mkononi na kuvunjika.
Mfalme akachukia zaidi kwa jinsi mtumishi huyo alivyokuwa mzembe wa kumwokoa mpaka akaliwa kidole, lakini mtumishi akasali kushukuru kuwa mfalme haku uawa.
Waliporudi nyumbani mfalme akaamuru mtumishi huyo afungwe gerezani baada ya kusababisha uzembe uliotaka kuhatarisha maisha ya mfalme na kweli mtumishi akafungwa gerezani
Siku nyingine mfalme akaenda peke yake mwituni kuwinda na alipofika huko akakamatwa na watu amabo huwashika watu na kuwatumia kwa ajili ya sadaka za miungu yao kama sala zao.
Kwa mara ya kwanza mfalme yule akasema Mungu wangu naomba niokoe na walipofika watu wale sehemu ya kutolea sadaka mfalme aliachiwa huru kwa sababu hakuwa na viungo vyote yaani hakuwa timilifu kwani kidole mkimoja hakuwa nacho.
Mfalme aliporudi akaamuru yule mtumishi afunguliwe na alipoletewa akamwambia, " Ndugu unajua leo nilikamwatwa na watu porini nikiwa nawinda na wakanipeleka mpaka kwenye sehemu ya kutolea sadaka yao na miungu yao ikanikataa kwa kuwa sikuwa na kidole kimoya yaani sikuwa kamili ni kama kilema sadaka isiyo kamili, hakika nimeamini Mungu wako ana nguvu"
"Mfalme wangu, nilikuambia kila kitu kinatokea kwa sababu na Mungu hujua yote haya, maana leo usingekuwa umenifunga tukaenda wote mimi ndio ningetolewea sadaka"
Kila kitu hutokea kwa sababu
Comment AMEN kwa kumshukuru Mungu kwani unaamini kila kitu maishani huja na sababu maalumu na Mungu ndiye mlinzi wetu.
0 comments: