Kuna haja ya kuisoma hii na kuhakikisha tunampa adhabu mwandishi wake... kaniboa sana

12:14:00 Unknown 0 Comments

Nilichelewa sana kuamka siku hiyo na moja kwa moja nikakimbia mpaka ofisini kwangu nilikoajiriwa hata bila ya kujiandaa vizuri.
Nilipofika pale nikakutana na mmoja wa wasaidizi wangu akiwa kainamisha kichwa chini kuashiria kuwa kuna jambo baya au la sgari lilikuwa limetokea.
Baada ya kumhoji aliniambia kuwa ni secretary wangu akutwa amekufa ofisini bila hata ya kuuliza zaidi niliingia na kuona akiwa amelala juu ya meza yake.
Nikarudi nje haraka na kutuma watu waende polisi ambako baada ya kuja na kufanya uchunguzi baadae waliruhu mwili wake upelekwe mochwari na taratibu za mazishi zianze.
Nilipewa jukumu la kuhakikisha nakuwa msimamizi wa shughuli za mazishi nikiiwakilisha ofisi yetu pale msibani.
Siku tatu baadae nikiwa ofisini niliambiwa kuwa nilihitajika kwenda kituo cha polisi kwa ajali ya mahojiano kidogo.
Nilinyanyuka na kuelekea huko bila kutambua hasa ni nini nilitakiwa kwenda kutolea maelezo au hayo mahojiano yalihusu nini.
Sikuamini kuanza mahojiano na kugundua kuwa nami nilihusishwa katika kifo cha yule secretary. Kiukweli nilichanganyikiwa na baada ya hapo nikawekwa ndani.
Nikawasiniana na  wakili wangu na kumwomba anisaidie baadhi ya vitu ikiwa ni pamoaja na kumsaidia mke wangu arudi kwa mama na mimi na wakali tupigane kuokoa uhuru wangu.
Ilinibidi nimrudishe mke wangu kijijini ili asaidiwe kwani alikuwa na tatizo la athma ambalo lilikuwa likimsumbua mara kwa mara na kuonekana kuwa sugu na kukua zaidi.
Ilichukua zaidi ya miezi tisa kabla ya kuachiwa huru kupitia jitihada za wakili wangu bwana zedekia na sasa nikajikuta nikiwa mtaani tena.
Ofisini nilishasimamishwa na kugundua kuwa ilikuwa ni mchezo mchafu uliofanywa na mmoja wa marafiki zangu wakubwa bwana majaliwa.
Maisha yalikuwa magumu sana kwani nilimchukua mke wangu kijijini na kuanza maisha mapya tukiwa kwenye chumba kidogo cha kupanga.
Nilianza kuzunguka na bahasha mkononi nikitafuta kazi upya na kama haitoshi nilitakiwa kuwahi kurudi nyumbani kumpikia chakula mke wangu kwani hakutakiwa kupatwa na moshi kutokana na tatizo lake la athma.
Hali ilizidi kuwa ngumu zaidi na  ikafikia wakati nikaanza kuona kila dalili za kukatishwa tamaa na kufikiri kurudi nyumbani tena kijijini kwetu kabisa kwa baba na mama.
Hakuna siku niliyowahi kuumia kama siku niliyopatwa na tatizo la mke wangu kuzidiwa na athma na kufika katika dispensary na kukosa huduma kisa sikuwa na fedha.
Nilikimbia usiku ule mpaka nakuja kupata fedha ilikuwa ni mida mibaya na mke wangu alikuwa kachoka sana baada ya matibabu.
Nililia sana usiku ule na kumuuliza Mungu ni kwa nini aliniacha na kupitia hatua hiyo. Hata kama ningebakia kuwa maskini ila asingemuacha mke wangu ateseke vile kwa kweli nililia.
Siku chache baadae niliamka na kwenda katika pita pita zangu na mida ya saa nne nilipiwa simu na kampuni moja na kuambiwa kuwa nilipita katika usaili na kuwa natakiwa kwenda kuanza kazi.
Sikuamini macho yangu na kurudi nyumbani ili nimsimulie mke wangu kwani ilikuwa ni habari njema sana kwetu.
Nilifika pale getini na kukuta geti limefungwa na haikuwa kawaida ya nyumba ile kufunga geti kuu. Nikagonga kwa muda lakini hakukuwa na mtu aliyefungua niakaamua kukaa pale kusubiri mtu atakayekuja anifungulie.
Kumbe wakati nasubiri pale mke wangu mle ndani alikuwa kaamua anisaidie kupika na kwa bahati mbaya moshi ukamsababishia athma ipande.
Nilikaa pale nje na baada ya muda mfupi akaja binti wa chumba cha jirani na kulifungua geti kwani alilifunga mara moja ili aende mashineni.
Naingia ndani nakuta mke wangu akiwa ana tapatapa huku akiwa hana msaada na jikoni vitu vikiwa vinaungua.
Nilimnyanyua kwa haraka na kumsaidia kumpa msaada wa dawa yake na baada ya kuona hakuwa akipata ahueni nikatafuta usafiri niende nae hospitali ambapo alifia mikononi mwangu nikiwa njiani.
Nililia sana na kujitupa chini kabla ya kuamka asubuhi hii na kugundua ilikuwa ni ndoto na muda huu sasa najiandaa kwenda kazini

You Might Also Like

0 comments: