Kwa wale mabingwa wa viteteo hii inawahusu
Kuna baadhi ya sababu au viteteo katika maisha ni vya kweli na vinakubalika wakati vingine ni michezo ya kipuuzi ya kukupotezea muda wako.Na kumbuka kuna wakati ambao kamwe huwezi tena kuja na aina mpya ya sababu au kiteteo na kikakubalika kwani wakati na ukweli vinakuwa vikikuumbua.
Kwa maneno mengine utajikuta ukikwama kusonga mbele bila sababu yoyote ya msingi kutokana na muda ulioupoteza hapo awali.
laikini iwe ni kwa sababu au kiteteo cha msingi, kiteteo kibaya au hata bila ya kiteteo ,leo hii jaribu kuikamata fursa iliyopo mbele yako na kuipa kipaumbele.
Songa mbele bila kukaribisha sababu au viteteo hata viwe vya msingi au visivyo vya msingi, wewe achana navyo na jaribu kuyaboresha maisha yako kwa kuyapa changamoto za kusonga mbele zaidi ukikamata fursa mpya kila siku.
Hatua moja ndogo ya leo ni faida kubwa kwa kesho yako
Fred Kihwele
0713317171

0 comments: