Mmiliki wa blogu hii afilisika na lawama zote awapelekea wasomaji wake

06:11:00 Unknown 0 Comments

Habari zilizotufikia hivi punde zinadai mmiliki wa blogu hii na mwandishi wa kitabu cha BOMASimu ya Ajabu na lango la Motoni bwana fuledi amefilisika kiasi cha kushindwa kupata muda wa kuiendesha blogu hii pamoja na mafuta ya kumwezesha kufika ofisini kwake  au hata zile za kuzunguka mitaani ili apate habari na mikasa inayoisibu jamii yetu na kuweza kuwahabarisha wasomaji wake.

Haya yamedhihiirishwa jana jioni ambako kamera zetu zisizo na mipaka zilipomfuma akinunua mafuta ya gari kiduchu kama vile alikuwa ana nia ya kwenda kuiwasha bajaji. 

Alipokutana na kamera hizo pamoja na jitihada za kukimbia hatimaye ilimbidi atulie na kuwa mpole ili nae ageuke kuwa habari





Pichani ni bwana fuledi akipokea mafuta ujazo wanusu lita

Hapa bwana fuledi anaonekana akiweka mafuta kwenye gari lake ambalo alijitahidi kulificha lisipigwe picha


Kilichohuzunisha zaidi ni kwamba bwana fuledi yeye kila alipohojiwa alidai kuwa hali imezidi kuwa ngumu mwaka huu kutokana na wasomaji wake waio wengi kutoa ahadi feki za kununua kitabu chake cha BOMA ambacho kina hadithi nzuri na zenye mafunzo mazuri kwa jamii yetu kinachouzwa kwa gharama nafuu sana shilingi 5000 tu na badala yake wasomaji wengi wamekuwa wakipiga simu na kuulizia tu.

Aliendela kudai kuwa hapo awali kitabu kilipozinduliwa alipata fedha nzuri zilizomfanya aweze kuishi maisha mazuri kwa muda lakini kwa kutokuwa makini na suala la bajeti pia imemkosti na kumfanya sasa aishi kwa mafuta ya kidumu kama dereva daladala.

Pichani ni bwana fuledi enzi zake akila bata wakati mauzo yalipokuwa juu.


Fuledi alimalizia kwa kuwaomba marafiki wazidi kujitokeza kwa wingi kununua nakala ya kitabu cha BOMA ambacho kinapatikana sehemu mbalimbali hapa nchini na pia kwa kupiga nmba 0713317171 au 0684868191 ili kuweza kuokoa kipaji cha kijana mwenzetu ambaye ana safari ndefu sana katika kukionesha kipaji chake,

Nakala ya kitabu cha BOMA

simu
Nakala ya kitabu cha Simu ya ajabu

Nakala ya simulizi ya Lango la motoni

Pia kitabu hiki kinapatikana kupitia tovuti ya karibu mbeya


Ujumbe aliouandika katika akaunti yake ya facebook


Fred Kihwele added 2 new photos.
10 hrs · 
Shkamoo 2015 naona mbwembwe zako zimeanza mapema
Like ·  · 

You Might Also Like

0 comments: