SAMAHANI KWA HII POST

09:27:00 Unknown 0 Comments



Hivi karibuni nimejaribu kufanya utafiti mdogo wa kawaida sana usio hitaji elimu kubwa sana kupitia hapa facebook juu ya mahusiano na kujifunza mengi sana.

Mimi hapo awali nilikuwa mmoja wa walioamini kuwa wanawake wote duniani ni sawa na kuwa wanatabia sawa, lakini nimekuja kujifunza kitu kikubwa sana kwangu.

Swali langu lilikuwa ni kwa nini mahusiano mengi ya sasa hayadumu na hata kama yanadumu basi jua kuna mengi ambayo wapenzi hao wanayapitia chini ya kapeti.

Amini usiamini nimegundua kuwa asilimia kubwa ya wanaume ndio chanzo cha mahusiano hayo kutodumu, na nikaainisha kama ifuatavyo.

Mwanzo wa mapenzi: Ikumbukwe kuwa kwa utamaduni wetu mwanaume ndio huwa mtu wa kwanza kumfuata mwanamke na inasadikika kuwa wanaume sio humtamani mwanamke na kumshawishi. Wakati huo mwanamke yeye huwa hana mguso wowote wa wazi na baada ya kutembea nae na kukaa nae ndipo naye sasa huanza kukupenda kwa dhati yaani wao huchukua muda kidogo.

Sasa wakati wa mwanzo mwanaume huficha uhalisia na kuwa na tabia ambazo zinaridhisha na kumshawishi binti ampende zaidi lakini muda unapozidi kwenda zile tabia asilia za mwanaume hujiachia na kumfanya mwanamke ajue rangi kamili ya mwanaume huyo na hapo sasa mambo huanza kwenda tofauti kwani mwanamke hujikuta yupo na mtu ambaye hakumtarajia.

Mitazamo yetu wanaume: Kwa sasa wanaume wengi tumekuwa tukiandika juu ya mwanamke tunayemtarajia katika maisha yetu na kwa kufanya hivyo tumewafanya wanawake nao wapritend kuwa na mitazamo au tabia tuzitakazo ili waolewe lakini ndani wanakuwa sio, hivyo tabaia zao halisi zinavyoanza kuchomoza basi wengi wetu huanza kuona tuko na watu wasio sahihi.

Kutokuwa na uvumilivu: Baadhi ya wanawake wamejikuta katika nyakati ngumu ndani ya mahusiano yao, kwani pindi mtu anapokosa kidogo basi mwanaume anaweza mkaripia sana, kumnunia hata kwa wiki kadhaa, kumkumbushia makosa ya zamani jambo ambalo limewafanya wanawake wengi kushindwa kuvumilia hali hizo na kuona ni bora wachukue njia nyingine ya kuwapa furaha.

Ubinafsi: wanaume wengi tumechukua kigezo cha maisha kuwa magumu na kujikuta tukisahau kuwa vile vile tuna haja ya kuwapa furaha wenzetu ambazo sio lazima zitumie gharama kubwa. Mfano kutenga muda wa kuwa na mwenza kumpa vijizawadi vidogo au hata surprises ambazo hazitagharimu kitu zaidi ya kuacha kumbukumbu ya furaha na kupalilia upendo baina yenu. Zawadi hata ya shilingi 2000 kwa mwanamke ina maana kubwa sana kuliko kumpa gari kama imetoka kwa upendo, unakuta umekaa na mtu kwenye mahusiano kwa zaidi ya miaka hata hata hujui anasukaje, nguo hata ya ndani wewe kumnunulia unashindwa kasha ubahili.

Usiri: idadi kubwa ya wanaume sio wasiri na hili ni tatizo kubwa kwani jambo dogo tuu umeshakaa na rafiki wa mkeo au rafiki zako na kuwashirikisha wakati ni suala la wewe na mpenzi wako… Utamu wa mapenzi ni pamoja na kutatua matatizo yenu wawili bila ya kualika jamii kuwa mashaidi

Matarajio: Zamani ilikuwa ni rahisi kuwatupia mpira wanawake kuwa wanaolewa au kuwa kwenye mahusiano wakiwa na matarajio Fulani, lakini hata sasa kuna wanaume wanao au kuwa na wapenzi kwa ajili na lengo Fulani. Mfano kuna watu wanaingia kwenye mahusiano kisa maisha magumu sasa wapate sehemu ya kujibana kwa muda huku wakiangalia uelekeo na pndi matarajio yao yakitimia basin a mahusiano ndio bai bai

Suala jingine ni kuwa huu utafiti ni feki na hauna maana yoyote tafadhali futa comment yako

www.karibumbeya.com

You Might Also Like

0 comments: