usisome haikuhusu
Siku moja jioni majira ya saa kumi na moja marafiki watatu wakaao nyumba moja waliamua watoke kidogo.Wakatembea umbali mrefu kwa miguu huku wakifurahi na kubadilishana mawazo kwa furaha na mwishowe kuishia sehemu ambako wakapata chakula cha pamoja na kisha kurudi nyumbani.
Huko nyumbani wakakutana na wanafamilia wengine na kuongea kidogo mpaka muda wa kulala ulipotimia na kisha kwenda kulala.
Usiku ule mdogo wao wa kike ambaye ni mwanafunzi wa chuo fulani akaona ni vyema aandae chai na vitafunwa kwa ajili ya kesho yake.
Akawasha jiko la mkaa na kuweka ndani na kabla ya kufanya chochote usingizi ukamwelemea na kulala.
Kwa kuwa mkaa mbichi hutoa moshi wenye sumu, usiku ule wale vijana ndani ya ile nyumba walikosa hewa na siku ya pili yake baada ya majirani kuona ukimya usio na kawaida wakavunja mlango na kuona wakiwa taabani baada ya kukosa hewa usiku ule na kuwakimbiza hospitali.
Wakiwa njiani wale vijana wakakata roho na mmoja akafanikiwa kufika hospitali na baada ya matibabu ya siku kadhaa akapona na kuwa mzima.
Wakati akitoa ushuhuda jinsi alivyopona pona alisema, "Kabla ya kulala niliomba kwa Mungu kuwa naikabidhi nafsi yangu mikononi mwako, naikiwa nitakufa usiku huu naomba uipokee nafsi yangu"
Akaendelea kusema, "Usiku ule wakati nahisi kukosa pumzi na nguvu ghafla nilimwona mtu nisiyemfahamu wala kumfananisha akinipepea na kuniambia utapona tu mwanangu, Naamini mtu huyo si mwingine bali ni Mungu"
Ndugu zangu, ni wangapi ambao tunalala na kuamka bila kumshukuru Mungu na kuomba ulinzi wake?
Umeshajiuliza ni magapi yanaweza kutokea ukiwa usingizini na ukafa bila kujijua?
Je unaiamini mifumo ya umeme, gesi uitumiayo au hata mafuta ya taa au gari yako yenye mafuta ya hatari kulipuka ndani ya nyumba yako?
Una kila haja ya kumshukuru Mungu wako kila wakati na kuomba ulinzi wake katika maisha yako.
Vijana wale waliagana kuwa tutaonana kesho na mipango mingi mbele yao bila kujua Mungu ndio mwenye funguo za kesho.

0 comments: