Nalijutia sana hili
Baada ya harusi mimi na mke wangu tukakubaliana kila mmoja arudi kazini kwake na kuendelea na kazi huku tukitafakari wapi tuweke kambi.
Kwa bahati mbaya wote tulikuwa waajiriwa hivyo ikawa haina jinsi zaidi ya kuendelea kuzitumikia kazi zetu huku tukiangalia njia rahisi ya kuja kuishi kwa pamoja huko tutakapoamua kuishi.
Maisha yalianza kwenda vyema na karibia kila mwisho wa mwezi tulilazimika kutembeleana ili mahusiano yetu yazidi kujengeka.
Kwa kuwa mimi napenda sana kujumuika na marafiki zangu katika vikao vya pombe na pia mke wangu anapenda mitindo basi tukaamua yeye awe na boutique moja kubwa pale mjini na auze nguo za aina mbalimbali na kubuni mitindo ya mazazi na kujipatia fedha.
Na mimi nikafungua bar moja kubwa yenye kutoa kuduma nyingi na wateja wakawa wengi hali iliyonifanya nami kuwa na kipato cha kutosha kuendesha maisha bila ya kutegemea mshahara pekee hali kadhalika na mke wangu biashara ikawa njema na maisha yakenda vyema.
Mipango ikaendelea kwenda vyema na utaratibu wetu wa kutembeleana ukaendelea na kila mmoja wwtu alipoata likizo alihakikisha anaimalizia kwa mwenzake na mwaka mmoja baadae tukawa tumefanikiwa kuanza ujenzi wa nyumba yetu huko dar ambako tul;ifikiri tungeenda kushi baada ya mambo kukaa sawa.
Kuna kitu kikaanza kwenda vibaya na nakumbuka kuna siku kwa hasira nilimpiga sana mke wangu nilipoenda kumtembelea. Kwani mara zote namkuta na kina mama mashangingi wa mjini ambao kwa namna moja au nyingine nikahofia kuwa wangeweza kumharibu mke wangu naye akaanza kuwa na mabwana pale mjini.
Nilimpiga hasa baada ya kunijibu kuwa hawezi kuwaacha kwni wanamsaidia sana kwenye mambo yake na pia yeye ni mtu mweye kujielewa na kujiheshimu jambo ambalo kwangu niliona ni kama dharau tosha.
Ugomvi ukaendelea kwani naye alipokuja kunitembelea hakupenda tabia ya mimi kubaki bar mpaka usiku wa manane nikiwa na marafiki na pale bar kuna wanawake wazuri waliokuwa wakihudumia hivyo akawa na wasi wasi wa mimi kuwa ningeweza kuwa na tabia za kutembea nao .
Maisha sasa yakawa ya kuwindana na kuviziana kuwa na safari za kutembeleana tena za kushtukiza ili kutengeneza ushahidi kwani kila mtu hakuwa na imani na mwezie tena na muda mwingi ulitumika kukosoana, kugombana na kusulihisha ugomvi usioisha zaidi kuliko kukaa kwa amani na kumlea mwanetu na kusimamia kazi zetu.
Taratibu habari zikaanza kuwafikia wasimamizi wa harusi yetu ambao walijitahidi kutushauri na baada ya kushindwa sasa ikawa zamu ya wazazi wa pande zote mbili ambao nao hawakuweza lolote ile hali yetu ikawa imeshaingia damuni na sasa ni ugomvi kila kukicha.
Siku moja majira ya saa kumi jioni nikiwa natoka kazini naelekea bar kwangu nikapokea simu kutoka kwa mpelelezi wangu niliyemweka pale mtaani awe anamfuatilia mke wangu na kuniambia kila siku za weekend mida ya jioni mke wangu huwasha gari na kwenda hoteli moja ya kitalii na kule hukutana na kina baba tofauti na kisha hukaa kwa muda akiwa pia na wale kina mama mashangingi wa mjini.
Sikumjibu zaidi ya kuongoza gari mpaka ofisi za shirika moja la ndege na kupata tiketi yangu tayari kwa siku ya pili ambayo ni weekend kwenda kushuhudia nini kinatokea huko na kwa wakati huu sikuwa na mchezo zaidi ya kwenda kumfumania mgoni wangu na kuhakikisha anaipata adhabu kali ya mwaka.
Siku ya pili nikafika mji ule na kumpigia mpelelezi wangu naye akanipa habari za kutosha tukawa tumekaa sehemu tunakunywa huku tukisubiri muda muafaka wa kwenda na kumfumania.
Haikupita muda mrefu gari la mke wangu likapita kuelekea uelekeo wa ile hoteli na nikavuta subira baada ya muda kidogo huku jasho la hasira zikinitoka na nimevimba nikanyanyuka na nilipofika pale hoteloni kweli nikamkuta mke wangu akiwa amekaa kwenye meza moja na dada mmoja na baba mmoja.
Bila ya kutaka maelezo ninyanyua kiti na kumtandika kichwani mke wangu nilipona kaanguka chini nikaanza kumpiga yule jamaa na wakati huo hakuwa akiongea kitu wala kutaka kupigana nami na yule mama akipiga kelele, nilipoona nimetosheka na kipigo nataka kuondoka na mke yuko chini damu zamtoka kichani mhudumu baba yule akaniuliza ndugu yangu kwani kipigo hiki ni cha nini?
Nikiwa nataka kumtandika tena yule mama akadaikia usiniulie mme wangu akili ikaanza kunijia na kuhoji kwani huyu ni mmeo? akajibu ndio nikaanza kuona kama kuna kitu sio cha kawaida na wakati nashangaa wakasema na kila weekend huwa twakutana hapa na mkeo kwani mimi ni mfanyabisha huwa nachukua mzigo kutoka duka la huyu mama (mkeo) na kutuma mikoani.
Nikiwa naanza kuona nimekosea wakaingi kina mama wanne na wote wakashangaa kuona vile yule mama akadaikia pia na hawa nao hununua nguo kutoka kwa mkeo na hapa huwa ni sehemu ya makutano yetu kwani pia tuna umoja wetu wa kusaidiana katika hizi biashara.
Nikakumbuka wakati nataka malizia nyumba kuna hela tulikosa akasema ngoja aazime kwenye kukundi chake na kina mama wafanyao biashara pamoja. Nikaanza kutokwa na machozi nikijaribu kuwaomba msamaha na baada ya hapo haraka tukamchukua mke wangu na kumpeleka hospitali ambako hakukaa zaidi ya masaa matatu na kupoteza maisha kwa kutokwa na damu nyingi na iti kilimpiga sehemu mbaya kichwani.
Mbaya zaidi nikaanza kulia kwani kila mtu alimsifia kwa jinsi alivyokuwa mfano wa kuigwa pale mtaani kazini na sehemu zozote kwa tabia njema na hakuwa mhuni kama mimi nilivyofikiria
Kilichotokea ni kwamba mimi na yeye tulikuwa na wivu wa kufikirika na mimi nilizidi zaidi kwani kila mtu alikuwa na wivu akiamini kuwa mwenzake anamsaliti hasa kwa kuwa na watu au marafiki mwenye tabia tofauti. Lakini nimekuja kugundua kuwa wale watu niliowaona walikuwa na mahusiano ya kibiashara na sio kama nilivyofikiria mimi.
Nimeandika haya kwa kuwa najua vijana wengi wenye mahusiano au hata walio katika ndoa zao wanaugua ugonjwa huu wa WIVU WA KUFIKIRIKA kila mtu akiamini labda mwenzi wake anafanya hivi kwa kuwa ana marafiki wa aina fulani au kwa sababu ana mtu nje ya mahusiano ajambo ambalo mara nyingi huwa ndivyo sivyo.
Anza leo kujenga tabia ya kumwamini mpenzi wako na kuamini kila afanyacho kina maana katika kuwajenga na sio kuwaboa na kamwe hawezi kukudanganya zaidi ya kuaminiana ndio silaha ya mapenzi bora.
Nitafurahi kupata maoni yako juu ya huyu kijana mwenzetu
0 comments: