Ulinde sana MOYO wako usidakwe na hawa

11:24:00 Unknown 0 Comments

Kama utafanikiwa kuisoma hii na
kuitumia naamini ina uwezo wa
kuchangia katika kuyabadili maisha
yako…
Nimewahi sana kuamka siku ya leo na
kujifungia sehemu nikiwa busy nasoma
na kuzihariri baadhi ya kazi zangu.
Naupenda ukimya wa alfajiri kwani
Napata nafasi pia ya kufikiri mengi na
kuongea mengi moyoni mwangu na
hata kujisemesha kwa sauti ya
chinichini kwa imani ya kuwa Mungu
ananisikiliza.
Nimetamani nikushirikishe na wewe
uone somo ambalo nimelipata na
kujifunza pia.
Ufunguo namba moja katika kukufanya
uyafikie mafanikio yako ni kuhakikisha
unaulinda tena unaulinda sana moyo
wako.
Sasa, mtu anavyokuambia uulinde moyo
wako anakutaadharisha na kujiweka
katika hali au kukubali hali
zitakazokufanya uumizwe moyoni wako
kutokana na watu au mambo
yanayoweza kukufanya uwe katika hali
ya msongo wa mawazo ikifuatiwa na
simanzi na kasha kuumiza moyo wako
pia. Pamoja na jambo hili ya moyo
kuwa na upana wake katika kuliongelea
lakini sitataka kuingia ndani sana .
Wakati tunazaliwa tuna kuja tukiwa na
moyo ulio safi kabisa na usio na doa au
jeraha la aina yoyote ingawa
tunavyozidi kukua mioyo yetu
hubadilika kutokana na mambo
mbalimbali pamoja na watu
tunaokutana nao kila siku yani
changamoto za maisha kwa ujumla.
Najua fika kuwa hatuwezi kuitunza
mioyo yetu ile ya udogo ikakua ikiwa
hivyo maisha yetu yote, hasa baada ya
kujikuta katika hali ngumu za kimaisha
kama vile kudanganywa, kusalitiwa,
kutumika vibaya, kudhalilishwa,
kuumizwa na hata kufanyiwa mambo
magumu. Niamini kuwa unaelewa
ninachokimaanisha pia kwani hata mimi
naandika hivi nikiwa na mifano hai
hasa katika baadhi ya mambo
niliyoyapitia katika maisha yangu na
kujikuta nikiumiza moyo wangu kuanzia
suala la mapenzi, ushirikiano, kazi,
marafiki hata biashara.
Nimewahi kuyapitia hayo kwa maumivu
ya aina yake ambayo kwamwe sitataka
kuyasimulia kwani niliyasahau na
kuamini sasa mimi ni Fuledi mpya, na
kama nawe umeshawahi kuwa na
uzoefu na maumivu hayo basi tupo
sawa ila kama muda huu uko katika
hali kama hiyo niliyowahi kukutana
nayo ya kuumizwa moyoni basi kuna
mambo mawili muhimu sana
ningependa uyafahamu asubuhi hii.
Jambo la kwanza, jifunze somo lililopo
ndani ya kuumizwa huko na kuona ni
kwa namna gani utaweza kujitoa na
kurudi kuwa mzima ukiwa na moyo
wako ulio salama huku ukutumia muda
mchache kuponyesha mjeraha yako.
Kwani baada ya kuligundua hilo
utaweza kusamehe kila
lililokusababishia maumivu hayo na
kusimama tena.
Jambo la pili, hutakiwi kumwacha mtu
huyo, watu hao au hali hiyo kukufanya
uubadili moyo wako na kuwa tofauti na
ulivyokuwa hapo awali.
Naamisha nini ninavyosema hivyo?
Kama wewe una moyo wa kusaidia
watu wengine yaani mtoaji na
umeumizwa na watu ambao uliwasaidia
na wakafanya visivyo basi usiache
kutoa tena……………..ila saidia watu
wengine wenye uhitaji zaidi.
Kama wewe ni mtu unayewapenda watu
na kuna watu wanakuchukia na
kukumiza basi wewe usiache
kuwapenda…. Wapende watu wengine
wanaopendeka. Kwani kuna siku
utafanikiwa kukutana na watu
wanaoutambua na kuuthamini moyo
wako wa upendo au moyo wako wa
kujituma.
Kumbuka hili, watu wengi wamejikuta
wakifanywa kuwa na mioyo inayokataa
kuwa na usafi au usalama ndani yake
na hawawezi tena kujikubali kuwa na
mioyo isiyo na jeraha na mara nyingi
sio makosa au makusudi yao kuwa
hivyo.
Hayo yote yanatokana na magumu
waliyokutana nayo katika maisha yao
na kuwafanya kuwa na mioyo hiyo.
Kwa upande wako usijaribu kukubali
wakubadili pia. Kuna watu wengi
watakuumiza na kuukataa moyo wako
wa ukarimu na upendo, na hata
ikitokea wakakukataa basi wewe
usibadilike au kuumia kwa muda mrefu.
Hebu jifanye wewe ni Yule Yule na
tafuta nafasi ya kuangalia upande wa
pili na kuwa ana furaha zaidi kwani
kuna watu wengi bado wanakusubiri na
wanauthamini huo moyo wako.
Kwa nini ni muhimu kufanya hivyo?
Kwa sababu Mungu anakubariki wewe
kwa jinsi moyo wako ulivyo. Kama
wewe moyo wako ni wa ukarimu na
upendo, utoaji na unagawana kile
ulichonacho na wengine bila kuwa na
jambo unalolitaka au kuliwinda kutoka
kwao kama malipo ya utoai au upendo
wako kwao, basi huo ndio moyo ambao
Mungu anataka

You Might Also Like

0 comments: