HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU " Sehemu ya kwanza na ya pili
HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Soma mwendelezo wake
Kama miezi miwili hivi iliyopita nilikuwa zangu katika mihangaiko yangu nje ya jiji la mbeya.
Usiku mmoja majira ya saa nne na nusu nikiwa chumba cha kulala wageni simu ikaita mie nikajua ni waif labda anataka kunitakia usiku mwema kwani nilikuwa sijaongea nae muda huo.
Kucheki nikaona ni namba ngeni, huwa sina mazoea ya kupokea namba ngeni ila nikasema ngoja nipokee pengine ni wenyeji wangu wa eneo lile.
Duu!! Ikatokea sauti moja laini sana ya kike tena inaonyesha alikuwa anajiandaa kulala na anataka kuongea na mpenzi wake zile chati kama wewe unayesoma unazopenda kuongea na mpenzi wako kwenye simu... usijifanye kama hujui...
Basi nikapokea na kabla sijaongea neno akaanza " Hellow Darling siku yako imeishaje, nimekumis sana na baridi hii hope utajilinda?"
Muda huo nikawa nashangaa maana sina kazi za nje kwa muda tangu nilipooa many years ago. Basi nikaona hapa nisijifanye kuuliza jina lake wala anataka kuongea na nani nami nikaanza kula naye sahani moja.
Aiseee yule binti ana sauti yaani dunia nzima, basi tukaongea kama nusu saa na tukaachana huku yeye akilala na mie nikiwa sasa nawaza huyu binti ni wa wapi na anataka nini kwangu au katumwa kupata data kutoka kwangu na waif.
Usiku ule sikupata jibu na asubuhi nilipotaka kumpigia simu ikawa haipatikni. Nikaendelea na kazi zangu na ilipofika usiku mida ile ile simu ikaita tena na sasa nikaongea nae kwa muda mrefu zaidi ya jana yake.
Tuliendelea kuongea kwa siku kadhaa mara nikarudi zangu home na kila ilipofika mida ile ya kuongea nikajifanya natoka kwenda kupata bia moja kumbe ili niisikie ile sauti ya binti wa kwenye simu ambaye hata jina naogopa kumuuliza kwani inaonkena twafahamiana na mie naelewa kuwa ni WRONG namba.
Binti alikuwa mtata na kuna wakati unaweza washa TV bila kutarajia hasa sauti na utaalamu wa maneno utafikiri ana kiwanda cha kuchapisha maneno matamu ya mapenzi mdomoni mwake.
Siku moja jioni mida ileile nikiwa najiandaa kupokea simu .......
ILIPOISHIA JANA>>>>>>>>>>>>>>>>> MWENDELEZO
kupitia namba yangu nyingine ulikuja ujumbe mfupi wa maneno usemao, " Acha kuipokea simu hiyo na uondoke hapo haraka"
Kweli nikasimama na kuondoka kuelekea nyumbani huku nikiwa na mawazo mengi. Nakumbuka wakati navuka barabara kuna dereva bodaboda mmoja kidogo anikwangue tako lakini nifanikiwa kuruka upande wa pili wa barabara na kusikia sauti ikiniita.
Nikajibana nyuma ya mti ili nijue sauti hiyo inatokea wapi huku nikiwa natetemeka na mkojo ukinibana. Sauti ile ikaita tena "Fuledi!! Fuledi!!! mbona umeondoka bila kulipa bili na bia zako umeziacha?"
Aaaah shit, kumbe alikuwa ni dada aliyenihudumia vinywaji nikagundua sikumlipa fedha yake hivyo nikampa na kumdanganya nilikuwa nataka kuongea na simu moja ya siri ili nije huko....
Yule dada akanitania na kusema, " mmmh haya naona kama kawaida yako mzee wa vilongalonga ... mkeo atakufuma iwe noma" sikumjibu kwani muda huo akili ikiwa imejawa na wasiwasi na uoga kutokana na ile meseji.
Nikatembea kama hatua ishirini na kusimama kisha nikajihoji, " Yaani mimi mwanaume wa shoka, mkakamavu niogope sms ???"
Nikaifungua na kuisoma tena kwa ujasiri kisha nikafanya maamuzi magumu na kurudi bar na kuzinywa zile bia na simu nikazima.Baada ya kutosheka kunywa nikaamua kuanza kurudi nyumbani.
Kwa kuwa sikuwa na saa na nilitaka kujua muda wakati huo ikanibidi niwashe simu ili kujua muda. Kabla sijamaliza kujua kama ni saa saba na dakika ngapi iliingia meseji moja ya kutisha sana.
Kutokana na ule ujumbe nikatupa simu chini huku nikihema juu juu kama mwizi aliyeponea kiberiti cha moto. Nikakimbia hatua tatu mbele lakini nikakumbuka thamani ya ile simu yangu nikarudi.
Nikatazama huku na kule nione kama kuna mtu aliniona huku kijasho cha usiku kikinitiririka kisha nikaiokota na kuipukuta simu yangu ili nisome vizuri ile text.
0 comments: