Hujibu sala zetu
Rubani mmoja wa
ndege alipata majanga akiwa angani baada ya ndege yake kuanza kushika moto,
yeye pamoja na abiria wake wakawa hawana jinsi zaidi kutumia parachitu ili
waweze kujiokoa .
Parachuti ile
ilimpeleka rubani yule baharini na baada ya siku nzima ya kuogelea kwa bahati
nzuri baharia yule akiwa peke yake alijikuta katika kakisiwa kadogo ambako watu
hawaishi huko .
Maajabu ya kisiwa
kile kilikuwa na kabonde kadogo alikoweza kupata maji ya baridi (yasiyo na chumvi). Baharia Yule ilimbidi
atumie majani ya minazi mitano aliyoikuta pale ili aweze tengeneza sehemu ya
kujisitiri usiku pamoja na kuwasha moto (kwa njia ya kupekecha) atakao utumia
kuchomea samaki ili ale pamoja na kujilinda dhidi ya viumbe hatari waishio
majini.
Kwa uzoefu wake
wa miaka mingi katika masuala ya anga na baharini alijua kuwa eneo lile kamwe
asingeweza kupata msaada wowote kwani hakuna meli wala boti ambayo ingeweza
kufika pale na pia kwa kuwa kale kakisiwa kako katikati ya bahari ni dhairi eneo
lile hakuna meli ambayo ingeweza tia nanga hivyo meli na boti hupita kando ya
kisiwa kile tena mabli sana.
Baharia
yulealiishi pale kwa zaidi ya wiki bila ya mafanikio na kuanza kujiona kama mtu
aliyetupwa kwenye dunia yake isiyokuwa na msada wa aina yoyote ile. Kazi yake
kubwa ilikuwa ni kuvua samaki, na kuja kuwachoma na kwa kuwa kuni zilikuwa zaenda kuishia hivyo
alijitahidi kuufumbika moto na kuutumia usiku tu.
Siku moja akiwa
bondeni anajitafutia samaki na maji ya kunywa ghafla akahisi kama kuna harufu
ya moshi ikambidi arudi kwenye kiota chake mara moja.Kufika pale akashangaa
kuona upepo ulipuliza ulemotona kuunguza kuni zake na kibanda chake kwa hiyo
hata weza kula wala kuwa na moto tena.
Kwa uchungu
mwingi rubani Yule alijitupa chini na kulia huku akiwaza kuwa sasa Maisha yatakuwaje
bila ya chakula, moto na hata kula samaki wa kuchoma tena? Baada ya kuwaza na
kulia kwa muda mrefu akapitiwa na usingizi mzito na kulala zaidi ya masaa matano.
Baada ya kuamka
akiwa na uchovu na njaa akashangaa kuona kwa mbali kuna meli inakuja na baada
ya kukaribia ikatia nanga wakashuka watu na na baada ya kuwauliza walijuaje
kuna mtu pale jamaa wakasema tukiwa kwa mbali tuliona kuna moshi unafuka hapa
tukajua kuwa kuna watu wanaishi hapa hivyo tukaamua tuje tutafute maji ya
kunywa kwani tuliishiwa kwenye meli yetu.
Baada ya hapo
jamaa akapata lifti na kurudi kwao
Funzo
- · Kila jambo katika maisha yetu hutokea kwa sababu maalumu na mwisho wa siku lazima jibu litokee.
- · Mungu wetu ni mwema na hujibu maombi kwa muda muafaka na wala hachelewi


0 comments: