Unajifunza nini katika mlolongo huu?

13:26:00 Unknown 0 Comments




Fuledi katoka katika chumba cha daktari na kuchukua majibu yake ambapo amegundulika anasumbuliwa na kikohozi cha kawaida tuu.

Akiwa nje anakutana na juma, fuledi anamsimulia juma kuwa amegundulika kuwa anakikohozi wanapeana pole na kuachana.

Juma akiwa njiani anakutana na Feruzi na kumsimulia kuwa amekutana na Fuledi akitokea hospital ila inaonyesha anaumwa sana maana anakohoa kohoa sana.

Feruzi anafika kijiweni kwake anakutana na marafiki na kuwaambia marafiki wamkumbuke Fuledi katika sala zao maana jamaa anaumwa sana.

Mmoja kati ya marafiki wale aliporudi nyumbani usiku wakati wa maombi kabla ya kulala anasali sana huku akimwombea rafiki yake Fuledi apone dhidi ya maradhi makubwa ya kifua.

Asubuhi mkewe akiwa saluni anawasimulia shoga zake kuwa Fuledi kifua kimembana na hawezi hata kusimama peke yake.

Mmoja kati ya wale waliopo saluni anaenda na kumsimulia Ashura ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa Fuledi kuwa Fuledi hoi.

Ashura anasema "Nilimkanya sana Fuledi , maskini akaendeleza tabia ya ngono na sasa kashaupata ukimwi uwiiiiiiiiii"

Ashura anaenda kupima na kujikuta yupo safi lakini kwa furaha anamsimulia Mary ambaye ni mpenzi wa sasa wa Fuledi kwamba fuledi ni mgonjwa sana.

Mary anakumbuka kuwa Fuledi anaumwa kifua na kimemsumbua sana baada ya kukumbuka anaenda mbio na kuanza kumtukana Fuledi 'mwanaume huna haya wewe angalia umeniua bila sababu na sasa umenipa ukimwi"

Fuledi anamsihi watulie na waende wakapime na baada ya kupima wanajikuta wako salama na wanaendelea na mipango yao ya harusi.

You Might Also Like

0 comments: