Siku Fuledi alipohaha kuisaka Almasi
Siku moja Fuledi alitembelewa na mzee mmoja mwenye Busasra sana, na katika mazungumzo yao, mzee yule alimwambia Fuledi " mtu ukiweza pata Almasi sawa na kidole chako unaweza kuununua mkoa wako wote na ukifanikiwa kupata almasi kubwa kama kidole kimoja cha mkono wako basi waweza kuinunua hata nchi yako"
Basi Fuledi hakulala usiku ule akiwaza juu ya maajabu ya almasi na ile Furaha na Amani vikamtoweka na kuanzia hapo akafikiria kuuza mashamba yake yote na mifugo apate fedha za kuacha pale nyumbani naye achukue kiasi kilichobaki ili akaisake almasi.
Basi siku chahce baadae akafanikiwa kuuza mali zake zote na kwenda kutafuta almasi, Alizinguka Tanzania yote akakosa, akaenda nchi zote za Africa, Asia, Ulaya hata America bila kupata almasi ile kubwa, Kwa kuvunjika moyo na hasira kubwa akaamua kujitupa kutoka juu ya hotel aliyofikia na kujiua na habari hazikurudi kamwe nyumbani kuwa alikufa.
Huku Tanzania yule mkulima aliyenunua yale mashamba kutoka kwa marehemu Fuledi, siku moja akiwa katika moja ya mto upitao katika shamba lake akaona jiwe moja liking'aa sana akalisogelea na kulichukua na kwenda kulipamba nyumbani kwake.
Siku ya pili yake yule mtu mwenye busara akamtembelea yule mkulima na alipofika sebuleni akamuuliza "Fuledi amerudi?' Yule mkulima akajibu hapana. Kauliza tena "sasa nani kaleta hilo jiwe hapo?" Yule mkulima akasema ni mimi nimeyachukua katika mto uliopo karibu na shamba nililo linunua kwa Fuledi na yapo mengi.
Bila hata kukawia waliondoka kwenda kuyachukua na kuyauza na sasa ni matajiri wakubwa sana ambao wamefaidika kutoka katika shamba aliloliuza marehemu Fuledi
Funzo
1. Kama tukijenga tabia za kufanya kazi zetu tukiwa huru na amani tutagundua tunafanya kazi ndani ya mashamba yenye almasi nyingi. Na mara zote tunakaa na mafanikioyetu bila kujua kinachotakiwa ni kutumia fursa tulizonazo katika kufanikisha malengo yetu (almasi).
2. Mara zote upande wa pili huonekana kama una neema kuliko upande wako jambo ambalo mara zote huwa kinyume..usikurupuke katika mipango yako.
3. Wakati wewe unatamani hali aliyonayo mwenzako naye anatamani jinsi wewe ulivyo hivyo amini katika ufanyalo
4. Watu tusipotambua njia za mafanikio yetu huwa watu wa kulalamika na kuona kama maisha yanatuonea na hujenga hoja nyingi zenye kutufelisha
5. Mafanikio huwa hayaji mara mbili, huwa ni mara moja na mafanikio ya pili huwa tofauti na yale ya mwanzo au huwa mabaya zaidi


0 comments: