Huu sasa ni ufala
Nyambafu, mpuuzi sana huyu, huu ni ujinga
kabisa, nasema tena huu ni ukosefu wa maadili
na hofu ya kuwepo kwa MUNGU.
Nimekuwa nadate na mtoto mmoja kwa muda
mrefu sana na kuniambia yuko nje ya nchi hivyo
makutano yetu yalikuwa humu humu faceboook
na wakati mwingine kutumiana picha via
Whatsapp.
Wiki moja iliyopita akaniambia angeingia inchini
akitokea Saudi Arabia ambako amekuwa akiishi
huko kwa muda mrefu na amejiajiri.
Na makubaliano ilikuwa aje tukae chini na
kupanga kuwa mtu na mkewe na kuna project ya
kuuza simu na laptop ilibidi tuanze mapema sana.
Basi tukakubaliana tukutane maeneo ya mlimani
city leo saa tisa, basi si wajua mwanamme huwa
ni muhimu uwahi ili usimchoreshe binti tena
ukizingatia hajakaa sana hapa bongo so
asingependelea kuwekeshwa sana kivile.
Nikiwa pale mlimani nimekaa zangu Napata bia
yangu nikawa naendelea kumsubiri huku nikichati
nae na akawa ananiambia yupo jirani anakaribia.
Dakika chache akaja jamaa mmoja wa kiume na
kukaa karibu yangu, nikamwambia siti ina mtu
anakuja.
Jamaa akasema wala usijali ni nani huyo
nikamwambia ni mpenzi wangu, sasa cha
kushangaza kila nikitext naona jamaa ananyanyua
simu na kujibu……
Jasho likaanza kunitoka kwa umbali na bia
ikaanza kutoweka kichwani nikawa nahisi kama
niko kwenye movie na adui ananikaribia kunitoa
roho.
Nikiwa sijui cha kufanya jamaa akaanza kusema I
can explain…..nikamuuliza kwani wewe ndio
nachati nawe hapa?
Jamaa akajibu ndio,nikamwambia dada yako
umemwacha wapi? Jama akajibu sikia umekuwa
ukichati nami ngoja nikuambie …… !!!
sikumsikiliza nikatoka spidi mpaka home kwani
niliona ningefanya fujo pale ningeweza kusanya
watu na yeye nikamuacha akiwa anapayuka
dear!!! dear!!! dear1!!! wangu rudiiii nikuambie
ican explain!!.
Hapanina hasira na kila rafiki wa kike hapa
facebook naona kama Yule jamaa tu na pia
nilivyozoea kwenda pale Mlimani city sasa
sitaweza kwenda maana naona kila mtu atakuwa
ananiona mimi sijui vipi yaani, na pale sehemu
nilipo kunywa wananifahamu sana na wakati
naondoka niliacha sautiza vicheko?.
Yaani sijui niende kwa mchungaji nikaungame
ama nini maana naona kama mkosi
unaniandama....
naombeni ushauri marafiki wa fuledi
Asante
I hate Facebook for real
0 comments: